Ni muda muafaka sasa kwa Tume ya Ushindani Tanzania FCC kulimulika swala la uwekezaji wa Mo Dewji Simba

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Wakuu Simba ni brand, siyo kikundi cha wahuni, na kila kilichopo Simba ni mali ya umma (wanachama). Hivyo kumpatia mtu hisa asilimia 49 kinyemela ni sawa na uhalifu.

Tume ya ushindani unapaswa sasa kuingilia kati hili suala la uwekezaji la huyu bwana, maana inavyoonekana mazingira yake ni ya kihuni.

Simba watuambie kama wameingia mkataba wa zaidi ya shilingi bilioni 20 na M bet inakuwaje umiliki wa asilimia 49 uwe na thamani ya bilioni 20 tu?

Lakini pia je Mo Dewji ni mmiliki wa kilabu ama mdhamini, maana jezi za kilabu zimejaa matangazo ya kampuni zake tanzu.

Wakuu ya kuzungumza ni mengi ila kwa hapa hapana, jamaa achunguzwe na watuambie je, ni kweli Klabu ya Simba inastahili kumilikishwa kwa mtu kwa thamani ya 20 bilioni?

NB. Ujenzi wa kiwanja wanachangia wanachama na Mohamed Dewji ameshaupatia tayari jina lake et MO Arena. Aibu kubwa hii watanzania.
 
FCC wanajuwa Simba inamilikiwa na serikali, Mo Dewji ni muendeshaji wa muda tu.

Hakuna mtu binafsi atakuja kumilikishwa Simba au Yanga labda serikali iamuwe kuziachilia.

GSM wanalijuwa hili vizuri ila Mo Dewji hajui kitu anadhani anaweza kuja kuimiliki Simba, haitakaa itokee.

Simba na Yanga zinamilikiwa na serikali kwa 100% najuwa hili litakushangaza au utahisi Mimi hamnazo lakini huu ndio ukweli wenyewe.
 
FCC wanajuwa Simba inamilikiwa na serikali, Mo Dewji ni muendeshaji wa muda tu.

Hakuna mtu mbinafsi atakuja kumilikishwabSimba au Yanga labda serikali iamuwe kuziachilia.

GSM wanalijuwa hili vizuri ila Mo Dewji hajui kitu unadhani anaweza kuja kuimiliki Simba, haitakaa itokee.

Simba na Yanga zinamilikiwa na serikali kwa 100% najuwa hili litakushangaza au utahisi Mimi hamnazo lakini huu ndio ukweli wenyewe.
Angalau mkuu umetoa maoni ya kueleweka Kuna Mjinga mmoja hapo juu anasema FCC hawahusiki kufatilia mambo ya uwekezaji Simba.
 
Angalau mkuu umetoa maoni ya kueleweka Kuna Mjinga mmoja hapo juu anasema FCC hawahusiki kufatilia mambo ya uwekezaji Simba.
FCC ndio wanaokwamisha mchakato wa Simba kuendeshwa kisasa, sababu ni hiyo Simba ni timu ya serikali hawawezi kuikabidhi kwa watu binafsi.

Serikali iliipora Simba kutoka kwa Waarabu Sunderland na kuipa jina la kawawa Simba wa Vita na Karume ndio alitowa pesa ya Kujenga makao mkuu ya Simba Msimbazi kama alivyotowa pesa za Kujenga makao makuu ya Yanga.
 
Katika hili mnapenda kuzungumzia upande wa muwekezaji TU mnasahau pia wanachama nao inatakiwa waweke 51%

Tukuulize mleta mada je 51% za wanachama pesa zimewekwa wapi?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Sijui niandike namna Gani ili usifikiri nimedharau hoja yako ila ungeulizia kidogo Kwa watu wenye uelewa wakuelimishe kuhusu maswala ya hisa ila Kwa kifupi wanachama walikuwa wanamiliki Simba Kwa Asilimia 100 hivyo hawahitaji kutoa hata Senti Tano ila wanaweza kuuza hisa
 
Mo Dewji alinishangaza sana kusema kuwa "nimemwambia Mugunda nikutane Naye ili nisikilize" nilishangaa sana uenyekiti wa bodi alimpatia mtu kinyemela. Hili jambo halikubaliki.
 
Sijui niandike namna Gani ili usifikiri nimedharau hoja yako ila ungeulizia kidogo Kwa watu wenye uelewa wakuelimishe kuhusu maswala ya hisa ila Kwa kifupi wanachama walikuwa wanamiliki Simba Kwa Asilimia 100 hivyo hawahitaji kutoa hata Senti Tano ila wanaweza kuuza hisa
Mkuu hisa hizo hazikuuzwa Bali ujuaji wa Mo uliwapumbaza viongozi wa wakati huo. Ndiyo maana mpaka leo unasikia Mo hajaweka hata Shilingi mia kwenye account ya Simba isipokuwa anatoa pesa kinyemela maana Simba inamfaidisha kupitia matangazo.
 
Mnaangalia Simba leo, wakati mchakato umeanza 2015-2016
Wakati huo Simba haina chochote zaidi ya jengo lililochoka KKOO
 
FCC ndio wanaokwamisha mchakato wa Simba kuendeshwa kisasa, sababu ni hiyo Simba ni timu ya serikali hawawezi kuikabidhi kwa watu binafsi.

Serikali iliipora Simba kutoka kwa Waarabu Sunderland na kuipa jina la kawawa Simba wa Vita na Karume ndio alitowa pesa ya Kujenga makao mkuu ya Simba Msimbazi kama alivyotowa pesa za Kujenga makao makuu ya Yanga.
Umemaliza mkuu, umeongea mambo ya muhimu sana.
 
Fafanua mkuu serikali inamiliki kivipi?
Do your home work, ukitaka ukweli utakuja kuujuwa fuatilia kuanzia usajili wa Simba na Yanga utapata ukweli.

Upande wa Yanga GSM wanajuwa kila kitu ndio maana wamemuweka Eng Hersi asimamie maslahi yao wanajuwa vizuri Yanga haiwezi kumilikiwa na watu binafsi.
 
FCC wanajuwa Simba inamilikiwa na serikali, Mo Dewji ni muendeshaji wa muda tu.

Hakuna mtu binafsi atakuja kumilikishwa Simba au Yanga labda serikali iamuwe kuziachilia...
We jamaa kweli hamnazo, serikali ipi hiyo inayomiliki Simba na Yanga? Kuna timu mojawapo kati ya hizo au zote inayopata ruzuku kutoka serikalini?
 
We jamaa kweli hamnazo, serikali ipi hiyo inayomiliki Simba na Yanga? Kuna timu mojawapo kati ya hizo au zote inayopata ruzuku kutoka serikalini?
Wewe ni mtoto Mdogo sana, huna ulijuwalo.

Ruzuku ya serikali inatolewa na wezi wanaoibia serikali kodi hao unaowaona GSM na Mo Dewji.

Reginald Mengi alikuja macho juu Yanga baada ya kuujuwa ukweli akakaa pembeni.

Zamani kwa watu wa Mwanza ukitaka kadi ya Yanga unachukulia kwenye ofisini za Toto Africa Mwanza, kuna mengi usiyoyajuwa ukikua utaacha huu ujinga wa kuwaita hamnazo watu waliokuzidi akili kwa mbali.

Kama upo karibu na Michael Wambura muulize mbona siku hizi hana kiherehere cha kugombea vyeo Simba?
 
Do your home work, ukitaka ukweli utakuja kuujuwa fuatilia kuanzia usajili wa Simba na Yanga utapata ukweli.

Upande wa Yanga GSM wanajuwa kila kitu ndio maana wamemuweka Eng Hersi asimamie maslahi yao wanajuwa vizuri Yanga haiwezi kumilikiwa na watu binafsi.
dare to talk openly
 
Back
Top Bottom