Dr Willibrod Slaa
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 675
- 1,523
Mbu Sugu,
TISS ndio walioandika barua kwa Waziri Mkuu Lowasa 2007, wakisisitiza "Hoja ya Dr Slaa isiruhusiwe kuingia ukumbini kwa kuwa Serikali haitakuwa na majibu". Kama utakumbuka hoja hiyo ilihusu Uwizi Mkubwa Benki Kuu(BOT na Hazina. Pia katika Taarifa ya Ernst and Young
kampuni inayomilikiwa na vigogo wa TISS ilikuwa moja ya makampuni yaliyojinufaisha na EPA, na JK hadi leo amepata kigugumizi kufikisha Kampuni hiyo mahakamani(Rejea Taarifa ya Ernst and Young).
Kama ushauri wa TISS kwa Waziri Mkuu (Naamini wasingeliweza kumshauri Waziri Mkuu bila kibali au angalau kumjulisha Rais, sasa ulitegemea nini. Watu wanaoitwa Usalama wa Taifa wanageuka kuwa "wahujumu" wa Rasilimali za Taifa! Ni kweli tumshukuru mtu kwa mema aliyofanya, na labda siyo wote pia wameoza, lakini nyumba isiposafishwa kwa uchafu mdogo kwenye kona hatimaye nyumba nzima itanuka na ndiko tulikofika leo.
Hoja yako ni ya kinadharia wakati ushahidi wa maandishi dhidi yao unaonyesha tofauti. Usalama wa Taifa ungelikuwepo, Kampuni iliyowasha umeme (Mwanza) kwa siku mbili 2007 isingeliendelea kulipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi wa Tanzania hadi leo, takriban miaka mitatu baadaye. Nadhani malalamiko ya wanajamvi yanaeleweka. Si vema kutetea nadharia isiyo na mshiko mbele ya "documentary evidence".

Ni upungufu wa weredi kama tutaendelea kufikiri kwamba kila jambo zuri au baya nchini limefanywa na majasusi na si vyombo vingine pia. Kwa maana kwamba kama TISS watalaumiwa kwa kila jambo baya linalotokea nchini basi pia wapewe sifa kwa mambo yote mazuri yanayotokea nchini. Ni muhimu tukajifunza mipaka ya uwajibikaji katika mifumo wa kisiasa na kiutendaji ili kutenda haki kwa kila chombo ndani ya mfumo wa serikali.