Uwanja wa wanasaikolojia, (Para-profesional & Professional Psychologists) wote tukutane hapa

mkuu unaweza kutupa dondoo au kwa undani zaidi kuhusiana na lugha ya mwili..?
Sawa mkuu ,,

Lugha za mwili au maarufu kama facial language/expressions ni lugha haswa zitokazp usoni hutumia macho, mdomo , paji la uso tabasamu kukunja sura na mengine mengi ,lengo la hizi lugha huwa ni kuonyesha kilicho ndani ya fikra za mhusika na Mara nyingi hutoka unconsciously kwa maana ya kuwa MTU hujikuta ka express feelings zake kupitia facial language

Ni rahisi MTU kuzuia kusema kwa mdomo kuliko kuzuia baadhi ya body language!

Mistakes are mine, karibu sana na wengine kama wapo karibuni msaidie
 
Mfano mtoto wa miaka 2 -4
-anpenda kucheza sana
-anajifunza kutembea
-kila anachokiona anataka akimiliki kuwa ni kitu chake
-anajifunza kuongea kwa kurudia maneno yanayotamkwa na mtu mwingine
- umri huu Watoto wanakuwa watundu na hawasikiii
-wanaharibu vifaaa mbalimbali vya nyumbani
-wanaonyesha upendo Kwa mtu Fulani ktk familia

Kwa kutumia saikolojia kwenye suala LA umri unaweza kubaini matendo ya mtt wako na kuweza kukabiliana nayo
Sawa kabisa mkuu huu umri uliotaja hapa ni umri sumbufu sana kwa walezi

Mfano katika hii age unakuta memory ya mtoto iko inaruhusu na INA hamu sana ya kujua kile anachokiona kwa maana kuwa mtoto anapenda kujifunza sana kwa matendo kuliko kuongea

Hii hufanya walezi wasioelewa kutumia adhabu sana kuwaajibisha watoto lakini huwa ni halo ya kawaida na kinachotakiwa ni kuwa na tahadhari ili alidhurike
 
KUCHANGANUA HULKA ZA WATU KWA KUTUMIA NYUSO ZAO.

Njia rahisi ya kutathimini hulka ya MT, kwako wewe mwenyewe huwenda isikupe majibu sahihi maana sio rahisi kujifahamu tabia yako kwa kiwango cha kutosha

USO MPANA, au kwa namna nyingine ni *uso mduara* kundi la watu wa nyuso kama hizo n waaaminifu, wawazi, sio wabaguzi na wanawiwa sana na kuthamini wenzao hata kwa muonekano wao wa usoni, ukiwatazama sana usoni ni kama wanasema *karibu* maana tabasamu zao hubebwa na uso mzima. Hawa watu ni wepesi hata kufikika yaani wanasikiliza na kushare na wengine kiurahisi "which in turn makes socializing easy for them" ni wazuri kutunza SIRI na ni wanauwezo mkubwa kwenye mambo mengi.

KINYIME CHA UZURI WAO, kama amegombana na MTU mara kadhaa hubaki na mwonekano wa amani sana na wanaonekana kuwa tayari kukubaliana na kushindwa ugomvi au upinzani, ni jambo jema wao kuwa hivo lakin wakati mwingine huweza kuonesha udhaifu mkubwa kwa sababu huonesha kutosimama katika kujali,kujilinda na kujitetetea.

USO MREFU,: ukionana na MTU wa aina hii tambua wana hali furani ya ubinafsi (self-preservation) kama kujipendelea katika mambo kadha wa kadha ambayo pengine ana share na wengine,hawa watu pia husemekana wanaweza uongozi pia wanaweza kuchukuwa maamuzi bila kuhitaji msaada wa watu wengine na pia ni watu wa kufikilia kiundani sana, (deep thinker)

ISIPOKUWA , wanapenda ku control au kuendesha na kujali maisha yao sana kuliko ya watu wengine mfano akiwa kiongozi au mtegemewa sehemu furani kitu ambacho huwasababishia sonona au msongo wa mawazo na hata watu wanaowazunguka kwa sababu ya lawama.

