April26
JF-Expert Member
- Jul 14, 2020
- 1,403
- 2,118
Habari ya weekend wakuu.
Kuna kozi mbalimbali za saikolojia (afya ya akili) zinazotolewa na vyuo vyetu hapa Tanzania kwa ngazi mbalimbali.
Kuna wahitimu wengi ambao wanafaa sana kuwa kwenye shule na vyuo vyetu kama wanasihi/washauri (school counselors) lakini wapo mtaani au wanatumika sehemu nyinginezo.
Mfano: waliosoma Bachelor of Education in Psychology, huu ni mfano mmoja tu lakini zipo kozi nyingine,,,,hawa ni special kwa kuwa wanasihi mashuleni kuhakikisha wadau wa elimu kuanzia wanafunzi, walimu, wazazi na viongozi wanakuwa fit psychologically kimaadili na kimaamuzi ili kulinda na kutoathiri lengo la elimu Tanzania.
Nafahamu kuwa kila mwalimu anagusa baadhi ya kozi za saikolojia ya watoto, lakini sio kama wale wataalamu waliosoma programme nzima. Kuna upungufu kiutendaji kwa baadhi ya walimu na means of counseling service aproaches inakuwa sio effective kiasi kinachotakiwa.
Kumekuwa na matukio mengi sana mashuleni ambayo kwa % kubwa chanzo chake ni matatizo ya kisaikolojia yanayopelekea tabia, maamuzi na matokeo mabaya.
Hawa wataalamu waajiriwe mashuleni kunusuru majanga kwa wanafunzi na walimu. Wizara husika inafahamu na vyuo wamewafunza hawa wataalamu kwa lengo hilohilo.
Sidhani kama chuo kinaweza kujipangia kozi za kufundisha bila kuwasiliana na gvt na bila kuangalia uhitaji.
Kama zamani palikuwa hapajaonekana uhitaji kwa sasa hata kama huna macho wala masikio ukipapasa utaona uhitaji ni mkubwa sana.
Bila shaka nimeeleweka lengo langu la kufikisha ujumbe kwa wadau ambao naamini wamo humu.
Ahsante!