Umasikini sio laana

Umasikini sio laana

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
4,031
Reaction score
4,616
UMASIKINI SIO LAANA NAKATAA KABISA KUPITIA MATATIZO KUPATA SHIDA HAIMAANISHI YESU AMEKUACHA ..UKIPATA SHIDA HAINA MAANA..MUNGU AMEKUSAHAU AU AMEKUACHA.

Yohana 9 1-12
1 Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa.

2 Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?
3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake

Elisha alikufa kwa ugonjwa uliomwua, lakini hata baada ya kifo chake, muujiza mkubwa ulitokea pale mifupa yake ilipogusa mwili wa mtu aliyekuwa amekufa na mtu huyo akafufuka.


2 Wafalme 13:20-21.

• Ugonjwa wa Elisha: Elisha alishikwa na ugonjwa uliomwondoa uhai. Tofauti na Eliya (aliyetwaliwa mbinguni kwa gari la moto), Elisha alikufa kwa njia ya ugonjwa wa kawaida wa kibinadamu.

• Mazishi: Baada ya kufariki, alizikwa katika kaburi la pango (kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi).

• Uvamizi wa Waandishi: Wakati huo, vikosi vya Wamoabi vilikuwa vikivamia nchi ya Israeli kila mwaka wakati wa masika.


• Tukio la Muujiza: Siku moja, watu fulani walikuwa wakimzika mtu, mara wakawaona wavamizi hao wakija. Kwa hofu ya kushambuliwa, waliamua kumtupa yule maiti kwa haraka kwenye *kaburi lile lile alilozikwa Elisha na kutoroka.
• Ufufuo: Mara tu mwili wa yule maiti uliposhuka na kugusa mifupa ya Elisha, yule mtu alifufuka na kusimama kwa miguu yake.

UKIPATA SHIDA HAIMAANISHI MUNGU AMEKUSAHAU AU AMEKUACHA...soma hata habari za Yusufu ..aliuzwa utumwani MISRI na ndugu zake,akafungwa gerezani,akakaa gerezani muda MREFU..baadae akaja kuwa waziri mkuu..na hata kama asingekuea waziri mkuu bado ..kuishi ni KRISTO na kufa ni FAIDA..Stefano alipigwa mawe na akaenda mbinguni..mbingu zikafunguka..

KUPATA SHIDA MATESO,MAGONJWA...AMA UMASIKINI...SIO LAANA WALA HAINA MAANA MUNGU AMEKUSAHAU AU AMEKUACHA.

mitume waliteswa..wapo mitume walichunwa NGOZI..na hata ukisoma ufunuo MASHAHIDI WAWILI..WATAKAOKUFA KUHUBIRI..huko siku za mbeleni wakati wa ziki kuu watauwawa..ila watafufuka siku ya tatu..watapata UZIMA WA MILELE.

Mashahidi wawili watakapomaliza kuutangaza ujumbe wao, mnyama atokaye kuzimu atapigana nao. Atawashinda na kuwaua. 8 Miili ya mashahidi hawa wawili italala kwenye mtaa wa mji mkuu. Mji huu unaitwa Sodoma na Misri. Majina ya mji huu yana maana maalumu. Huu ni mji ambako Bwana aliuawa. 9 Watu kutoka kila asili, kabila, lugha na taifa wataiangalia miili ya mashahidi hawa wawili kwa siku tatu na nusu. Watu watakataa kuwazika. 10 Na Kila aishiye duniani atafurahi kwa sababu mashahidi hawa wawili wamekufa. Watu watafanya sherehe na kupeana zawadi kwa sababu manabii hawa wawili walileta mateso mengi kwa watu waishio duniani.