PUA PANA, ni watu ambao huonekana wanaishi au hupenda kuishi mfumo wa maisha yaliyo nyooka (tengemaa) wana uwezo mkubwa wa nguvu wengi wao, na wanapenda sana kujihusisha na mazoezi, wanapenda kutafiti vitu vingi na kuwa na uwelewa wa mambo wengi kutoka katika tamaduni mbalimbali ,,shida yao kubwa ni kuwa wanapenda sana mabadiliko lakini huwachukuwa mda mwingi sana kuchukuwan maamuzi hata katika vitu vizuri wanavyovitamani wao, wanapenda kutoka sehemu mbalimbali ,kusitasita huko huwafanya kukosa fulsa nyingi sana zinazokuja dhidi yao na ikitokea wakachukuwa maamuzi ni watu wa kufanikiwa.

PUA NDOGO, hawa sifa yao kubwa ni watu wanaojari kwa wepesi sana,,wanajikuta kwao ni rahisi sana hata kusaidia watu bila hata kutafakari kwa undani (They find it easy to put themselves on others shoes before judging the other person) kwa sababu yao hiyo ya kujari jari hujikuta wana tengeneza marafiki pia kwa haraka,lakin pia tabia yao hiyo huzalisha tena tabia nyingine kwao ya kuwa na wepesi wa kuhitaji zaidi mambo watakayoyaona kwa yule ambae wanatoa msaada au kuonana nae,hivyo ni kuwa nao makini.

WATU WENYE PAJI NDEFU ZA USO, au uso mrefu,hawa n watu ambao kuna urefu mkubwa kutoka katika macho yao hado kwenye mstari wa nywele zao kichwani, inasemekana na kuonekena wana uwezo mkubwa wa kiakili,na kufanya mambo yao kwa kujiamini pia kwa umakini sana. (These people are highly intelligent, contain high level of confidence and are very analytical when approaching things.) sio watu wa kususia susia lakin hujiridhisha na jambo au hali kabla ya kuchukuwa maamuzi ambayo huyafanya kwa kutumia maono yao ,,na ndo maana kutokana na hali hii na hiyo tabia yao huwafanya wawe waoga na hofu ya mambo *wanachoogopa na kuhofia ni kushindwa Yale wanayokusudia yawe licha ya kuwa wanajiamini sana na sio watu wa kushilikisha saana wengine.

PAJI FUPI YA USO, hawa tabia zao n kinyume na yao waliopita yaani wenye uso mrefu, maana wao ni watu wa kususia,hawafikilii sana vitu, pia kwa upande mwingine ni wakorofi na uwezo wao kiakili sio mkubwa sana lakin pia sio watu wa marafiki sana maana mara nyingi maamuzi yao hufanywa bila kufikilia kiundani.

PAJI YA USO MDUARA , Mhawa huonekana wavumbuzi, wasanii na wana endeshwa sana na mihemko (creative, artistic and highly emotiona).na kwa sababu hiyo ya kuendeshwa kwa mihemko hujikuta wanafanya mambo bila mpangilio

PAJI LA USO FLAT, ni watun ambao pia kufanya mambo yao kwa kufikilia kiundani na maamuzi yao huwachukuwa mda mrefu kuyafikia na huyaangalia mambo kutoka katika sura tofauti tofauti.

WATU WENYE NYUSI NGIUMU, (Strong eyebrows:). Hawa watu ni wa kujiaminisha na kabambe, wanatumia mpangilio zaidi katika maisha yao ila kwenye mapenzi wanaendeshwa na nguvu kubwa sana wana deal na hisia na mihemko yao kwa makini sana hivyo kwao ni wepesi wa kusimama mbele za watu.

NYUSI NYEMBAMBA , ( thin eyebrows) hawa watu wa aina hii ukikuta nyusi zake ni za asili basi wanaonekana kupigania sana uwezo wao wa kujiamini yaani huonekana wakujiamini sana lakin kiukweli matokeo ya mwonekano wao huwa ni kinyume na uharisia wao.

