Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 902
- 788
Dunia ina idadi kubwa ya watu wasio na shida na wewe, na wala hawana mpango wa kugombana na wewe, ikiwa utawahakikishia kuwa wewe ni wa kawaida, mnyonge, huna mbele wala nyuma na mwenendo wa mambo unaonesha kuwa utaendelea kuwa chini.
Katika biblia, kwa mfano, tunasoma habari za Yusufu mwana wa Yakobo, kijana wa tofauti aliyesimulia ndoto zake zilizoonesha kuwa ana kitu kinachomtofautisha na ndugu zake. Ingawa Yusufu hakusimulia kwa nia ya kujionesha, matatizo yake na ndugu zake yalianzania hapo ndoto zake zilipowatia unyonge ndugu zake.
Kosa kubwa unaloweza kufanya na likakugombanisha na watu usiowatarajia ni kuonesha kuna kitu Mungu ameweka ndani yako kinachokutofautisha na wengi, na kwamba upo uwezekano wa kufanya yale ambayo wengi wanatamani kuyafanya lakini, kwa sababu mbalimbali, hawawezi kuyafanya.
Ikiwa hujajiandaa vizuri kupambana na chuki, saa nyingine kutoka kwa watu wa karibu, kuonekana ni mtu usiye na mbele wala nyuma inaweza kukuepusha na mengi. Ikiwa ni lazima simulizi la kazi unazofanya lisikike ukifanikiwa kuonesha kuwa huna mahali unaenda, uwezekano wa kujiepusha na mengi unakuwa mkubwa. Halaiki, kwa kawaida, haipendi kuona kuna mahali unasogea.