Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,674
- 20,689
Kuna tatizo la ubonge linainyemelea nchi. Hasa kwa watu wa kipato cha kati. Kiufupi ubonge unatokea pale ambapo unakula chakula chenye nguvu nyingi kuliko unazohitaji. Matokeo yake chakula hicho kinaenda kuhifadhiwa kama mafuta mwilini na kuleta ubonge.
Hivyo basi ili kuepuka ubonge tunahitaji kufahamu mahitaji ya nguvu mwilini na nguvu zilizomo katika vyakula tunavyokula. Kwa kawaida mahitaji ya nguvu katika mwili yanategemea mambo mengi. Kama jinsi yake, mwili wake, kazi yake, mazoezi etc. Lakini kwa wastani ni kati ya 2,000 kilocalories hadi 3,000 kilocalories. Mwanaume wa kawaida asiye active physically anahitaji kama Kcal 2,200 hivi kwa siku.
Sasa katika vyakula tunavyokula Tanzania mara nyingi, hakuna chenye nguvu nyingi kama mboga maharage. Kilo moja ya maharage ina Kcal 3,470!! Kwa siku ukila gram 200 tu za maharage tayari unakuwa umeingiza kama Kcal 700 hivi.
Maharage yana nguvu kuliko nyama ya ng'ombe. Kilo ya nyama ya ng'ombe inahesabika kuwa na Kcal 2500.
Chakula kingine tunachokula sana ni ugali. Unga wa mahindi ni moja ya vyakula vyenye nguvu hasa. Kilo moja ya unga wa mahindi una Kcal 3800. Kama ukila ugali mchana na usiku kwa kusonga jumla nusu kilo basi unakuwa umetumbukiza mwilini Kcal 1400.
Mchele, kilo moja ya mchele ina Kcal kama 1300. Unga wa mahindi una kama mara tatu yake. Pengine ndiyo maana Waasia wala wali hawanaga ubonge.
Kilo moja ya ngano ina kama Kcal 3400.
Bia. Walevi huwaga si walaji wazuri, sababu moja wapo ni kuwa bia nazo zinashibisha sana, kwa maana zina nguvu nyingi. Lita moja ya bia ina kama Kcal 450. Tena zile za kienyeji zinaweza kuwa hata mara mbili yake. Ukipiga yale mabia makubwa ya nusu lita manne ujue umeingiza Kcal kama 1,000 hivi. Wine zina kama 625 kwa chupa. Rum kama konyagi ukipiga nusu lita basi unakuwa umeingiza kama Kcal 800.
Soda zinacheza kwenye Kcal 400 hivi kwa litre.
Viazi vya kuchemsha ni kama 900kcal kwa kilo. Na mihogo ni kama 1600Kcal kwa kilo.
Vitu vyenye mafuta ndivyo vyakula vyenye nguvu kuliko vyote. Kilo moja ya karanga ina Kcal 5700. Zaidi ya mara mbili ya mahitaji ya mtu wa kawaida. Ukipiga packet mbili za karanga za 100g kila moja ujue umeingiza 1000Kcal. Unashangaa mbona sili sana!! Asubuhi napiga tu chai na karanga lakini nanenepa? Kumbe umeingiza Kcal za kutosha. Kuna zile karanga miti zinaitwa Macadamia nuts, zile kilo moja ina Kcal 7200!!! Pia kuna nazi. Lita ya tui la nazi ina Kcal 2300. Unakuta wamaza wa pwani vibonge vibonge kumbe matui ya nazi.
Litre moja ya maziwa ina Kcal 650.
Samaki hazina calories nyingi, ila siyo ndiyo tuzile kilafi.
Ubonge una madhara mengi sana kama Presha, kisukari ambacho huleta shida ya figo, macho na kifo cha mapema. Tunavyokula tuangalie sana kiasi cha mahitaji yetu ya calories kwa siku na calories zilizopo kwenye vyakula tunavyokula.
Wafilipi 3:19
19 Mwisho wa watu hao ni kuangamia, na Mungu wao ni tumbo; kwa sababu wao huyaonea fahari mambo ya aibu na mawazo yao yametawaliwa na mambo ya dunia.