Karibu ujiunge na Chama Cha Wanasaikolojia Tanzania (TAPA)

Dom2

Member
Jul 15, 2021
72
99
Tanzania Psychological Association(TAPA) ni shirika lisilo la faida (non-Profit Organization) ambalo lina dhamira ya kukuza na kusaidia mafunzo na huduma za kisaikolojia nchini Tanzania.

Chama kinafanya shughuli zifuatazo ili kufikia dhamira iliyo hapo juu;

1. Kuhakikisha kuwa chama kinabaki kuwa chombo cha jumuiya ya kiraia bila kujihusisha na chama chochote cha kisiasa.

2. Kuendeleza saikolojia kama sayansi, taaluma na kama njia ya kukuza ustawi wa binadamu.

3. Kujitahidi kikamilifu kwa haki ya kijamii, na kufanya utetezi kwa watu binafsi au vikundi ambavyo vinanyimwa ufikiaji wa manufaa ya nyenzo na kisaikolojia muhimu kwa maendeleo bora ya binadamu wote, na kupinga ukiukwaji wowote wa haki za msingi za binadamu.

Pia chama hiki kimesajaliwa na kutambuliwa na Serikali. Baadae kutakuwa na Bodi ya Chama cha Saikolojia, kuna sheria inakuja ambayo itatoa leseni ya kutoa huduma za Kisaokolojia.

Chama cha Wanasaikolojia Tanzania / Tanzanian Psychological Association(TAPA).

Aina za uanachama:
1. Student Member anayesoma Shahada au Uzamiri au Uzamivu fani ya Saikolojia
Gharama kwa mwaka ni Tsh 10,000/-
Ada ya kujiunga kwa mara moja ni Tsh 10,000/-
Jumla ni 20,000/=

2. Full member
Kwa Udom ni Bed - Guco na Psych. Degree holder wa Psychology.
Ada ya Kujiunga ni 10,000/- (mara moja)
Ada ya Mwaka ni 50,000/-
Jumla 60,000/-

3. Local Affiliate member
Mtu yeyote mwenye mapenzi na Fani hii Ya Psychology(Saikolojia)
Ada ya kujiunga ni Tsh. 10,000/-
Ada ya mwaka Tsh. 30,000/-
Jumla ni Tsh. 40,000/-

Faida za Kua Mwanachama
1. Nafasi ya Kujiendeleza kielimu kupitia Semina na mafunzo mbali mbali yanayotolewa na chama kwa Wanachama wake.

Mpaka sasa kila Mwisho wa Mwezi chama kinatoa Training kwa Zoom.

2. Nafasi ya bure ya kupata Mentor wa kukuongoza au kukupa Counselling ya bure (Kutika kwa Mbobezi wa Saikolojia mwenyezi elimu zaidi ya Masters, Ph.D ndani ya Chama).

3. Nafasi ya kupata mentorship ndani ya Chama na nje ya Nchi.Pamoja na Counselling ya bure unapokua na Changamoto.

Mpaka sasa tuna ushirikiano na American Psychological Association (APA) na Vyama vingine ambapo mpaka sasa wanachama wananufaika na trainings na Mentorship.

4. Kupata Connection na Wanachama wengine pamoja na Kazi aidha Serikalini au Taasisi binafsi.

5. Kwa full member,Unapata nafasi ya kuchagua au Kuchaguliwa kua kiongozi ndani ya chama.
Local Affiliate member yeye ana haki ya kuchagua tu ila hana haki ya kugombea nafasi ya Uongozi.

6. Unapata Kitambulisho cha Uanachama na Kutambulika.

7. Nafasi ya kutangaza Brand yako kipindi cha Mkutano Mkuu wa mwaka wa chama (AGM).

IMG-20220817-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom