Uzembe wa madereva watajwa kuwa chanzo kikuu cha ajali za barabarani Zanzibar

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
ASILIMIA 48 ya wahojiwa kuhusu ajali za barabarani, kisiwani Zanzibar wameeleza kwamba uzembe wa madereva ni kati ya chanzo kikuu cha ajali za barabarani, huku asilimia 27 wakisema ni kutozingatiwa sheria za barabarani.

Takwimu hizo zimebainishwa hivi karibuni Mkoani Dar es Salaam, kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu 2021, iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Kisheria Zanzibar (ZLSC), Harusi Mpatani amesema hali hiyo inasababisha kuondolewa haki ya kuishi kutokana na ongezeko la ajali huku sababu baadhi zikitokana na uzembe wa kibinadamu.

Alisema ZLSC kwa kushirikiana na taasisi ya kupambana na changamoto za vijana Zanzibar (ZAFAYCO), mwaka 2021, ilifanya utafiti kuhusu haki za binadamu, haki ya kuishi ambapo ilibaini hayo.

"Asilimia 19 walitaja mwendokasi ni chanzo cha ajali na asilimia tatu tu ya waliohojiwa walitaja ubovu wa miundombinu ya barabara, huku wengine asilimia tatu walitaja sababu nyingine na moja walisema hawajui," alisema Harusi.

Pia, Harusi alitaja ongezeko la matukio ya kujichikulia sheria mkononi huku kesi za mauaji zikiwa hazina mwendelezo na pia kwenye haki ya elimu akieleza usawa bado, na kwamba wanafunzi kwenye baadhi ya skuli hukaa chini na wengine kulazimika kutumia vyoo vichache licha ya wingi wao.

Haki ya afya, pamoja na jitihada za mwaka jana, kuna changamoto bado, kuna upungufu wauguzi na ma-specialist, ni wachache, na kusababisha wagonjwa kuja Dar es Salaam, kupata tiba.

"Dawa pia ni changamoto, kuna hospitali au wananchi walikosa dawa muhimu hii inaweza kusababisha haki ya afya kuvunjwa. Uviko-19 pia imesababisha haki ya afya kupungua kwa kuwa suala la ubaguzi lilichukua nafasi kubwa.

"Iwapo mgonjwa aliyeugua akifika hospitalini iliangaliwa huyu ni nani hakukuwa na usawa hii iliweza kupunguza haki ya afya."

Harusi alibainisha kuwa, ukatili wa kijinsia (GBV), umeripotiwa mara kwa mara visiwani humo, akisema ubakaji kipindi cha mwaka 2021, uliongezeka kuripotiwa hasa kwa watoto na wanawake.

Alisema utafiti huo wa haki za binadamu ulijikita katika maeneo tofauti, ikiwamo vurugu za makundi, haki ya watoto, haki ya jinai, upatikanaji wa haki, ajali za barabarani.

AJALI ZANZIBAR.png

Kielelezo: Chati kuonesha vyanzo vya ajali Zanzibar
 
Back
Top Bottom