Uvumbuzi huu umefanywa na wasomi wazawa

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,154
Madaktari pamoja na wafamasia wetu wamegundua namna ya kuiba dawa na kuzipeleka kwenye maduka yao binafsi bila kushikwa.

Wahandisi wetu wa ndani wamegundua namna nzuri ya kuiba pesa za miradi bila kushikwa.

Wakuu wa shule nao hawako nyuma wamegundua namna ya kuiba pesa za ruzuku bila kushikwa.

Wahasibu nao hawako nyuma wamegundua namna nzuri ya kuiba pesa za umma bila kushikwa licha ya ukaguzi wa mara kwa mara kutoka kwa ma auditors.

Wabunge pia sijawasahau wanaiba pesa za miradi ya Jimbo kwa kushirikiana na wakandarasi bila kushikwa.

Madiwani nanyi tunaijua janja janja zenu kwenye miradi ya kata.

Maafisa kata , kijiji na tarafa nao wamegundua namna nzuri ya kuiba pesa za umma bila kushikwa.

Maafisa manunuzi wa Tanzania nao wamefanya uvumbuzi amaizing.

Huwezi kuwashika ng'o.
 
There we go baby....🤣
 

Attachments

  • IMG-20240318-WA0009.jpg
    IMG-20240318-WA0009.jpg
    82.8 KB · Views: 2
  • IMG-20240318-WA0008.jpg
    IMG-20240318-WA0008.jpg
    77.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom