Uzi maalum wa kutambua kazi kubwa na muhimu inayofanywa na wasanii Roma na Ney wa mitego

Afghanistan

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
308
399
Uzi huu ni maalum wa kuwapa maua wana hawa wawili waliojitoa peke yao kuwasemea wananchi kupitia kazi zao za sanaa.

Siyo jambo rahisi kwa msanii wa bongo kutunga wimbo wenye content ya kuisema serikali pale inapotokea hakuna mtu mmoja wa kuonya wala kuwasemea wananchi.

Kuna wasanii wengi ni waandishi wazuri sana huwenda kushinda roma na ney lakini hawana ujasiri wa kuandika ujumbe wa kukosoa au kuonya watawala,siyo wasanii wengi/wote wanaoweza kufanya hivyo.

Roma na Ney wapo front line katika kukemea mabaya yanayofanywa na serikali japo ni kama kujinyooshea mtutu wa bunduki wenyewe lakini yatupasa tuwaombee wasanii hawa wazalendo kati ya wasanii machawa wengi.

Baadhi ya nyimbo zao zinazokemea uchafu ni NIPENI MAUA YANGU wa ROMA na wimbo mpya wa NEY WA MITEGO uitwao AMKENI.

Na huu ni uzi maalum kwaajili ya kuwapongeza,kuwapa moyo na kutambua kazi yao kubwa wanayoifanya.
Binafsi hawa ndiyo wabunge bora kwa sasa na siyo wale wa dodoma.

CHUKUENI MAUA YENU KABLA HAMJAFA
 
Hilo nalo neno.
Me jamaa nawakubali miaka buku.

Achana hizo mbwa Koko za kokobichi,zenye matako mabichi wananuka maziwa mabichi kutokana na stanza zao mbichi.

Sauti zao zinaishia Kijichi.

Miamba ni hao tu.

Eti Hip Hop 4life ni NEY + ROMA

Waongea ukweli,achana na watoto wa mama.
 
Wa mitego,kazi yake ni ndogo ndo maana bado yupo nchini,yani hata uongozi wa serikal za mitaa haujawa na wasiwasi nae,
 
Hilo nalo neno.
Me jamaa nawakubali miaka buku.

Achana hizo mbwa Koko za kokobichi,zenye matako mabichi wananuka maziwa mabichi kutokana na stanza zao mbichi.

Sauti zao zinaishia Kijichi.

Miamba ni hao tu.

Eti Hip Hop 4life ni NEY + ROMA

Waongea ukweli,achana na watoto wa mama.
Jamaa wako committed kupinga uzwazwa
 
Binafsi naomba tu niwape maua yao mapema kabisa hawa viumbe.

Roma Mkatoliki, tafadhali chukua haya maua yako hapa. 🌷🌹💐

Ney wa Mitego, na wewe maua yako haya hapa. 💐🌹🌷

Aisee nyinyi mko tofauti kabisa na wale waimba Amapiano na Singeli. Hakika nyinyi ni sauti za raia wenzenu wengi wasio na sauti.
 
Jambo zuri sana hili,
Ila naona kama haitoshi kwa kazi kuwa wanazozifanya atleast na zile viewers ziongezeke kama tufanyavyo kwa wanenguaji tunaowapenda ambao likija jambo la kutetea wananchi wananyamaza wanasubiri kuitwa kwenye kampeni
 
Zero kabsa kwaiyo ww unahamasishwa na roma kwaiyo roma anakupa faraja sana ktk maisha yako
Kwaiyo unataka sema roma anakupa moyo sana kwa mattzo na maisha unayopitia
 
Zero kabsa kwaiyo ww unahamasishwa na roma kwaiyo roma anakupa faraja sana ktk maisha yako
Kwaiyo unataka sema roma anakupa moyo sana kwa mattzo na maisha unayopitia
Unaona wivu kisa jamaa kamkubali Roma na Ney wanaoimba ukweli kuhusu madudu ya serikali? Unashangaza
 
Back
Top Bottom