Uwanja wa Benjamin Mkapa | Simba Super Cup: Simba SC Vs TP Mazembe

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
Patashika ya michuano ya Simba Super Cup inafikia mwisho leo January 31, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ambapo Mnyama Mkali Simba SC inapepetana na Mabingwa wa Afrika mara tano TP Mazembe kutoka Congo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku kila timu kuhitaji ushindi na kunyakua taji hilo, Simba SC aliweza kushinda mchezo wa kwanza huku TP Mazembe akipoteza.

Je TP Mazembe atakubali kupoteza michezo yote miwili na Simba SC kushinda michezo yote miwili? Jibu ndani ya dakika 90 za mchezo huu.

Kumbuka mtanange huu ni kuanzia saa 11: 00 Usikose Ukasimuliwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Kikosi cha Simba SC

1. Beno Kakolanya
2. David Kameta
3. Mohamed Hussein
4. Pascal Wawa
5. Joash Onyango
6. Taddeo Lwanga
7. Miraji Othuman
8. Rally Bwalya
9. Chris Mugalu
10. Claotus Chama
11. Luis Miquissone

Subs:
Salim, Gadiel,Kennedy, Morrison, Mzamir, Ajibu, Kagere, Kahata, Lokosa, Peter, Chikwende

===========

Klabu ya Simba na TP Mazembe wa wamemaliza mchezo wao bila kufungana katika mchezo wa michuano ya Simba Super Cup uliofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa

Kwa matokeo hayo Simba SC imebeba taji la Simba Super Cup kwa kufikisha alama nne kufuatia ushindi katika mchezo wa kwanza wa mabao nne kwa moja dhidi ya Al Hilal.
Screenshot_20210131-090352.jpg
 
Naaaam vikosi vyote vipo uwanjani vipipasha misuli moto kijiweka tayari kwa mchezo huu wa SSC..!
 
Patashika ya michuano ya Simba Super Cup inafikia mwisho leo January 31, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ambapo Mnyama Mkali Simba SC inapepetana na Mabingwa wa Afrika mara tano TP Mazembe kutoka Congo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku kila timu kuhitaji ushindi na kunyakua taji hilo, Simba SC aliweza kushinda mchezo wa kwanza huku TP Mazembe akipoteza.

Je TP Mazembe atakubali kupoteza michezo yote miwili na Simba SC kushinda michezo yote miwili? Jibu ndani ya dakika 90 za mchezo huu.

Kumbuka mtanange huu ni kuanzia saa 11: 00 Usikose Ukasimuliwa.

.... Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Kikosi cha Simba SC

Beno Kakolanya
David Kameta
Mohamed Hussein
Pascal Wawa
Joash Onyango
Taddeo Lwanga
Miraji Othuman
Rally Bwalya
Chris Mugalu
Claotus Chama
Luis Miquissone

Subs:
Salim, Gadiel,Kennedy, Morrison, Mzamir, Ajibu, Kagere, Kahata, Lokosa, Peter, Chikwende

View attachment 1690873
Gadiel Michael hata kwenye mabonanza haaminiki.!?
 
Mkuu kimechelewa kidogo kutoka lakini kipo tayari hapo kwenye ubao, pamoja sana!
Mkuuu niseme Ukweli Nikisha Ona Line Up na hilo Gobore la Kikongo mnaliita Mugalu najua timu inacheza na wachezaji 10 Uwanjani. Mchezaji hana Agrressiveness, Hana Nidhamu ya kuendana na kasi ya Mchezo, Hana uwezo wa Kusoma mchezo hasa kusaidia kukaba timu inapozidiwa inshort Mugalu ni Boya Uwanjani Wanasimba Wenzangu tupaze Sauti Benchi la Ufundi nashukuru huwa wanatusikiliza huyu Mcongo HAPANA
 
Vikosi vyote vipo uwanjani kwa ukaguzi na kupiga picha za kumbukumbu muda wowote mpira utaanza

Simba SC Vs TP Mazembe
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom