Kiukweli hiki ndiyo kimefanya Ney wa Mitego na Harmonize waonekane wameuharibu wimbo wa Kontawa "Champion"

Little Dreamer

Senior Member
Sep 12, 2017
178
149
Wimbo wa champion at first time niliuona kwenye status ya rafiki yangu, maneno yake yalinivutia hasa pale anaposema "tumeishi na watu wanaoamini kuwa bahati bahati zote alipangiwa Bukuku" enewei kila neno aliloimba Kontawa linavutia.

Wengi waliskiliza kipande cha Kontawa ila walipofika sehemu ya Ney wa Mitego munkari unapoa kidogo na waliskiliza wimbo Mara ya pili sehemu ya Mitego wanaipotezea, na mashabiki wengi wanahisi kuwa Mitego hakuwa na sababu ya kuingiza verse kwa ule wimbo

Ukija kwa Harmonize nae alitoa cover ila kiukweli licha ha umahiri wake wa utunzi na !ashairi na sauti back hatujaukubali sana.

Huu ni ukweli kwanini Ney wa Mitego na Harmonize waonekane wamezingua.

Kontawa maneno aliyoimba ni Yale ambayo yanawahusu watu wengi sana, na hata Kama sivyo ila yanajenga licha ambayo inatamaniwa na watu wengi. Imagine mtu anakwambia "oya mitaa niliyotoka polisi wanauza gongo😀"

Ukija kwa upande wa Harmo na Mitego, maneno waliyoingiza kwa ule wimbo yapo too personal, yaani wametumia wimbo ule kuingiza kuhusu maisha yao binafsi.

Ukweli ni kwamba watu hawavutiwi na maisha yako binafsi, Kama "niliomba nafasi ya kuimba back sikupata" everyone is going through difficulties kuliko hizo so it makes no sense kwa sisi kuanza kuskiliza matatizo yako coz nasisi tunayo yetu, wadau wa muziki tunavutiwa na stori zinazotuhusu sisi😄 masuala sijui ya nilitembea kwa mguu kutoka wapi mpaka wapi, nikaamini ntafanikiwa, so what? Sisi tunataka burudani.

Wimbo wa Kontawa naufananisha na wimbo wa Roma unaoitwa "Mkombozi" matukio aliyoimba Roma naamini sio ya kweli ila Kuna namna Fulani yanatuhusu sisi, yaani Kuna neno koja au zaidi hatimaye tunavutiwa na wimbo.
 
aysee.
Nilijua ni mawazo yangu tu,Ney amezingua kabisa humu,nausikiliza hapa toka asubuhi.
Ni bora hata asingepewa collabo kabisa.
kwanza kikifika kipande cha Ney huwa narudisha nyuma nauanza upya.

"ili sabuni zisiishe si tulinyoa madongo"
 
Hivi hayo madongo yanamaanisha Nini?

Ukija mtaani kwetu kutwa difenda, kukimbizana januari mpaka disemba
 
  • Thanks
Reactions: y-n
aysee.
Nilijua ni mawazo yangu tu,Ney amezingua kabisa humu,nausikiliza hapa toka asubuhi.
Ni bora hata asingepewa collabo kabisa.
kwanza kikifika kipande cha Ney huwa narudisha nyuma nauanza upya.

"ili sabuni zisiishe si tulinyoa madongo"
Mi nahisi huo wimbo ungenoga Kama angemshirikisha mtu Kama Roma, Stamina, au Prof May Kama angekuwa yuko kwenye afya yake
 
Mi nahisi huo wimbo ungenoga Kama angemshirikisha mtu Kama Roma, Stamina, au Prof May Kama angekuwa yuko kwenye afya yake
angemaliza mwenyewe wote tu....
"Mtaani kwetu sio,mtu aliyetoboa sana alitoboa sikio"
 
angemaliza mwenyewe wote tu....
"Mtaani kwetu sio,mtu aliyetoboa sana alitoboa sikio"
Ney anakuja ku
Kontawa nae hana punch maneno ya kitoto toto ndo anayotumia mfano mtaani kwetu sio mtu alietoboa sana katoboa sikio kaimba ushubwada mwingii tuu
Katumia figure of speech mkuu, Kontawa ni mtaalamu wa sanaa... So kwa maneno hayo kafanikiwa kutengeneza imagination kwenye vichwa vya watu ambayo mwisho wa siku Inamsisimua msikilizaji
 
Kabla wimbo haujatoka, Nay alipata bahati ya kuusikia kwenye gari ya jamaa yake anaehusiana na Kontawa.

Wimbo aliimba Kontawa peke yake na hapo Nay aliusifia sana na kuapa kuwa huu wimbo jamaa atatoboa, lakini pia akasema huyu ni msanii mchanga hivyo inawezekana asipewe sikio na kutaka yeye awemo kama kum'beba kupitia jina lake, wengi wakisikia Nay yumo watataka kujua ameimba nini...na hapo ngoma ikapikwa upya.

Kuhusu Konde alisikia goma likipepea hewani tayari na kukiri kuwa ni kali, hivyo akaomba remix ikafanyika na hapo kukawa na dhana mbili, ama jamaa ni mtu anaejiamini juu ya msanii yeyote na asifunikwe, ama anapenda kutembelea upepo.
 
Back
Top Bottom