Uwe makini ujipende uwe na misimamo na malengo kuna siku rafiki uliemuamini atakukimbia akipata njia ya maisha

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,432
11,101
Binadamu ni kiumbe mwenye hila, uongo, unafiki, ubinafsi, rafiki ulienza nae sie utakaemaliza nae kuna siku atakusaliti, kuna siku ataacha kuwa rafiki akipata njia nzuri ya maisha kukuzidi au kulingana na wewe na hutaamini, kuna mtu uko nae karibu unamuona rafiki kumbe ni adui yako na mshindani wako, wengine wakati anahangaika namna ya kuiba nyota yako ya kieleimu, kifedha, kibiashara, kupendwa na watu.

Anza kujipambania mapema usimpe rafiki aslimia hata 50 ya kumwamini jipe homework ya kumtafiti na umjue vizuri. Endapo ukawa rafiki mchawi au mshirikina na wewe ni debe tupu hujui chochote utaumia maisha yako yote.

Huyo rafiki atakukimbia baada ya kuangamiza nuru ya mafanikio yako yote. Utashangaa na hutaamini na ndio itakuwa imeisha hio. Pambana uwe Mwamba uwe shujaa uwe gaidi jipange, jiulize rafiki unampa nini na yeye anakupa nini je be yeye maisha yakoje palipo na yeye unapata nini.

Ipo siku wanaokuzunguka nyakati za furaha hawatakuwa na wewe wakati wa shida na hawata hali kuhusu wewe. Ulizaliwq peke yako jipange mambo yako mengi iwe Siri yako.

Jifunze uwe na marafiki wa aina nyingi kwenye nyanja mbalimbali. Friendship with diversity ndio mpango mzima. Ni ijumaa tena huku Gaza watu wanalia na kusaga meno.

Tuwe makini wakati wote.

Mobare nangai

Wadiz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom