UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina


Like father like son
Nakumbuka Lowassa wakati anaachia uwaziri mkuu alijaribu kusema kwamba mjengoni ni wengi ila wanamtosa akijaribu kupata huruma ya wabunge na wananchi kwamba wengi ni wachafu yeye asitolewe kama mbuzi wa kafara.

Hapa Bashe naye kaja na gia ya kuonyesha uchafu wa Lowassa na kulinganisha na wa Malecela kila mmoja tutamsema kwa wakati wake ila hilo ulisemalo la wewe kumsupport Lowassa wala halina tatizo katiba inakuruhusu lakini sisi wananchi tunaamini ampendae na kumsupport jambazi ni JAMBAZI.
 
Congratulation Bashe, my worry is ushauri wako utazingatiwa? Kiongozi mkuu hataki ushauri asioupenda na hilo kamrithisha Nape, nadhani umemsikia anachoendelea kufanya Rukwa. Ni heri kumfundisha mnyama kucheza mziki kuliko kumbadili mawazo mpumbavu!!!!!
 

- Salute!

William @ NYC, USA.
 

- Ushauri tu wa bure!

William @ NYC, USA.
 


Mkuu Bashe kuna maswali unatakiwa kutoa majibu muafaka mbona umekimbia ?.
 
Mkuu Bashe kuna maswali unatakiwa kutoa majibu muafaka mbona umekimbia ?.

Subirini kaenda uliza majibu Monduliiiiiii na hata akirudi msitegemee cha ajabu maana hajui hata kuibia majibu mazuri...ukitaka umfaidi Bashe ongea naye ukiwa unasoma majibu toka kwenye sura yake...ila ni jasiri kweli kwani huwa hana mshipa wa aibu kwa kusema uongo
 
B
Alisema leo CCM inaimba Nyimbo za Chadema na akasema Tumeingia katika POLITICAL TRAP ya chadema tunafanyia kazi ya kwao na kuacha ya kwetu 2015 tutaulizwa yakwetu tutakua hatuna majibu, alisema CCM tumekua REACTIVE badala ya PROACTIVE,badala ya kuwa Viongozi sasa Tunaongozwa,

Kumbe wanajua kuwa Chama tawala kinaongozwa???????
 

Mkuu Ngisibara

Bashe alidhani JF ni sawa na UVCCM una bwabwaja unapigiwa makofi.


Vijana wa leo bure kabisa nakwambia miaka ya 60s tungekuwa nao hadi leo mkoloni angekuwa ameweka kambi.
 
- Duh! noumaaaaa!

Willie @ NYC, USA.

Nyambala, leta ushahidi kuthibitisha kwamba 'LAMPARD' ni 'hkigwangalla'

FYI, I have never hidden my identity kwenye hizi public forums hata mara moja, hivyo mimi huongea my mind na nikitaka nihukumiwe kwa kauli yangu...I am not like you bro!
 


Sijawahi kufikiri kwamba ndani ya chama cha Magamba kuna viumbe vimesalia na Busara zao, Ahsante kwa kumwelimisha huyo chali.:majani7:
 


Haya sasa ni mengine!!! kama sisi binadamu tungepewa nafasi ya kutoa hukumu siku ya mwisho(kiama) pasingetosha ili mradi tu kumalizana.
Kweli kundi lake ni baya lakini kuna uwezekano yeye asiwe hivyo!! nahisi anatumika tu. Anatia huruma masikini lkn hajui afanyeje. Kweli rafiki ya mwizi siku zote naye mwizi hataka kama hajawahi kuiba.
 
Basha amenena kweli kumbe matatizo wanayajua sasa wanakusanya maoni ya nini!!
 
