Uwezo wa Roma Mkatoliki kutunga na kuandika nyimbo za harakati za kisiasa na utawala ni mdogo mno

Huyu kijana anauwezo mdogo wa kutunga na kuandika nyimbo kufikisha ujumbe wa aliokusudia. Badala yake amejikita kwenye hisia, mihemko na nadharia. Ila ukikaa na kusikiliza hakuna ujumbe unaoleweka.

Hawa vijana wangejifunza kwa majabali ya muziki waliotangulia akina marijani rajabu na wengine. Nimepata muda wa kusikiliza wimbo wa Roma mkatoliki sijaona cha maana wala meseji za kueleweka zaidi ya upayukaji tu. Nashangaa Kwanini watu wamehamaki wakati ni wimbo wa kawaida tu uliojaa hisia kuliko uhalisia

Mimi nilikuwa mfuasi wa nyimbo za Mr.Sugu, Profesa Jay, Solo thang na Afande Sele kwenye upande wa nyimbo za kufoka foka

Hawa wanamuziki wasasa sio wabunifu ni muda sasa tuwachoke
We MWENYEWE POST YAKO YA MUHEMKO TUACHE.. WASALIMIE LUMUMBA.
 
Back
Top Bottom