UVCCM Zanzibar: Abeid Karume afukuzwe CCM

UVCCM Zanzibar: Abeid Karume afukuzwe CCM

Karume yupo cuf siku nyingi wala siyo leo maana hata yule mtoto wake ameolewa na kiongozi mmoja wa cuf hata mambo yake mengi hufanya kwaajili ya cuf.
Hivi siasa zimeshatufikisha kutooleana...
 
Kama hali ipo hivyo miongoni mwa makada wa CCM,je kwenye vyombo vya usalama nako hakuna mgawanyiko wa kiitikadi kweli?Mgogoro wa kisiasa Zanzibar unaingia ktk hatua nyingine kabisa kuwahi kushuhudiwa.
 
Kwahiyo kama wewe ni ccm lazima utetee hata ujinga kisa we ccm.Mi siamini katika hili.Kufuta matokeo ni kosa.Jecha kashindwa kujitetea,leo eti kwakuwa mi ni ccm nimtetee!
 
Hivi huo muungano unaolindwa sana una faida gani kwa sisi watu wa Tanzania bara? Kuna nchi ambazo hata hatujaungana lakini zina faida kibiashara kuliko hata hiyo tukiyoungana nayo. Mapato tunayoingiza kupitia nchi ambazo hatujaungana nazo ni makubwa sana kuliko hayo ya Zanzibar. Serikali itaendelea kutumia nguvu hadi lini kule Zanzibar. Suluhisho la mgogoro ni kuwaachia Wazanzibar wenyewe waamue kama walivyoamua kwenye sanduku la kura. Wazanzibar waheshimiwe maamuzi yao kwenye kura kuliko kikundi cha watu wachache kuwaamulia Wazanzibar. La sivyo kila uchaguzi lazima mgogoro uibuke
 
Kwa nini kisifutiwe uanachama kwanza CHAMA CHA MAPINDUZI kuliko kuwaza anachokifanya Karume ?
CCM wameuwa sana nchi hii..
wametesa sana watu nchi hii,walemavu ni wengi..
wameleta matatizo mengi nchi hii..DODOMA wanakula viwavi vijeshi.
Maendeleo waliyoyaleta ukilinganisha na makusanyo ya kodi ya miaka 54 na tani za madini ambazo zimeshasombwa,haingii akilini kusema tumejenga barrabbarrra,
huu ni upuuzi,hata tatizo la maji limewashinda kulitatua.
 
Vijana wa CCM Zanzibar wametoa kauli ya pamoja kwamba Rais mstaafu Aman Karume afukuzwe CCM kwa kuwa anaungana na upinzani kukizamisha chama.

Vijana hao wanaoonekana kutumwa wamesema asipofukuzwa watatumia njia mbadala.

===================
SADIFA waheshimu wazanzibar acha ubinafsi wako maamuzi ya kura za Wazanzibar ni muhimu kuheshimiwa mbona maifanya Zanzibar kuwa Burundi nyingine.By the way Sadifa ameshatoka Honey moon?
 
"Kansigo, post: 15074720, member: 30697"]Chokochoko zote za karume, nia yake muungano uvunjike, wazanzbar ni wabaguz sana[/QUOTE]
Alikuwa na nafasi ya kuuvunja wakati alipokuwa rais kama ndo nia yake
 
Hivi huo muungano unaolindwa sana una faida gani kwa sisi watu wa Tanzania bara? Kuna nchi ambazo hata hatujaungana lakini zina faida kibiashara kuliko hata hiyo tukiyoungana nayo. Mapato tunayoingiza kupitia nchi ambazo hatujaungana nazo ni makubwa sana kuliko hayo ya Zanzibar. Serikali itaendelea kutumia nguvu hadi lini kule Zanzibar. Suluhisho la mgogoro ni kuwaachia Wazanzibar wenyewe waamue kama walivyoamua kwenye sanduku la kura. Wazanzibar waheshimiwe maamuzi yao kwenye kura kuliko kikundi cha watu wachache kuwaamulia Wazanzibar. La sivyo kila uchaguzi lazima mgogoro uibuke
Tanganyika ni Mkoloni wa Zanzibar kupitia koti la Muungano! Nyerere alipewa amri na Mabepari aitawale Zanzibar
 
Wazanzibari nao mazuzu tu kama Wabara, wanaibiwa lakini wapo wapo tu hata hawaeleweki
 
Shein amekata mirija ya maslahi ya Amani Karume, ndio maana muda mwingi Amani Karume anatumia kumuhujumu Shein. Kutokana na utawala na kashkash kipindi cha chaguzi za mwaka 2000 na 2005, hivi Amani Karume anapata wapi ujasiri wa kumkosoa Shein?
Na ashukuru sana kwakuwa Shein ni mpole, angekuwa Salmin ni Rais, Amani Karume angekuwa ananyea debe.
Amani Karume anampinga Shein kwakuwa maslahi yake binafsi yamezuiwa, na sio kwamba ana mapenzi mema na Zanzibar au wazanzibar.
ndiyo maana kikwete kang'ang'ania madaraka kisa magufuli alimwambia anasafiri nje ya nchi kuliko kwenda kumsalimia mama yake, ccm ukimkosoa mtu kwa ujinga anaofanya aachii madaraka.
 
Karume yupo cuf siku nyingi wala siyo leo maana hata yule mtoto wake ameolewa na kiongozi mmoja wa cuf hata mambo yake mengi hufanya kwaajili ya cuf.
Duh! kama bintiye kaolewa na kiongozi wa cuf japo hujasema ni nani, basi mpaka hapo uaminifu wake haupo kabisa. Nijuavyo mimi watu wa cuf na ccm walikuwa hawaoleani kabisa kwa siasa zao zilivyo tangu miaka mingi nyuma.
 
Karume anaendeleza historia ya Marais wastaafu waliotawala zanzibar, wote wamekuwa wanabadirika baada ya kustaafu na kuanza kudai wanaouita Uhuru wa Zanzibar toka kwa watanganyika. Kwa wafuatiliaji wa Siasa, hatutashangaa na Shein naye akigeuka baada ya muda wake kutawala kutaradad.
 
Nyie UVCCM Zanzibar kwani CCM baba zenu ndio waliianzisha mpaka mumfukuze Rais mstaafu Aman Karume? Acheni upumbavu wenu kosa lake mini?
 
Shein hana tofauti na laurent gnagbo alieshindwa uuchaguzi alafu anang'ang'ania kubaki ikulu
 
Karume yupo cuf siku nyingi wala siyo leo maana hata yule mtoto wake ameolewa na kiongozi mmoja wa cuf hata mambo yake mengi hufanya kwaajili ya cuf.
kwa hiyo mkuu Simiyu, wewe binti yako akiolewa na mtu mwenye itikadi tofauti na wewe, ni kosa? ..kwa nini unakuwa na chuki kiasi hiki?

Mi nadhani Karume anajitambua na ndio sababu yeye hujali maslah ya Zanzibar kuliko chama...
 
Kama hali ipo hivyo miongoni mwa makada wa CCM,je kwenye vyombo vya usalama nako hakuna mgawanyiko wa kiitikadi kweli?Mgogoro wa kisiasa Zanzibar unaingia ktk hatua nyingine kabisa kuwahi kushuhudiwa.
tena kwa wakati huu cuf wapo ngangari,wamoja,na wapo technical fit. Mpaka sawa ngoma droo.
 
Back
Top Bottom