Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,295
4,558
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imeitaka serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuhakikisha inaufungia mtandao wa 'X' zamani ukijulikana kama 'tweeter' kwa kuwa mtandao huo kutangaza dhamira ya kuruhusu kupokea maudhui yanayokinzana mila, desturi na silka ya Watanzania

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohamed Ali Mohamed (Kawaida) wakati akizungumza na wanahabari leo, Jumanne Juni 11.2024 jijini Dar es Salaam ambapo amesema hatua ya kuufuta mtandao huo itasaidia kuendelea kulinda maadili ya vijana wa Tanzania kwa kuwa mitandao ya kijamii haipaswi kupewa kipaumbele kama inachochea uvunjifu wa mila na desturi

Kawaida amesema hivi karibuni mtandao huo (X) umetoa tangazo ukieleza kwamba maudhui yote ya kingono na Yale yanayofanana na hayo yameruhusiwa kupokelewa jambo ambalo halikubaliki kwenye taswira ya jamii ya Tanzania

Amesema taarifa hiyo ya kusikitisha imepokelewa kwa hisia hasi na UVCCM hivyo kuitaka serikali kuchukua maamuzi kama iliyowahi kuchukua siku za nyuma ambapo serikali ilifungia mitandao iliyokuwa ikipandisha maudhui kama hayo

Pia soma:
 
FB_IMG_1574277425198.jpg
 
Mbona almost social media zote zinaruhusu hizo content? Lakini pia zina option if hutaki unaweza disable kuona hizo content
 
Bado news ni kwamba facebook, telegram, whatsapp, almost social media zote ziliruhusu kabla ya twitter. Best solution fungia yote
Hao UVCCM mkubwa wao si anatuhumiwa na dada mange kwa ukosefu wa maadili? sasa kwa umri ule mambo hayo alifundishwa na mtandao wa X? Haya mambo ya ushoga kuyapigia mayowe ndivyo tunavyozidi kuyatangaza na kuyapa nguvu.
 
Back
Top Bottom