UFUNUOMashahidi wawili watakapomaliza kuutangaza ujumbe wao, mnyama atokaye kuzimu atapigana nao. Atawashinda na kuwaua. 8 Miili ya mashahidi hawa wawili italala kwenye mtaa wa mji mkuu. Mji huu unaitwa Sodoma na Misri. Majina ya mji huu yana maana maalumu. Huu ni mji ambako Bwana aliuawa. 9 Watu kutoka kila asili, kabila, lugha na taifa wataiangalia miili ya mashahidi hawa wawili kwa siku tatu na nusu. Watu watakataa kuwazika. 10 Na Kila aishiye duniani atafurahi kwa sababu mashahidi hawa wawili wamekufa. Watu watafanya sherehe na kupeana zawadi kwa sababu manabii hawa wawili walileta mateso mengi kwa watu waishio duniani.

11 Lakini baada ya siku tatu na nusu, Mungu akawarudishia uhai mashahidi hawa wawili. Wakasimama kwa miguu yao. Na wale waliowaona wakajaa hofu. 12 Kisha mashahidi wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikisema, “Njooni huku juu!” Na wote wawili wakaenda juu mbinguni katika wingu, adui zao wakiangalia wanavyokwenda.


NINA USHUHUDA WA KWELI

Mwinjilisti Mmoja alifungua huduma yake kanisa,Kijiji kimoja UKEREWE sasa kile kulikuwa na watu wengi wamefungwa kwa nguvu za Giza uchawi,akawaombea wengi wakafunguliwa wakapona wakampokea Yesu kanisa lake likazidi kujaza akajenga lingine kubwa akawa na waumini wengi sana..

Miongoni mwa waumini wake Tena viongozi WA kanisa lake wazee WA kanisa kulikuwa na wengine ambao wanatumiwa na ulimwengu WA Giza ni washirikina.

sasa wakakaa kikao na waganga WA kienyeji na washirikina wengine wakakaa katika ulimwengu WA Giza,wakasema huyu mwinjilisti anatuharibia wateja WETU watu wameacha kuja kwa waganga WA kienyeji wanaenda kanisani tinakosa pesa,na wagonjwa tuliowafunga na vifungo vya kichawi yeye anawaombea wanapona,na Tena maombi yake anayosali SALI..yanaharibu nguvu zetu za Giza tunapata HASARA vitu vyetu vinaharibika na nguvu yake ya maombi.

Wakasema huyu tumtengenezee UGONJWA ..wakamtupia UGONJWA WA KANSA..wakamtupia ukampata..mwinjili akaanza kuumwa KANSA mbaya.

Akaenda hospital akaambiwa anaumwa KANSA Haina tiba haiponi

Yule mwinjilisti aliposikia hivyo akamkasirikia sana Mungu..akamlaumu sana akazira..AKASEMA ya ni YESU pamoja na kukutumikia kote huku na kufanya KAZI yako,Yani umeruhusu niugue KANSA..yani..umeniacha..!?

AKASEMA kama Yesu umeniacha basi na Mimi nakuacha..nankumtumikia KIASI hiki bado unaruhusu..niteseke!?

yule mzee WA kanisa mshirikina na kundi lake la washirikina wachawi na waganga WA kienyeji wakasema tumemuweza ngoja tuone atafanya Nini sasa?

basi yule mshirikina mzee WA kanisa akaenda kumshauri mwinjilisti,kuna mtaalamu(mganga WA kienyeji namfahamu anaweza kukusaidia ,kama HUKO hospital imeshindikana kupona siyo vibaya tujaribu na kwa MTAALAMU..mana imeandikwa nisaidie na Mimi nitakusaidia(UONGO) Tena hata Hawa waganga WA kienyeji nao wanamuomba Mungu(UONGO)

Yule mwinjilisti AKASEMA SAWA kama Yesu ameniacha Mimi popone kwingine nitaenda ili TU nipone kama Yesu ameshaniacha basi popote nitakapo weza kupona kwingine popote nitaenda ,,SAWA ni peke TU kwa mganga??

alipofika kwa mganga akalala kwa mganga WA kienyeji siku nne akifanyiwa dawa..

mganga WA kienyeji na kikundi kizima Cha wachawi wakafanya sherehe ,wakasema ,huyu maombi yake yalikuwa yanaharibu sana nguvu zetu ,Leo tumempata amekuja mwenyewe kwetu..

