Uzi maalum wa vyakula vya Pwani tu

Uzi maalum wa vyakula vya Pwani tu

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
137
Reaction score
158
Wapenzi wa vyakula, habari zenu!
Hivi ukiambiwa vyakula vya Pwani, lazima kuna chakula kinachokujia kichwani haraka. Iwe ni pilau, biriani, wali wa nazi, samaki wa kupaka, urojo, viazi vya karai, vitumbua au mkate wa sinia, kila kimoja kina ladha yake!

Sasa hebu tujuane kupitia mapishi yetu. 😋

Nipe majibu ya haya maswali matatu;
  • Ni chakula gani cha Pwani ambacho unaweza kula kila siku bila kuchoka?
  • Kati ya pilau na biriani, unachagua kipi? Na kwa nini?
  • Una siri gani ya kufanya chakula cha Pwani kiwe kitamu zaidi? ni tui la nazi, viungo au ni mbinu tu za kupika?
Na kama kuna chakula cha Pwani ambacho umekuwa ukitamani kujua jinsi ya kukipika, kitaje hapa ili wadau wenye ujuzi watufundishe.

Karibuni jikoni, wakuu! Leo tunashibishana kwa maneno, lakini tusisahau kushibishana kwa mapishi pia
 
Mmmhhhh hivi kuna chakula ambacho unaweza kula daily bila kukinai?
 
Uzi utavamiwa na mijitu ya mikoani sasa hivi, kujifanya wao ndo high class wakat kwao makande na parachichi ndo breakfast
 
-Ubwabwa wa nazi,samaki wa nazi na maharage na mboga
-nachagua pilau sababu ni healthy tofauti na biryani Mchele wa basmati plus kulowekwa au kuchemsha na kuyamwaga maji kunapunguza nutrients kwenye Mchele,mafuta mengi sana,viungo vingi sana
-,Nazo,viungo,mbinu za mapishi vyote vina mchango
 
Back
Top Bottom