Hivi inawezekana vipi makombora dhaifu ya Muiran yaweze kupenya mifumo imara ya ulinzi wa anga ya Marekani bila kukumbana na kizuizi chochote.
Kama hili limewezekana basi siku za taifa teule hapo mashariki ya kati zitakuwa zinahesabika.
Kama hili limewezekana basi siku za taifa teule hapo mashariki ya kati zitakuwa zinahesabika.
Kwa yanayoendelea huko Mashariki ya Mbali, ni wazi vita inanukia.
Wasiwasi wangu kwa Marekani anaweza kupata aibu kubwa sana baada ya hii vita kama itatoka.
Hata wao walivyoanza kwa tambo za bwana Trump na vitisho vyake ni wazi anataka kucheza vita ya maneno baada ya kutambua adui yake jinsi alivyo.
Alijaribu kutafuta uasi ndani ya Irani akakosa,
Akajaribu vikwazo akashindwa,
Vitisho akashindwa pia,
Kupenyeza inteligencia yake, lakinI mara nyingi walikamatwa hata kabla ya kuanza.
Hata zile ndege zisizo onekana mawinguni ziligundulika hara bila kutegemea.
Akaona asogeze vikosi vingi karibu na nchi ya Irani. Navyo vinaonekana na madhaifu huku Wairaq waliokaribu wakimkata juzi juzi na kuamuru aondoe jeshi lake haraka.
Saudia Arabia ndipo anapopategemea tu ambao nao wameishia kujidhalilisha tu kwa kuwapa nafasi Wamarekani katika ardhi yao.
Mmarekani alimpiga Afghanistan kwa msaada wa waasi, ilimpiga Sadam kwa msaada wa waasi. Iran wapo very strong ktk umoja wao kamwe hawakumruhusu marekan awagawe.
Hii vita naona mrusi na mchina watovyojidai kukaa mbali huku wakiyafanya yao chini kwa chini ili kumbamiza mmarekan kwa mgongo wa Iran.
Kwa Syria, marekani alifyata baada ya kuwaona Warusi na Waturuki wakitanua misuli. Akaamua kulazimisha uasi. lakini kafeli, akizidisha uasi na huku warusi wanawafyeka kwa mgongo wa Assad na mpaka sasa kashindwa kuwatumia hao ISIS, hata hao ISIS wa iraq naona ameanza kuwalinda kwa kuwaamishia makazi yao.
Marekani kamwe asidhani atatawala milele hii dunia huku akiwafanyia unyama wengine, ndo anazidi kujizalishia maadui wapya ambao soon wataja kumlambisha mchanga.
Nimeanza kwa kusema Iran siyo taifa la kubezwa Mmarekani, mwenyewe analifahamu! Hivyo hawezi kwenda akashambulia kiholela kwani anajua huyu siyo mtu wa mchezo na pia anajua Mashariki ya Kati patabana kwa Marekani.
Fikiria Syiria kumembana Iraq kumebana, Pakistan juzi ndiyo kafanya mazungumzo kulikuwa kumebana kinoma na kule ndiko chimbuko la ugaidi. Afghanstan kumebana hadi akawatoa wanajeshi wake baada yakuona wanauawa akawa anatoa misaada ya kijeshi kwa NATO na safari hii nato imesema haitaki kujihusisha na ujinga uliofanywa na marekani!
Fikiria Angel Mikhael anaenda kukutana Putin kuna mipango mingi sana Marekani hawezi kuthubutu hata hivyo kwa sasa Trump atakuwa katika vikao na washauri w anchi katika maswala ya kivita, pia kumbuka ukipiga Iran ni kuwa umewasha Israel hivyo yote haya yanaangaliwa kwa mapana.
Hivyo kwangu naona ni propaganda za kisiasa Trump akitafuta kuungwa mkono na washirika wake ili aanze chokochoko.