Siku ya nne mtumishi WA Mungu akafa..

Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

Ayu 22:21
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.

KUOKOKA HAIMAANISHI KWAMBA HAUTAKIWI KUPATA SHIDA AU MATESO..

UMASIKINI SIO LAANA..

Haya mfano kanisani KWAKO amekuja mbunge kusali..ama waziri ama RASI amekuja kusali kanisani KWAKO...ama mfanya biashara TAJIRI mkubwa ..Tena labda UTAJIRI wenyewe KUPATA kwa RUSHWA ,utapeli,kutambika mizimu ama waganga WA kienyeji, dhuluma na mauaji..kumwaga damu..ama ni tajiri TU WA kurithi au ni tajiri TU WA halali TU kadiri NEEMA aliyobarikiwa..kama yule TAJIRI MPUMBAVU aliitwa NABALI mume wake ABIGAILI

Ama kuna mwingine yeye siyo tajiri ki hivyo lakini yeye kwake MAANA ya utajiri kwake ana upa MAANA tafsiri nyingine tofauti na WEWE unavyotafsri MAFANIKIO..yeye kwake maisha yake MAFANIKIO yake ni baraka nyingine TU za kawaida alizonazo AMERIDHIKA nazo na Wala hatamani MAFANIKIO hayo sio kila MTU ana tamaa ya mafanikio ya kimwili ya DUNIA hii ,wengine FURAHA Yao wamwsharishika...na hata hawazi kuhusu utajiri AMERIDHIKA tu na maisha yake ..

UTAMUHUBIRIA NINI..utamuhubiria Nini sasa..UTAMWAMBIA NJOO KWA YESU UPATE UTAJIRI na MAFANIKIO ya kimwili..wakati YEYE TAYARI anajiona maisha yake AMERIDHIKA nayo na kwake haoni tatizo..

Si KILA MTU anayekuja KUABUDU na kusali ana kuja ili kumwabudu Mungu wake ili APATE UTAJIRI..

JUA kuna makundi ya watu mbalimbali wanokuja kusali,..kuna wenye ELIMU KUBWA kuliko,ELIMU ya darasani,ELIMU ya MAISHA,elimu ya kiroho,ELIMU ya kijamii..na MAHITAJI tofauti tofauti.na UELEWA na mitazamo tofauti tofauti..

HALAFU wewe unaanza kuwahubiria POKEA UTAJIRII..NJOO KWA YESU UPOKEEE..

sio wote tunaokuja KUSALI kanisani tumekuja kutafuta MAFANIKIO YA KIMWILI YA KIDUNIA..ili tupate pesa .tuna UELEWA tofauti sana na mahitaji tofauti sana..na mitazamo tofauti sana ..

ILA WOTE TUNAMUHITAJI YESU...UKIMPATA YESU..UMEPATA VYOTE...

MBILI...sisi tunamtafuta Yesu kwa sababu wote tunamuhitaji Yesu kweli ..

SWALI..JE TUNAJUA YESU ANATAKA NINI KUTOKA KWETU...LENGO la Yesu kuja DUNIANI na kufa msalabani kwa AJILI yetu ni Nini?..

YESU hakuja kwa AJILI ya MAISHA yetu ya KIDUNIA..na hata utawala wake na malengo yake kwetu..si kwa AJILI ya DUNIA hiii..hata UFALME wake..hakulenga sana juu ya mambo ya dunia hii...TUKIJUA YESU ANATAKA SISI TIFANYE NINI..? ndio tutajua tufundishane Nini?utajua si INJILI YA MAFANIKIO YA DUNIA HII .POKEAA..POKEAA POKEEAAA..