MIDOMO MIPANA , (full lips) hawa huwa ni wacheshi na huweza kutengeneza marafiki pia kwa haraka maana wanajuwa Ku care vizuri na katika mahusiano ni wepesi wa kujibu na kurudisha mwonekano wa mahusiano kuchanua ZAIDI pale wanapokuwa na wapenzi wao,nao sio watu wa kununa nuna.

MDOMO MWEMBAMBA , (thin lips) hawa wanapenda sana kujitenga na kuwa pekee kivyao kama ni nyumbani atakuwa Mara nyingi n MTU wa kujichemba chumbani au sehemu mbalimbali wanazokuwa akishindwa kukaa peke basi kukaa na mpenzi tu au MTU wa karibu sana, ni wasiri wa mambo yao Mara kwa Mara hawapendi wajulikane hata wakiwa sehemu furani.

WATU WENYE LIPSI KUBWA ZA CHINI, (large buttom lips) hawa wanaonekana kuwa watu wanaotafuta sana furaha au starehe zaidi (pleasure seekers) wao hupenda kuishi maisha ya furaha lakin pia ubaya ni kuwa huwa hawana uwezo wa kuji balance kitu ambacho hupelekea kujitosa jumla kwenye starehe au mapenzi.

HUU NI UCHAMBUZI NA UTAFITI ULIYOFANYWA NA WANASAIKOLOJIA AMBAO HAUJAHUSISHA MUONEKANO WA SURA AU USO ULIOFANYIWA MAREKEBISHO (MAN MADE OR MAKEUP) BALI UNAHUSISHA SURA AU USO AMBAO NI WA ASILI

NB: Mtu anaweza kuwa na mwonekano au sifa ZAIDI ya moja na kuonekana ana tabia isiyozidi moja, hill ni kawaida au akawa na tabia ZAIDI ya mbili na kuendelea Bali ya kuwa sifa anayo moja tu. kumbuka malezi na makuzi pia mazingira yanaweza Ku shape tabia ya MTU na kumtoa katika uhalisia
 
Mfano mtoto wa miaka 2 -4
-anpenda kucheza sana
-anajifunza kutembea
-kila anachokiona anataka akimiliki kuwa ni kitu chake
-anajifunza kuongea kwa kurudia maneno yanayotamkwa na mtu mwingine
- umri huu Watoto wanakuwa watundu na hawasikiii
-wanaharibu vifaaa mbalimbali vya nyumbani
-wanaonyesha upendo Kwa mtu Fulani ktk familia

Kwa kutumia saikolojia kwenye suala LA umri unaweza kubaini matendo ya mtt wako na kuweza kukabiliana nayo
Kuna siku huwa unaongea madini kama doctor fulani hivi au leo kule jukwaa pendwa hujakanyaga, hapo juu kuna swali langu ngoja nije pm unijibu swali langu.... Naona halijapata mbobezi
 
Hivi ni kweli kila mwanadamu anazaliwa na chembechembe za ugonjwa wazimu na ni kweli huwa zinalipuka na MTU huyo huwa kichaa kamili?
 
Hivi ni kweli kila mwanadamu anazaliwa na chembechembe za ugonjwa wazimu na ni kweli huwa zinalipuka na MTU huyo huwa kichaa kamili?
Ni kweli kuna watu wanazaliwa na hali kama hizi lakini sio binadamu wote mfano, Autism spectrum hawa huwa wana mental disability na Mara nyingi wanazaliwa nazo ,lakini pia kuna ukichaa ambao unatokana na matatizo yanayosabishwa na malezi kama mama mjamzito kutokuwa mwangalifu kulea mamba kwa kujihusiha na risk behavior au mtoto kupata maumivu ana majeraha wakati wa kujifungua haswa kichwani

Pia ni hali ya maisha na malezi hata ikiwa MTU amekuqa mkubwa mfano kujihusisha matuzmizi ya vilevi n.k hali hii pia huweza kutokea kwa MTU kutokana na kuzidiwwa na msongo wa mawazo ulio up to the maximum (Depression) hi hufanya ubongo kufika tamati ya kufikiria au kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa sababu ya matatizo ambayo MTU hushindwa kusolve au kuyakubali
 
