Uzi maalum kwa madereva bodaboda (Maafisa usafirishaji)

Kazi ni kipimo cha Utu, hongereni kwa kazi
Nyie wadau jifunzeni kuwa Wasafi.

Jifunzeni kuwa Wasiri, sio nakuja kupata huduma unaanza kutoa siri za Mteja wa jana.

Punguzeni kung'ang'ania pesa za Wateja wenu kwa kisingizio cha kukosa chenji.

Jifunzeni kuheshimu watumiaji wengine wa barabara siyo kukwaruza na kugonga na kuvunja Side miror za magari na bajaj.

Jifunzeni kujali Uhai wenu kwa kuepuka spidi na kutumia vilevi muwapo barabarani.

All in all Bodaboda mnasubir kiongozi mwenye maono afute utumiaji wa bodaboda kama njia ya usafiri maaana kwenye jamii yoyote iliyostaarabika kamwe haikubaliki!
 
Karibuni madereva bodaboda kwenye uzi wenu
Ina maana kwamba Watu ambao siyo bodaboda hawaruhusiwi kuchangia chochote kile kwenye uzi huu? Anyway.

Isipokuwa ningependa kuwashauri bodaboda kwamba:-
1. Suala la Usalama Barabarani walipatie kipaumbele zaidi Namba 1 katika kazi zao.
2. Bodaboda wasikubali kutumika na Wahalifu. Kumbukumbu zangu zinaonyesha kwamba bodaboda wengi sana wamekuwa wakiuawa kinyama baada ya kugundulika kuwa kwa namna moja au nyingine, basi muuliwa alikuwa anajihusisha na Mambo ya uhalifu. Kutumika kama 'Mawakala wa Wadhalimu' katika 'kuchora Ramani' ili Watu wengine waweze kutekwa, kudhuriwa au kuhujumiwa kwa namna mbalimbali Kama vile kuwekewa sumu au kunyang'anywa pikipiki, hasa pikipiki ambazo ni mpya, kuchukua wake za Watu au kuwafanyia udalali, n k.
 
Kazi ni kipimo cha Utu, hongereni kwa kazi
Nyie wadau jifunzeni kuwa Wasafi.

Jifunzeni kuwa Wasiri, sio nakuja kupata huduma unaanza kutoa siri za Mteja wa jana.

Punguzeni kung'ang'ania pesa za Wateja wenu kwa kisingizio cha kukosa chenji.

Jifunzeni kuheshimu watumiaji wengine wa barabara siyo kukwaruza na kugonga na kuvunja Side miror za magari na bajaj.

Jifunzeni kujali Uhai wenu kwa kuepuka spidi na kutumia vilevi muwapo barabarani.

All in all Bodaboda mnasubir kiongozi mwenye maono afute utumiaji wa bodaboda kama njia ya usafiri maaana kwenye jamii yoyote iliyostaarabika kamwe haikubaliki!
Wapunguze pia na kutembea na wake za watu
 
Bodaboda wengi ni wambea sana, mambo yao ni kama wanawake.

Akikupeleka sehemu haondoki mpaka akuone unaelekea wapi.

Mimi huwaga nakausha, nikishuka kwenye boda sisogei hata hatua moja.

Basi atajibaraguza palee, atajifanya kama anarekebisha pikipiki mara hivi mara vile mwisho wa siku anajistukia anaondoka na mie ndio naondoka.
 
Kazi ni kipimo cha Utu, hongereni kwa kazi
Nyie wadau jifunzeni kuwa Wasafi.

Jifunzeni kuwa Wasiri, sio nakuja kupata huduma unaanza kutoa siri za Mteja wa jana.

Punguzeni kung'ang'ania pesa za Wateja wenu kwa kisingizio cha kukosa chenji.

Jifunzeni kuheshimu watumiaji wengine wa barabara siyo kukwaruza na kugonga na kuvunja Side miror za magari na bajaj.

Jifunzeni kujali Uhai wenu kwa kuepuka spidi na kutumia vilevi muwapo barabarani.

All in all Bodaboda mnasubir kiongozi mwenye maono afute utumiaji wa bodaboda kama njia ya usafiri maaana kwenye jamii yoyote iliyostaarabika kamwe haikubaliki!
Hoja zote uko sahihi kabisaa, nakazia.
 
Boda boda jamani hii ⛑️ ni helmet na sio elementi.
Halafu ni kwa ajili ya usalama wenu na abiria wenu.
Boda boda guy, unamwambia naomba helmet nivae anakwambia huku hamna kamata kamata dada.
Eti wanavaa ili wasikamatwe.
 
Bodaboda wengi ni wambea sana, mambo yao ni kama wanawake.

Akikupeleka sehemu haondoki mpaka akuone unaenda wapi

Suala hili limekuwa likiwagharimu bodaboda wengi sana. Wapo baadhi ya Watu wengine wamejiingiza kwenye kazi hiyo ya bodaboda lakini kiuhalisia siyo bodaboda kamili, bali ni Mawakala wa wale jamaa wavaa kaunda suti.Wapo kwenye vilinge vya bodaboda wakiwa na ajenda zao za Siri mifukoni mwao, Sasa bodaboda wengine ambao bado hawajashutukia mchezo wamekuwa wakizibeba ajenda za hao jamaa ambazo huwa wanazipenyeza kwa Siri kwa bodaboda hao na kisha kusababisha madhara mabaya Sana kwa baadhi yao ambao hawajui mambo ya undani kabisa kuhusu ajenda hizo. Wengi wao wamekuwa wakiuawa na kufa vifo vyenye utata bila ya kujulikana bayana kwa Wanandugu zao vyanzo halisi vya vifo hivyo.
Bodaboda wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa sana kuhusu suala hili.
 
Pia kuna wale wanozikwanyua side mirror kwa makusudi, sasa huwa najiuliza je, wanawezaje kuona chombo kinachokuja nyuma yao? na wanazitoa ili iweje? au wananufaika na nini kwa kuendesha bila side mirror?
 
Suala hili limekuwa likiwagharimu bodaboda wengi sana. Wapo baadhi ya Watu wengine wamejiingiza kwenye kazi hiyo ya bodaboda lakini kiuhalisia siyo bodaboda kamili, bali ni Mawakala wa wale jamaa wavaa kaunda suti.Wapo kwenye vilinge vya bodaboda wakiwa na ajenda zao za Siri mifukoni mwao, Sasa bodaboda wengine ambao bado hawajashutukia mchezo wamekuwa wakizibeba ajenda za hao jamaa ambazo huwa wanazipenyeza kwa Siri kwa bodaboda hao na kisha kusababisha madhara mabaya Sana kwa baadhi yao ambao hawajui mambo ya undani kabisa kuhusu ajenda hizo. Wengi wao wamekuwa wakiuawa na kufa vifo vyenye utata bila ya kujulikana bayana kwa Wanandugu zao vyanzo halisi vya vifo hivyo.
Bodaboda wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa sana kuhusu suala hili
Uko sahihi kabisaa.
 
Back
Top Bottom