Uwanja wa Benjamin Mkapa | Simba Super Cup: Simba SC Vs TP Mazembe

Mazembe viungo wao washazeeka speed hamna, wanaitaji mtu Kama fei pale
 
Mohamed Hussein anapiga krosiiiiiiii kwake Mugalu anapiga kichwaaaa njeee
 
46+2'

kuelekea kuwa mapumziko uwanja wa Benjamin Mkapa si Simba wala Mazembe

Kona inapigwaaaa wanakosa TP Mazembe Inaokolewa

Anakwendaa Kalaba anapiga kichwaaaa eeeeh njee

Mchezaji wa TP yupo chini baada ya kupata rabsha

Naaaam mpira ni mapumziko uwanja wa Benjamin Mkapa si Simba wala Mazembe

HT: Simba SC 0-0 TP Mazembe

..... Ghazwat
 
Patashika ya michuano ya Simba Super Cup inafikia mwisho leo January 31, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ambapo Mnyama Mkali Simba SC inapepetana na Mabingwa wa Afrika mara tano TP Mazembe kutoka Congo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku kila timu kuhitaji ushindi na kunyakua taji hilo, Simba SC aliweza kushinda mchezo wa kwanza huku TP Mazembe akipoteza.

Je TP Mazembe atakubali kupoteza michezo yote miwili na Simba SC kushinda michezo yote miwili? Jibu ndani ya dakika 90 za mchezo huu.

Kumbuka mtanange huu ni kuanzia saa 11: 00 Usikose Ukasimuliwa.

.... Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

....Kikosi cha Simba SC

1.Beno Kakolanya
2.David Kameta
3.Mohamed Hussein
4.Pascal Wawa
5.Joash Onyango
6.Taddeo Lwanga
7.Miraji Othuman
8.Rally Bwalya
9.Chris Mugalu
10.Claotus Chama
11.Luis Miquissone

Subs:
Salim, Gadiel,Kennedy, Morrison, Mzamir, Ajibu, Kagere, Kahata, Lokosa, Peter, Chikwende

View attachment 1690873
Tuwekee na kikosi cha TP Mazembe acha kuwa na mahaba na timu moja tu... Thats bias
 
Karibia wachezaji wote wanaotoka Yanga na kwenda Simba, huishia tu kusugua benchi! Kuanzia Ajibu, Gadiel Michael, Morrison, Benno Kakolanya, nk!

Ila wakitoka Simba na kuja Yanga, huwa moto balaa! Kuanzia Kelvin Yondani, Amis Tambwe, Dida, Ajibu, na wengineo wengi. Hii inamaanisha Yanga ina uwezo mzuri wa kuwajenga na kuwatumia vizuri wachezaji kuliko Simba.
Inamaanisha yanga wachezaji wao viwango vyao ni vidogo kama wangekuwa wanawajenga wachezaji kina Mhilu, Lusajo na Charles Manyama walishindwaje kuwajenga
 
Back
Top Bottom