Wakuu leo nilikuwa namsindikiza binamu yangu kwenda India kwa dhumuni la matibabu,lakini tumefika Uwanja wa Ndege wa JNIA tumepata taarifa za "kufungwa" kwa uwanja na safari kuhairishwa mpaka hapo tutakapotaarifiwa,na habari zinazoendelea ni kuwa abiria wanatakiwa kupelekwa hotelini ili kusubiri utaratibu mwingine.
Mpaka sasa haijajulikana haswaa swala ni nini?Wenye info za huko ndani mkuu Pdidy wa JNIA hebu tupe kinachoendelea hapo.
Picha:
Mpaka sasa haijajulikana haswaa swala ni nini?Wenye info za huko ndani mkuu Pdidy wa JNIA hebu tupe kinachoendelea hapo.
Ni kweli Uwanja ulifungwa kwa muda kadhaa,zaidi ya masaa mawili...Mimi pia nilikuwa natoka Mbeya kuja Dsm na Fastjet FN126...Tumezungushwa sana huko hewani mpaka matumbo yaakaanza kuunguruma,baadae tukatangaziwa kuwa uwanja umefungwa tunatakiwa tukatue Zanzibar....Tukapelekwa Znz toka saa moja mpaka saa tatu ndio tukaruhusiwa kuja Dsm.
Wacha watu tudhani mambo ya Uturuki yamekuja Dsm...Kila mtu anawaza lake na "Allah Akbar" na "Yesu Wangu" za kumwagaaaa....maana huko juu tumepiga mzunguko wa maana,mara Kisarawe mara Bagamoyo,unachungulia chini unaambiwa hii Mafia!!Yaani full kuzunguka huko juuu.
Baadae tumeshuka Dsm usiku wa saa tatu hivi,tukaambiwa kulikuwa na ndege ya Oman Air imetuwa vibaya na kupasuka tairi ya mbele,hivyo walikuwa wanabadili na ilikaa kwenye njia ya kutulia kwa masaa yote hayo ikalazimika uwanja kufungwa.Sasa kwamba mpaka sasa uwanja bado umefungwa hadi watu kwenda hotelini??Hiyo sina majibu...,
Cc: Pdidy Preta
Picha: