Uwanja wa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwanja wa Taifa

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mwiba, May 16, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tanzania imekosa mapato ambayo ingeyapata kama timu zingeukodi uwanja huo kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Dunia yatakayofanyika Afrika kusini kesho.
  habari zilizotufikia kutoka vyanzo vyetu vya habari hii vinasema kuwa kuna timu imeurudisha uwanja huo na kuapa kuwa haitaukodi tena kwa maana Tz isahau kuwa uwanja huo kutatokea timu itaukodi ,maana yake watapakazia dunia nzima.

  Kilichotokeaa timu hio ilikuwa imeanza mazoezi na ni siku ya mwanzo nyakati za usiku baada ya mataa kuwashwa kulitokea wadudu kibao ,yaani senene au kumbikumbi kwa kwa lugha za walaji kiasi ya kusababisha wacheza wavae mask ili kuwazuia wasiingie midomoni na puani kwa jinsi walivyokuwa wengi.

  Hawajakaa vizuri mara umeme umezimwa mara umewashwa ,mara umezimwa tena ,akatafutwa anaehusika na majenereta ikajibiwa kuwa hayupo na haijulikani funguo anazo nani.
  Jamaa wakaongozwa kwa tochi hadi vyumba vya kulalia na asubuhi yake wakatafuta ndege na kuelekea kusiko julikana.
   
 2. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  usijekuwa na mdomo mbaya bwana, weka kisa cha kweli, vya kufikirika hivi watu wengine wanakuwa na midomo mibaya.
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ni simulizi la tahadhari bila shaka!
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kipindi cha kamatakamata ya kodi miaka ile, kuna wajamaa walijifanya wamebeba maiti (mwenzao aliyekuwa ana act) ili wakwepe kusimamishwa na kizingiti cha mgambo wa kukamata kodi, walipofika mbeleni baada ya kufanikiwa kuachwa, jamaa akakutwa kafa kweli, hapo sasaaaaaaa.
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  usituchurie mwanangu .kombe la dunia kucheza tena africa ni mpaka tena mwaka 3000
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mh! kautabiri kama kana ukweli flani hivi.
   
 7. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Du jaamaa yangu umekuwa Shekh Yahya. Naomba yasitokee usemayo!
   
 8. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  SOURCE?

  Ligi zenyewe za Ulaya ndio kwanza zimeisha jana rasmi, na bado fainali ya Champions League haijachezwa, hiyo timu iliyokuja kuweka kambi Tanzania ni ipi? Ambayo hata magazeti hayajaandika?

  Kweli wabongo tumezoea vitu vya hovyo hovyo!
   
 9. senator

  senator JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Jamaa amesema ni tetesi ila nimependa mfano wa mwana wa mungu....
  Kwa hali ya hewa ya sasa DSM jambo kama hilo kutokea ni wazi kabisa..Huenda Mwiba ni mmoja kati ya wale wanaona mbali..
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tatizo hamjui au hamna kalenda ,ndio maana yake. Hivi mnaelewa kuwa timu za Taifa zinazoshiriki kombe la dunia karibu zitamaliza na kufunga kambi za mazoezi ? Kwani mechi zikianza kunakuwa na instruction training tu za maelekezo na warmup nyepesi nyepesi ,chanzo changu cha habari kimestushwa na uelewa wenu kuwa hamjui kuwa kuna timu ilikuwa iwepo hapo kwa muda mrefu hadi kubaki kwa wiki tu kabla ya mechi kuanza.
  Kwa taarifa yenu timu ya Ghana ndio ilikuwa ndio iwepo hapo na walikuja ila hayo yaliotokea ndio yaliowakimbiza ,chanzo kilidai.
   
Loading...