Yohana 6
Yesu akawajibu, “Kweli nawaambieni, mnanitafuta si kwa kuwa mmeona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. Msikishughulikie chakula kiharibikacho; kishughulikieni chakula kidumucho kwa ajili ya uhai wa milele ** UZIMA WA MILELE


Yohana 3:16
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na *uzima wa milele

Luka 18:28-30
28 Ndipo Petro akauliza, “Sisi je? Tumeacha vyote tulivyokuwanavyo tukakufuata! JE TUTAUPATA NINI???

” 29 Yesu akajibu, “Nawaam bia hakika, hakuna hata mmoja aliyeacha nyumba yake, au mke, ndugu, wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, 30 ambaye hatapewa na Mungu mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya na kupata uzima wa milele katika maisha yajayo

Luka 12:23
Kwa sababu uzima ni bora kuliko chakula, na mwili ni bora kuliko mavazi.

UZIMA WA MILELE NI NIN? MANA NDIO LENGO KUU SISI TULIOMKIRI YESU TUPATE UZIMA WA MILELE NDIO SECONDRAY OUTCOME LENGO KUU KABISA.

Yohana 17:
3 Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, na kumfahamu Yesu Kristo ambaye umemtuma

Namnukuu mwalimu LUGANO ndile aliwahi kumuuliza mwalimu wake ,mwalimu mwakasege ni lipi jambo la muhimu kabisa unaloweza kunishauri katika MAISHA ya kiroho..Mwakasege akamjibu

Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia" ni kauli inayotokana na mstari wa Biblia katika kitabu cha Ayubu 22:21

UKIMJUA MUNGU UKAJUA NA AJENDA ZAKE MALENGO YAKE KWA MWANDAMU..utaelewa Nini unatakiwa kufanya na Mungu anamakusudi Gani na maisha Yako.

Yos 1:8
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Zab 53:2-3
Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu

Zaburi 119:11:
"Moyoni mwangu nZaburi 119:11:
"Moyoni mwangu nimeliweka neno lako Nisije nikakutenda dhambi."imeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi

Waebrania 11:6
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wanaomtafuta kwa bidii


Ebr 11:1-3 SUV

Basi *imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.

Ebr 10:38
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani* Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.

Mt 4.4
Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

NAjua wengine WETU tunamtafuta YESU kwa AJILI ya MIKATE...(MIKATE=RIZIKI=MAFANIKIO YA KIMWILI YA KIDUNIA..chakula Cha KIMWILI kihabribikacho..

YESU ANATAKA kutupa chakula Cha UZIMA WA MILELE.

SI KWELI KWAMBA KUOKOKA NI LAZIMA UWE TAJIRI SI KWELI KWAMBA UKIOKOKA HAUTAKIWI ..UPATE SHIDA ..hutakiwi KUTESEKA hutakiwi kuwa MASIKINI..hutakiwi kuugua au hutakiwi kufa ..au KUPATA shida..SIO KWELI.

LAKINI UZIMA WA MILELE NI HAKIKA..
 
NINA USHUHUDA MWINGINE

Nikiwa nahudumia wagonjwa hospitali,mgonjwa Mmoja mtoto WA miaka 7 amekuwa anaugua kwa muda mrefu,na bado naendelea na kliniki mbalimbali za matibabu ya hospitali.

UGONJWA wake yeye unampata pale akiwa anaenda shule TU..damu zinaanza kumtoka puani AKIINGIA TU geti la shule zinamtoka mfululizo mpaka anaishiwa nguvu,inabidi kumtia walimu wampigie simu mzazi aje ACHUKUE ampeleke hospitali .

Akirudi nyumbani akiwa njiani TU anapotoka geti la shule KURUDI nyumbani na damu zinakata kutoka puani..

Akiwa nyumbani ikafika kipindi ..akivaa TU sare za shule anataka kwenda shule zinaanza kumtoka damu puani..zinaongezeka kadiri anavyoepekea shule...akiigeuza KURUDI nyumbani na damu zinaa acha kutoka..

Hiyo hali imeendelea hivyo muda MREFU..