Sawa kabisa mkuu huu umri uliotaja hapa ni umri sumbufu sana kwa walezi

Mfano katika hii age unakuta memory ya mtoto iko inaruhusu na INA hamu sana ya kujua kile anachokiona kwa maana kuwa mtoto anapenda kujifunza sana kwa matendo kuliko kuongea

Hii hufanya walezi wasioelewa kutumia adhabu sana kuwaajibisha watoto lakini huwa ni halo ya kawaida na kinachotakiwa ni kuwa na tahadhari ili alidhurike
Kabisa na ninataman Sana sku moja niwaze kupata wasaaa na wazaz mbalimbali kuwapa madini haya lakin watanzania wengi hatupendi seminar ambazo kwa watu wanayoielewa saikolojia vizur wanaweza kukusaidia kukabiliana na matatizo mbalimbali kwa upande wangu nilijikita sana na mambo yahusuyo umri wa binadamu kuanzia siku ya kutungwa mimba mpaka uzeee japo sjapata nafasi niweze kajifunza zaid napenda sana saikolojia
 
Kuna siku huwa unaongea madini kama doctor fulani hivi au leo kule jukwaa pendwa hujakanyaga, hapo juu kuna swali langu ngoja nije pm unijibu swali langu.... Naona halijapata mbobezi
Usjali hapa ndo penyewe nawapenda Sana watu wenye madini Kama mtoa mada itabidi nimtafute anifundishe zaidi niwe imara
 
Ni kweli kuna watu wanazaliwa na hali kama hizi lakini sio binadamu wote mfano, Autism spectrum hawa huwa wana mental disability na Mara nyingi wanazaliwa nazo ,lakini pia kuna ukichaa ambao unatokana na matatizo yanayosabishwa na malezi kama mama mjamzito kutokuwa mwangalifu kulea mamba kwa kujihusiha na risk behavior au mtoto kupata maumivu ana majeraha wakati wa kujifungua haswa kichwani

Pia ni hali ya maisha na malezi hata ikiwa MTU amekuqa mkubwa mfano kujihusisha matuzmizi ya vilevi n.k hali hii pia huweza kutokea kwa MTU kutokana na kuzidiwwa na msongo wa mawazo ulio up to the maximum (Depression) hi hufanya ubongo kufika tamati ya kufikiria au kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa sababu ya matatizo ambayo MTU hushindwa kusolve au kuyakubali
Kabisa mfano ninapoishi kuna baba alikuwa anafanya biashara za madini mererani akawa amejenga majumba na kununua gari akaamua kurudi kijijin kuwekeza baada ya mambo ya madini kuyumba mererani kadri siku zinavyoenda akaanza kufiliska baadae akaanza kuuza kitu kimoja kimoja mpaka akabaki na nyumba moja ambayo mke alificha hati saivi amekuwa kama kichaaa na kwake amehama analewa ovyooo hii ni kutokana na msongo wa mawazo hakuwa tayari kupokea hali hiyo hivyo ubongo umeshindwa kufanya Kazi ipasavyo kutokana na mkanganyiko wa mawazo
 
Exactly!
 
Kabisa na ninataman Sana sku moja niwaze kupata wasaaa na wazaz mbalimbali kuwapa madini haya lakin watanzania wengi hatupendi seminar ambazo kwa watu wanayoielewa saikolojia vizur wanaweza kukusaidia kukabiliana na matatizo mbalimbali kwa upande wangu nilijikita sana na mambo yahusuyo umri wa binadamu kuanzia siku ya kutungwa mimba mpaka uzeee japo sjapata nafasi niweze kajifunza zaid napenda sana saikolojia
Oohh! Hongera sana wasaa upo japo changamoto ni kuwa hata wanasaikolojia wenyewe hatujitoi zaidi, ila bado hii ni platform nzr kufikisha ujumbe na pale inapowezekana then tunatoka nje ya media na kuwafata physically.

Pamoja sana
 
Pamoja nitajitahid kadri ya uwezo wangu kuandaaa madini alafu niweze kuwapa wahusika maana mambo mengi tunakosea kutokana na kutoelewa vyanzo vya matatizo
 
Back
Top Bottom