Nilishawai kuandika kuhusu hwa jamaa TISS, ni kwamba CCM ni kama bango tuu ila wanaoiaribu hii nchi ni hawa jamaa
Mfano:- CCM inatambua bila hawa jamaa awawezi kuingia madarakani na ndio maana kila mkoa kwenye uchaguzi wanakuwepo.
Pili-Hata kumchagua Rais ndio hao wanahusika na ndio maana utakuta marais wote nchini wanaongozwa na wao hawawezi kumweka mtu kama slaa au magufuli cause utakua mwisho wao wa kutukuzwa. Tatu ukikumbuka hawa jamaa ni inteligencier ya mwalimu na wengi wao waliku darasa la saba au hawakusoma kabisa so walipopata mwanya wakajisomesha ili kuja kushika mashirika yote hapa nchini na baadhi ya private sector kujipenyeza kwa ajili ya usalama wa taifa so, utakuta all CEO katika mashirika yote ya uma ni wao na baadhi ya private sector mwanajf utajidanganya kuuomba uCEO kwenye sector za umma na ukapata bila kuwa mwanausalama.
Nne utakumbuka wakati alipokua nyerere mashirika yalikua yanaongozwa na Raia wenye elimu na ujuzi na ndio maana yalikua active so, baada ya nyerere zikafanyika propaganda mpaka wakaweza kuyamiliki mashirika yote ya uma na ndipo kufa kwa mashirika mengi yakaanza hapo.
Tano- Jiulize mikataba yote mibovu lazma wao waipitie hata kuwaleta mainvestors matapeli wao ushiriki mfano EPA na kampuni zake zote zilizoshiriki utakuta ni wao
Sita- Rais awezi kuja kuhutubia taifa bila wao kuhusoma hotuba na kuihakiki, Rais uandaliwa bajet kubwa na safari ukiwa na msururu wa wanausalama ilimradi wapate posho.
SAba- ulishawai kusikia wapi mjadala wa bajeti ya hawa watu? hata kujadiliwa bungeni? wizara zote zinaendakuomba fungu pale lakini hawa warecommend tuu tunataka kiasi fulani na akina mahesabu.
so wanajf mtasumbuka sana kuilaani CCM lakini ccm kwa ujinga wao wanatumiwa kama chambo tuu ila wahusika wanaoisumbua hii nchi ni wao.
Na ukiwa mfuatiliaji sana wanakumaliza hata slaa ataongea sana ila anakikomochake cause baadhi yao walishakula kiapo cha kutunza siri sifahamu kama slaa ameshakula kiapo ila ukishafikia grade kama ya slaa lazma usign hicho kiapo.
Nchi inaendeshwa na TISS na sio chama hata mweke chama gani TISS ndio inayoongoza nchi kupitia mgongo wa chama
Wana jf huu ndio mchango wangu kaa chini na tafakari.
Duh Mzee nimejiservia kama ulivyosema nashukuru sana Mkuu, Kumbe hujasinzia Mkuu hiyo ni avatar!
ukiangalia matokea ya uchaguzi wa mwaka 2010 haiingii akilini kwamba TISS waliingiza makonteina ya kuchakachua kura. Binafsi naona Rais asingepata asilimia 61 kama tulivyoshuhudia. Hizi ni propaganda za kisiasa za kulikuza jambo hili ingawa mtazamo wangu haondoi ukweli kwamba hakuna uchaguzi unaoweza kukosa malalamiko.Wakati TISS walipoingiza kontena la kura kule Tunduma mbaona UVCCM hawakuona wanavuruga nchi?
Mbona Mkapa hawakuwahi kusema usalama wa Taifa haumsaidii? huyu Mkwere ni janga la Taifa, anachotaka kusikia yeye ni mambo matam matam, mfano umwambie kwamba foleni kubwa kwenye barabara za jijini Dar ni dalili za maisha bora hapo ndio atafurahi, hataki umwambie kwamba tatizo barabara ni chache na zile za mitaani hazipitiki ni mbovu na miundombinu ni mibovu, ukimueleza hayo wewe unavunja amani na utulivu.
Heshima kwako Dot Connector,
Mkuu kwa hili niko pamoja na UVCCM.Ukiisikiliza hotuba ya Kikwete mwisho wa mwezi uliopita utagundua kweli TISS wanampatia taarifa za kumwangamiza kabisa badla ya kumsaidia kumjenga.Ipo tafauti kubwa baina ya Kikwete kipindi kile akiishambulia picha ya mapanki [Sangara] au wakati akifungua bunge mwaka 2005 na hotuba alizozitoa baadaye anaonekana akilalamika kama mwananchi wa kawaida asiye na mamlaka yoyote.Kitendo cha kulaani maandamano ya CHADEMA kkiliitimisha hisia zangu Kikwete nchi imeshamshinda siku nyingi.
Kwani yeye kabila gani kama si mkwere, mimi ni msukuma najiona fahari ukiniita hivyo.
Lakini hawa vijana wanataka TISS ndiyo wawe wanasema kwenye media? Je wanataka TISS iwaambie inamsaidia vipi rais?
Je kuna chochote kinachofichika ambayo JK hayup?
Je gharama za maisha hazijapanda sana?
Je vipato vy Mtanazania havijashuka?
Je ufisadi haujakithiri?
Miundo mbinu, je? Inafanyiwa kazi?
Nchi haipo gizani?
Wale wanaotusaidia budget wameona kuna tatizo na ndiyo maana hawajatoa fedha.
Hata budget ya mwaka 2011/12 inabidi iwe ndogo na yenye kutegemea mapato ya ndani kwa zaidi ya 80% ili angalau tuonyeshe ukweli katika kupanga kwetu na mapato yetu.
Vijana inabidi wajue majukumu yao na siyo kumharibia JK, wao wanadhani wanawaharibia EL na Sumaye, lakini wanamharibia rais zaidi ya CCM yao wanaichimbia kaburi zaidi.
Hawa watoto inabidi saa nyingine wakemewe, waache longolongo na kucheza na media, maana media itawamaliza mara moja!!!!!
Ukisia ushamba ndio huu, JK original alikuwa anaitwa mchonga, kuna sehemu inaitwa kibaha kwa mfipa, mifano ya namna hiyo iko mingi nadhani wenzangu wataongezea orodha hapa, ninachokiona hapa kwako ni zile posho za lunch mlizopewa pale Dodoma za sh 50,000 kila mjumbe ndio bado zinakulevya. otherwise una point tambaa.
Nick name yanayokubalika na jamii mara nyingi hubandikwa watu kulinga na hali, jinsi au mambo wanayoyafanya na kwa kweli huya yanakaa vizuri kuliko hata majina yao. Kwa hiyo Mkwere siyo jina baya na kwa kweli linamkaa vema. Kuhusu kulalama kwa UVCCM, Matatizo ya CCM yapo kila idara sasa hivi. Kuanzaia shina hadi taifa na watawalalamikia wengi muno kwa sababu si watu wa kutatua matatizo. Walianza na CDM, Makanisa, sasa TISS. Sasa TISS si ndo wanoongoza nyingi au wamewatenga na kumwajiri sheikh Yahya. Kama ndo hivyo, basi wameshapotea njia. Kila la kheri CMM kwani uswahiba, ufisadi, rushwa na Uvivu ndo vinakuuwa.
Tatizo hapa JF mkwere linatumika kama jina la kumdhihaki Rais. Tuheshimu makabila ya watu.