Ametibiwa hospitali nyingi kubwa kubwa ndani na nje ,wakimpima HOSPITALI Vipimo vyote husika HAWAONI TATIZO..

Japo ni WA Imani tofauti..ila ameharibu matibabu ya NJIA zote na kwenye MAOMBI ameenda mpaka kwa mitume na manabii wanaotumia mafuta ya upako..

nikamshauri AENDELEE na kliniki zake za damu,magonjwa mbalimbali na matibabu ya hospitali asiache

AKASEMA Yani sasa NASHINDWA hata nifanyaje ..mana wiki ijayo natakiwa nirudi Dresalaam nikaonane na Nabii WA mafuta ya upako..ana kliniki ya mitume na manabii lakini pia BADO HALI INAOENDELEA ...mpaka shule sasa ameshindwa kuendelea ..asipoenda shule anakuwa mzima kabisa...alianza kuvaa tu sare za shule akiwa anajiandaa kwenda shule shule TU. Basi hapohapo damu zinaanza kumtoka puani .au aende shule ...TU ..walimu watampigia simu mzazi NJOO mchukue mtoto WAKO damu zinamtoka puani kama Bomba..

Shule hasomi sasa .karibu mwaka mzima ..mzazi i anazunguka kutafuta msaada huku na huko bila MAFANIKIO ...Tena japo ni WA Imani ya pili .. lakini ameenda mpaka kwa mitume na manabii WA mafuta ya upako kuombewa lakini mtoto bado..hali yake AKIENDA SHULE TU ..DAMU ZINATOKA PUANI.

nikamwambia kama UNA AMINI YESU anaweza kumponya mtoto na una Nia hiyo WEWE mwenyewe,achana na mitume na manabii WA MAFUTA YA UPAKO...Mimi ninaye mchungaji wangu..kanisani kwetu..kajaribu na kwake kabla hujaenda Tena HUKO Daresalaam kwa Nabii WAKO WA mafuta ya upako..

Akaruka kwa FURAHA AKASEMA kama una mchungaji una mfahamu anaweza KUJISAIDIA nipo tayari hata Sasa hivi niende nimechoka Mimi kuzunguka hospitali kila siku..mtoto kama sasa hivi HASOMI..Sina RAHA..


nikamuunganisha kwa mchungaji WETU kiongozi..mama YETU.. Mchungaji *******

JUZI mchungaji ananipa taarifa yule mtoto sasa AMEWEZA kwenda shule Mungu ametenda..Ile hali IMEISHA...

nikamwambia Amina Yesu ni TABIBU MKUU,na Mimi nilitamani hata nimuombee lakini kama daktari natakiwa nitibu wagonjwa kwa sayansi ya taaluma ya tiba..sio kuwaombea.

NASHUKURU YESU AMEMPONYA MTOTO SASA ANAWEZA KWENDA SHULE.. kupitia mchungaji wetu kiongozi mama yetu EDA MBWAMBO...

na huyo sio WA kwanza

Mungu amtunze azidi kumuinua mchungaji wetu na huduma yake..na azidi kumlinda nankumbariki zaidi..mchungaji ************.🙏
 
UMASIKINI NI LAANA YA KIMUNGU AU KIBINADAMU(UKOO AU FAMILIA). Nahuo ndo uhalisia kuna haja ya kupambana kiroho kukataa hicho kikombe huku ukifanya kazi kwa bidii na malengo.
 
Sijasoma andiko lote lakini Umasikini ni laana ya kibinadamu na mazingira na inavunjwa kwa kuchanganya maombi,bidii na malengo.
 
