dem boy
JF-Expert Member
- Nov 4, 2016
- 5,852
- 14,519
Ndugu Mo Dewji, Salim Tryagain na Mutaza Mangungu, Nini mnaweza kutuambia mashabiki tukawaelewa baada ya leo kuhitimisha msimu Simba ikikosa makombe yote? Simba imekosa ubingwa wa ngao ya Jamii, imekosa ubingwa wa Mapinduzi, imekosa ubingwa wa ligi kuu, imekosa ubingwa wa Klabu Afrika. Na sasa tumebakiwa na Super league tu. Iwe mwanzo na mwisho kuleta utapeli katika usajili wa wachezaji!
Ni ukweli usiopingika wachezaji wa Simba 80% hawana sifa ya kutumikia klabu hii, usajili msimu huu ulikuwa ni wa kitapeli tangu klabu yetu ifanye mageuzi ya kimfumo katika kipindi cha miaka kumi hivi iliyopita. Tuliletewa wachezaji magalasa na free agent wengi ili kuziba macho ya wanasimba kisa chaguzi.
Lakini ni ukweli mtupu kwamba Mwekezaji wetu Dewji alituchuuza akashindwa kutos pesa ya usajili, Amekuja kurudi bada ya kuona timu imefuzu kwenda makundi ya klabu bingwa kwakuwa huko kuna maokoto. Ukweli huu mchungu anatakiwa kuambiwa wazi kwamba Simba sio familia yake anayoweza kuifanyia chochote cha ajabu na cha mzaha askosolewe. Huyu alisusa tumu akaenda kwenye ngumi. Alipoona timu imefuzu kimiujiza tu akarejea.
Hebu tukubaliane jambo moja, Mohamed Dewji anamiliki hisa 49% kama hajazilipia kwanini milango isifunguliwe ziuzwe kwa mwekezaji mwingine atakayeweka mzigo wa kutosha na tukaepuka hii susasusa ya kimanyema? Kama hilo ni gumu kuuza hisa kwakuwa alishalipia kwa njia ya kiini macho cha hundi, Basi tukubaliane hisa za wanachama 51% zitolewe kiasa ziuzwe kwa mwekezaji mwenza (kama mwanachma) ili tuache kuonekana tumeshikilia hisa 51% wakati hatuna hata hela ya usajili wala ya kuendeshea klabu. Zinafaida gani kuonekana wanachama tuna hisa hizo ikiwa hazileti pesa?
Viongozi wa Simba acheni urasmu, fungueni milango ya wadau wapya waingie katika klabu waweke pesa. Lakini vilevile Serikali Wizara ya Michezo na Wizara ya Biashara na Uwekezaji, Acheni Urasmi, Simba na Yanga sio mali ya kisiasa, wala sio vitengo vya ccm, Vilabu hivi dunia ya leo ni Biashara ya uwekezaji, Malizieni mchakato wa mabadiliko. Simba haistahili kusajili mchezaji wa 100M au 150M, wachezaji wa bei hizo wanastahili Namungo, Azam, na Ihefu huko. Simba hadhi yake ni mchezaji wa 400M na kuendelea
Na YN
UNAMWAMBIA YN NINI KWA MAONI HAYA JUU YA KLABU YAKE(YENU)