UWAZI: Mfalme Charles III wa Uingereza kutibiwa tezi dume wiki ijayo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,818
4,569
Mfalme Charles III wa Uingereza anatarajiwa kupatiwa matibabu ya tezi dume wiki ijayo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, Jumba la kifalme la Buckingham limesema leo Januari 17, 2024 kuwa Mfalme atapitia "utaratibu wa marekebisho".

Shughuli za kijamii za mzee huyo wa miaka 75 kwa Taifa zitaahirishwa kwa muda mfupi hadi atakapopata nafuu, ilisema taarifa kutoka kasri la kifalme.

Tangazo hilo linakuja muda mfupi baada ya kutolewa kwa taarifa kuwa binti mfalme wa Wales, Kate yuko hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.
 
Wafalme hawaumwi mara Kwa mara ndio maana akiumwa inakuwa habari kubwa

Kwa Maskini shida Leo anakohoa,kesho anaharisha ,keshokutwa kichwa kinaumu ,mtondogoo anaona mawenge mawenge vitu vinayambaa mwilini nk
 
Wafalme hawaumwi mara Kwa mara ndio maana akiumwa inakuwa havari kubwa

Kwa Maskini shida Leo anakohoa,kesho anaharisha ,keshokutwa kichwa kinaumu ,mtondogoo anaona mawenge mawenge vitu vinayambaa mwilini nk
Mfalme hata ikitokea akajamba mara mbili kwa siku lazima Afya ichunguzwe!!

Sisi huku hata ukijamba mara 72 ni sawa tu! Ndo maana hata ukizidiwa hakuna matangazo
 
Mfalme Charles III wa Uingereza anatarajiwa kupatiwa matibabu ya tezi dume wiki ijayo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, Jumba la kifalme la Buckingham limesema leo Januari 17, 2024 kuwa Mfalme atapitia "utaratibu wa marekebisho".

Shughuli za kijamii za mzee huyo wa miaka 75 kwa Taifa zitaahirishwa kwa muda mfupi hadi atakapopata nafuu, ilisema taarifa kutoka kasri la kifalme.

Tangazo hilo linakuja muda mfupi baada ya kutolewa kwa taarifa kuwa binti mfalme wa Wales, Kate yuko hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.
Allah akbabar. Ilikuaje akapata hayo maradhi hana walinzi? Au walisinzia?
 
Back
Top Bottom