Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,820
- 4,572
Mfalme Charles III wa Uingereza anatarajiwa kupatiwa matibabu ya tezi dume wiki ijayo.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, Jumba la kifalme la Buckingham limesema leo Januari 17, 2024 kuwa Mfalme atapitia "utaratibu wa marekebisho".
Shughuli za kijamii za mzee huyo wa miaka 75 kwa Taifa zitaahirishwa kwa muda mfupi hadi atakapopata nafuu, ilisema taarifa kutoka kasri la kifalme.
Tangazo hilo linakuja muda mfupi baada ya kutolewa kwa taarifa kuwa binti mfalme wa Wales, Kate yuko hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.