rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 14,925
- 19,618
Huu mjadala unatakiwa kujadiliwa bila kuweka ushabiki, kabla ya maswala ya uwekezaji kuanza zilitungwa sheria na sheria zilisema timu zote zilizoanzishwa na wananchi zinatakiwa ziuzwe hisa si zaidi ya asilimia 49 na katika uuzaji wa hisa wawekezaji wanatakiwa wasipungue 3. Kinachofanyika Simba kitakuja kuleta vurugu baadae kwa sababu kuna viongozi na wanasiasa wamejiingiza kuleta mashinikizo ili sheria zivunjwe, Mwakyembe akiwa waziri wa michezo aliruhusu Simba iwe na mwekezaji mmoja huku akijua kuwa sheria haisemi hivyo baada ya tume ya ushindani kuweka ngumu kina makamba , kitila Mkumbo na wabunge wengine walijiingiza kushawishi mo apitishwe bila kujali sheria inasemaje.
Ikitokea mwanasimba akaenda mahakamani ni wazi taratibu hizo zitatenguliwa kwani mwekezaji pekee aliyepitishwa na mkutano mkuu wa Simba ni Mo dewji hao wengine wanaootajwa hawajawahi kupitishwa na kikao chochote.