Girland

JF-Expert Member
Jan 24, 2016
1,824
2,841
Habari za Jumapili wananchi wenzangu, nimekuwa nikijiuliza maana halisi ya uzalendo.

Tumekuwa tukisikia viongozi mbalimbali wakisisitiza wananchi kuwa wazalendo, na wakati mwingine wakilalamikia kinachoitwa "kupungua kwa uzalendo."

Kwakuwa JF ni home of Great thinkers iwapendeze kunijibu, je uzalendo ni nini haswa?

a) Je, uzalendo ni kuvaa tai yenye bendera ya taifa?
b) Au uzalendo ni kuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi?
c) Je, ni mambo yapi hayapaswi kufanywa na mzalendo?
d) Je, mzalendo wa taifa letu ana haki zipi?
e) Au uzalendo ni kuzishabikia timu zetu katika mashindano ya kimataifa?
f) Je, uzalendo wetu unapimwaje?
g) Viongozi wetu wanaohubiri uzalendo, wanakidhi vigezo vya kuitwa wazalendo??

Nawakaribisha nipate kufahamishwa kwa kina maana halisi ya uzalendo na mzalendo.
 
Back
Top Bottom