Mjadala Ulikuwa Mzuri sana

Asante Hussein Bashe
 
mr Bashe umechelewa sanaaa!
Kwa sasa mshaurini muheshimiwa aachie ngazi tu!
ili CCM Ijivue gamba kiukweli!
Hapo tena baada ya kutubu ndipo muombe ridhaa kwa wananchi!
Maneno yako si matamu zaidi ya kuondoa umaskini ujinga na maradhi si matamu zaidi ya maisha bora kwa KILA mtanzania!
Leo watanzania wameona hayana mashiko bali ni usanii kama unaouleta sasa!
dawa kaeni pembei lmuangalie mlipo jikwaa, kisha mrudi muwaombe radhi wananchi wakiwasamehe mtapewa ridhaa tena!
kama ni gari is beyond economic repair!
Muda utasema.
 
Mheshimiwa sana William,
Mimi siko upande wa Bashe kabisa kwa kuwa yeye ni mshiriki wa chama magamba kama wewe, chama kilichotufikisha kwenye malumbano haya. Chama kilichokuwa kikisema kuwa hakuna mafisadi katika chama na baadaye kukili wako. Chama kisichosimamia kauli zake na hivyo kupoteza imani kwetu.
Ninanachohitaji kusema hapa ni kauli yako ya kumtetea baba yako. Ukweli ni kwamba pamoja na kwamba yeye ameanza utumishi wa serikali akiwa na miaka 22 haimuondoi kwenye hatia za ufisadi. Ukweli kabisa ni kwamba baba yako akiwa waziri mkuu kuna maeneo alishiriki au alishirikiana na mafisadi wa wakati wake. Hakuwa msafi kama unavyotaka kutuaminisha. Bahati nzuri mzee wako kawa waziri mkuu wakati nikiwa mtu mzima na ninamfahamu vema. Yawezekana hujui, Amini hakuwa msafi na Mungu anajua hakuwa msafi! Nitasema ukweli daima fitina kwangu mwiko.
Tuendelee na hoja iliyo ukutani!
 
Dogo ondoa hapa hadithi za kizamani. FYI mimi ni over 50 kwa hiyo angalau naweza kusimulia yote ninayokumbuka tangu nikiwa TYL miaka ya 1967. Historia ya nchi hii haijawahi kujengwa na watu wawili wa Pemba na Ilala tu unaosema. There many elders walioko huku vijijini wanaofahamu historia ya nchi hii bana. Nina mashaka na elimu yako kama unadhani historia ya nchi hii inajulikana kwa watu wawili tu........ ndio sababu umepoteza mwelekeo.
Ukweli tunaujua woteeee. Sasa kaa chini ufundishwe usijifanye kuwa msomi usiye na kitu bana. Sisi pia tumesoma na tunaendelea kusoma na uzee wetu unasikia?
 

- Mkuu huu ni mjadala wa Bashe, wewe baba yako sio msafi na wewe unajua sana kwamba ninajua sana, sasa naomba ufungue mjadala wa baba zetu tuwaongelee wazazi wetu, yaani wangu na wako!, huu ni wa Bashe! Baba yako alipokuwa pale Ubalozini alifanya mengi sana ya ajabu,

- So! utakua mjadala mzuri sana wewe ni kufungua tu thread utakapokua tayari na nifahamishe!

Much Respect!
na Karibu Sana mkuu Wangu!

William @ NYC, USA.
 
Nyambala, leta ushahidi kuthibitisha kwamba 'LAMPARD' ni 'hkigwangalla'

FYI, I have never hidden my identity kwenye hizi public forums hata mara moja, hivyo mimi huongea my mind na nikitaka nihukumiwe kwa kauli yangu...I am not like you bro!

Bwana mdogo unahitaji kuwa makini!!!!!!! huu ndiyo ushauri wangu wa bureeeee kabisa! You can run but you can never hide!
 
Sawa bana. Msg sent anyaway...........
 
Bashe,

Ondoka CCM kama hupendi vyama vya upinzani ni heri usiwe na chama kama mimi. Utakuwa more objective na utakosoa vizuri sana. Ukisema sasa hivi kila mtu anakufikiria labda tu unawatetea ma-triplets. Kuondoa hayo toka huko tukosoe tukiwa huru. Usije uko-Kolimbwa bure tukapoteza mpiganaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…