Luka 16:19-31

• Yule Tajiri: Alikuwa akivaa mavazi ya gharama kubwa (zambarau na kitani safi) na kufanya karamu za anasa kila siku. Alipokufa, alizikwa na kwenda kuzimuni kwenye mateso makali.
• Lazaro: Alikuwa maskini aliyekuwa amejaa vidonda mwilini, aliyelazwa mlangoni pa yule tajiri akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka kutoka mezani pake, huku mbwa wakija kulamba vidonda vyake. Alipokufa, alichukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu mbinguni.
• Mazungumzo toka Kuzimuni: Yule tajiri akiwa katika mateso alimwona Ibrahimu na Lazaro kwa mbali, akamwomba Ibrahimu amtume Lazaro kupoza ulimi wake kwa maji, au awatumie onyo ndugu zake watano waliokuwa hai. Ibrahimu alikataa akisema wana Maandiko (Musa na Manabii) ya kuwasikiliza, na kwamba hata mtu akifufuka kutoka kwa wafu hawatashawishiwa kutubu
 
Yohana 9

1 Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa.
2 Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?
3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake
 
Marko 12:41
“Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. 42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.

43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;

44 maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia”.
 
Yohana 16:33
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu

DUNIA MNAYO DHIKI
 
Tena sasa UNAKUJa DHIKI KUU ambayo wote WANAOKATAA KUPOKEA CHAPA YA MNYAMA ...666 MFUMO WA mpinga KRISTO watapoteza kila KITU..hawatamiliki chochote na watakuwa wanawindwa watateswa prosecution,watafungwa watauwawa..HAWATAWEZA KUNUNUA WALA KUUZA ,NJAAA KALI...UMASIKINI ...

na hii DHIKI kuu inaanza soon kabla ya 2035..MFUMO WA digital ID ..MFUMO WA AI cashless cordless system..one world DIGITAL WORLD..digital currency..

WAKRISTO WOTE WATAKUWA MASIKINI NA WATATESWA..

2 Timotheo 3:12 – "Naam, na wote wapendao kuishi kwa utauwa katika Kristo Yesu watateswa."

Wafilipi 1:29 – "Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, bali na kuteswa kwa ajili yake."


1 Petro 4:12 – "Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho."


NJIA YA KUMFUATA YESU INA MIIBA...SIO STAREHE..


SHEATANI HANA UWEZO WA kuipendezesha JEHANAMU ya moto iwe nzuri..hivyo anafanya bidii kubwa kuipamba ili iwe ya kupendeza na yenye RAHA..NJIA INAYOELEKEA JEHANAMU..

DHIKI KUU IKO KARIBU KUANZA..kabala ya 2035..hapa KATIKATI pengine wakati wowote kuanzia sasa DHIKI kuu mateso..makali kwa wale wanaotaka kuishi maisha ya UTAUWA utakatifu kujitenga na MFUMO WA mpinga KRISTO (the beast system,watakao kataa kupokea chapa ya mnyama 666. yani huu mfumo WA digital world, digital ID, digital currency cashless system,one world system ya kuwekewa microchip neurolink,AI kwenye paji la uso na mkononi.

watateswa..lakini mwenye KUVUMILIA hata mwisho ndiye atakayeokolewa,MTU hataishi kwa mkate TU,...msiwaogope wauwao mwili TU wasiweze kuua na Roho Yako...mateso ni ya kitambo kidogo TU..lakini kuna UZIMA WA MILELE..

ila watakaochagua KUUPOKEA MFUMO WA beast system wao kwao NJIA Yao imepambwa anasa na starehe za DUNIA hii...NJIA YA KWENDA MITONI Haina mateso Ina starehe na anasa za DUNIA hii.
 
YESU HAKUWAHI KUSEMA UMASIKINI NI LAANA...HAYA MAFUNDISHO YA UMASIKINI NI LAANA ,MUMEYATOA WAPI..??

YESU ALISEMA WANAOTAKA KUISHI MAISHA YA UTAUWA WATATESWA..

MITUME WOTE WALITESWA..

na hata MASHAHIDI WAWILI WATAKAO kuja kuhubiri watauwawa siku ya tatu na NUSU watafufuka..

Haya mafundisho ya kwamba UMASIKINI NI LAANA YANATOKA WAPI????....!!???
 
