Uwekezaji Simba: Wako wapi wawekezaji wengine wawili waliotajwa kwenye kanuni za Tume ya Ushindani?

Huu mjadala unatakiwa kujadiliwa bila kuweka ushabiki, kabla ya maswala ya uwekezaji kuanza zilitungwa sheria na sheria zilisema timu zote zilizoanzishwa na wananchi zinatakiwa ziuzwe hisa si zaidi ya asilimia 49 na katika uuzaji wa hisa wawekezaji wanatakiwa wasipungue 3. Kinachofanyika Simba kitakuja kuleta vurugu baadae kwa sababu kuna viongozi na wanasiasa wamejiingiza kuleta mashinikizo ili sheria zivunjwe, Mwakyembe akiwa waziri wa michezo aliruhusu Simba iwe na mwekezaji mmoja huku akijua kuwa sheria haisemi hivyo baada ya tume ya ushindani kuweka ngumu kina makamba , kitila Mkumbo na wabunge wengine walijiingiza kushawishi mo apitishwe bila kujali sheria inasemaje.
Ikitokea mwanasimba akaenda mahakamani ni wazi taratibu hizo zitatenguliwa kwani mwekezaji pekee aliyepitishwa na mkutano mkuu wa Simba ni Mo dewji hao wengine wanaootajwa hawajawahi kupitishwa na kikao chochote.
 

HUU NI UKWELI MCHUNGU.

AKITOKEA MZEE KILOMONI MMOJA KWENDA MAHAKAMANI, MO ATAANGUKIA PUA KWEUPEE
 

WAWEKEZAJI WATATU NA KUENDELEA ndo Sheria mkuu.

Tume ya Ushindani hawajatoa Tamko la kubariki hili. Ni kauli za Mo tu ndo zimezagaa, Na anasema wanaendelea kukamilisha taratibu kadhaa kwa tume ya ushindani.

Subirini tu Muone hii Movie
 
Wahini CAS mkashitaki ili Mo anyang'anywe hizo hisa. Simple.
 
Wahini CAS mkashitaki ili Mo anyang'anywe hizo hisa. Simple.
Tusubiri wao waweke hao Wanahisa Watatu.

Ili tuige toka kwao.

Sasa hivi ni maneno ya mkosaji tu hapo.

Wafanye uwekezaji huo sahihi, na tuone faida yake ili waweze kukosoa aliyekosea.

Mi kwa uzoefu wangu wa Biashara ya Mpira wa Miguu, sijawahi kuona timu moja ina wawekezaji watatu.

Mazembe fc, Katumbi
Man City, Mwarabu.
Hivyo hivyo kwa
Mamelod Sundawn
A.S Vita
Manchester United
AC Millan
Chelsea,
Nk.
 
FC Bayern Munich ... ina wawekezaji watatu.
1. Adidas.
2. Audi.
3.Allianz SE.
 
Ziishe ziende wapi sasa?.. Hivi unajua hata maana ya hisa?.

How do stocks work?​

Companies sell shares in their business to raise money. They then use that money for various initiatives: A company might use money raised from a stock offering to fund new products or product lines, to invest in growth, to expand their operations or to pay off debt.

Huku ndo zinapoweza kwenda. Nani anawakaririsha Fyongo Mkuu. Kuna mtu anasema Mo kaongeza mtaji tu na hautumiki. Dah

Nahisi kuna wengine mambo ya hisa wameanza kuyasikiasikia sana wakati huu wa mchakato wa mabadiliko. Nao wanachambua kama mpira
 
Simba SC ni timu ya familia ya Mo Dewji

Anaweza kufanya chochote atakacho, hata makombe huwa anayahifadhi ofisini mwake badala ya klabuni, na anapenda hivyo.

Well, hayo sio ya msingi...la msingi ni kuheshimu katiba na sheria za klabu, kama imetokea hivyo solution ni IPI? Nani wa kumpenalize Mo Dewji?

Wengine ni vi mikia tu
 
Mchakato ukirudiwa Mo hatachangia tena, ataona ni magumashi na hivi ameshajipublish sana mitandaoni
 

Ogopa saba Collabo ya Masikini na Tajiri
 
Tume ya Ushindani hawajatoa Tamko la kubariki hili. Ni kauli za Mo tu ndo zimezagaa, Na anasema wanaendelea kukamilisha taratibu kadhaa kwa tume ya ushindani.
Sasa kama Tume haijatoa tamko, wasiwasi wako ni nini? Na kama anasema anaendelea kukamilisha taratibu kule Tume, tatizo liko wapi?
 
Hajakamilisha taratibu. Wameundaje Bodi?

Na yeye amekuwaje Mwenyekiti wa Bodi kwa miaka 3?

Nijibu kwa taratibu na kanuni plz. Usifokefoke
Sasa kama Tume haijatoa tamko, wasiwasi wako ni nini? Na kama anasema anaendelea kukamilisha taratibu kule Tume, tatizo liko wapi?
 
Mbona mnapenda kuendeshwa na maneno ya vijiweni? ni lini bakhresa alitaka kuwekeza simba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…