Uko sahihi kabisa katika jambo moja kuu: Yesu Kristo hakuwahi kufundisha kwamba umaskini ni laana, na Biblia inaonyesha wazi kuwa watakatifu, mitume, na hata mashahidi wa nyakati za mwisho wanapitia mateso makubwa na dhiki, wala si maisha ya utajiri wa kidunia pekee.
Mafundisho yanayodai kuwa "umaskini ni laana" au kwamba kila mkristo lazima awe tajiri wa mali yanajulikana kama "Injili ya Ufanisi" (Prosperity Gospel).
Hapa kuna ukweli wa kibiblia kuhusu chanzo cha mafundisho hayo na jinsi yanavyopingana na maisha ya Yesu na mitume:

Chanzo cha Mafundisho ya "Umaskini ni Laana"

Wale wanaofundisha misingi hii kawaida hutumia mistari ya Biblia nje ya muktadha wake (kupotosha maana) na kuchanganya mambo yafuatayo:
• Tafsiri Mbaya ya Torati ya Musa: Katika Kumbukumbu la Torati 28, Mungu aliahidi baraka za kimwili (mazao, mifugo, fedha) kwa Israeli kama wangetii, na laana (pamoja na umaskini) kama wangeasi. Walimu wa ufanisi wanachukua agano hili la kale la kijamii na kulileta kwenye Agano Jipya bila kuzingatia mabadiliko ya kiroho.
• Tafsiri Mbaya ya Mistari ya Agano Jipya: Wanatumia mistari kama 2 Wakorintho 8:9 ("...ijapokuwa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikuwa maskini, ili ninyi kwa umaskini wake mpate kuwa matajiri") wakidai Yesu alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri wa pesa. Hata hivyo, muktadha wa mtume Paulo hapa ulikuwa unazungumzia utajiri wa kiroho na neema, si akaunti za benki.
• Falsafa ya Kidunia ya New Thought (Mawazo Mapya): Kihistoria, injili ya ufanisi ilianzia nchini Marekani karne ya 20, ikichanganya imani ya kikristo na falsafa ya kwamba ukiwaza chanya, ukinena chanya (Positive Confession), na ukitoa pesa ("mbegu"), lazima Mungu akubariki kwa utajiri.

Maisha ya Yesu na Mitume Yanavyopinga Mafundisho Hayo

Kama ulivyosema, ukweli wa Maandiko unavunja kabisa hoja hizi:
• Yesu Mwenyewe Alikuwa Maskini wa Mali: Alizaliwa kwenye hori la ng'ombe, wazazi wake walitoa sadaka ya maskini (njiwa wawili), na alisema, "Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake" (Mathayo 8:20). Kama umaskini ungekuwa laana, maana yake Yesu alilaaniwa, jambo ambalo si kweli.
• Mitume Walikuwa Maskini wa Mali lakini Matajiri wa Imani: Petro alisema, "Fedha na dhahabu sina; lakini nilicho nacho nikupa..." (Matendo 3:6). Paulo anasema alijua kuwa na njaa na kupungukiwa (Wafilipi 4:12).
• Mateso na Kifo cha Mashahidi: Kama ulivyotaja kuhusu Mashahidi Wawili wa Ufunuo 11, na mistari ya utauwa (2 Timotheo 3:12), Biblia inatabiri dhiki na mateso, si anasa na utajiri usio na kikomo.

Biblia Inasemaje Kuhusu Maskini?

Biblia haisemi umaskini ni laana, bali inaonya kuhusu hatari ya kupenda fedha:
• Yakobo 2:5 – "Je! Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu huu wawe matajiri wa imani, na warithi wa ufalme alioahidi wale wampandao?"
• 1 Timotheo 6:10 – "Maana shina la mabaya yote ni kupenda fedha..."
Mafundisho hayo unayoyaona leo yanatokana na tamaa za kibinadamu na upotoshaji wa maandiko ili kuwavutia watu wanaotafuta miujiza ya kiuchumi badala ya wokovu wa roho zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom