UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina



- Well, siwezi kuwa kwenye usingizi wa aina yoyote, I mean how can kiongozi wa taifa wa stature yako akaja hapa JF kumlilia mwananchi kama mimi aliyelala usingizi, huoni kwamba wananchi walio macho watashindwa kubaini kati yangu na wewe nani yuko usingizini? ha! ha! ha! ha!

- Ni kweli kabisa kama mwanachi nina haki ya kukuuliza wewe kiongozi uliyefukuzwa mara mbili, Moral Authority ya kutoa hotuba za kuelimisha wanachama wa chama kilichokufukuza uongozini mwake umeitoa wapi? Waannchi wengi wamekuuliza maswali humu mbona huwajibu, ila umenikomalia mimi mwananchi niliyelala usingizi? ha! ha! ha! ha! ha! ha! Unajua una hoja zinachekesha sana! ambazo ninaweza kuzijibu bila hata kufikiri sana!

- Tuufunge mjadala maana sasa unakugusa pabaya sana, hapana hapa tunaelimishana na kuelimisha taifa, waannchi wanajionea ni kwa nini hili taifa limedumaa ni kwa sababu ya kuwahi kuongozwa na watu kama wewe, unayeamini kwamba wananchi wana shida ya umeme, lakini wewe utampigia kura Lowassa aliyewaletea hilo hilo tatizo la umeme, Bashe watu kama nyinyi ondokeni huko kwenye siasa za taifa maana wewe na hao MAPACHA WATATU tayari Mmeshindwa, waachieni wengine sasa, I mean mimi hata nikiwa anything sio kiongozi na wala sikutoa hotuba anywhere na kuwadanganya wananchi kwa maneno ambayo mimi mwenyewe nikiwa kiongozi nimsehindwa kuyatimiza,

- Bashe mimi ni mwananchi ni haki yangu kukuuliza maswali ya msingi reardless of who is my father au mother, tizama kwenye hoja zangu ni wapi nimeuulizia kuhusu baba yako au mama yako, wewe hoja ya kwanza Mama Kilango, Malecela! badala ya kusimamia hoja zako mwenyewe ulizozitoa kwenye UV-CCM na kuwalipa media wa kupambe, sasa ukaona na huku JF nako unaweza kupambwa hapa hatupambi mtu, umetoa hotuba umeileta hapa sasa simama hapa ujibu maswali waliyoshindwa kukuuliza kule UV-CCM kwa sababu ya kuwaogopa wanaokutuma MAPACHA WATATU,

- Bashe siasa za kisasa ni hoja, sio manguvu na hasira, mimi sio kiongozi mwenzio wewe ndio mwenye burden of the proof ya kuonyesha kwamba una uwezo wa uongozi, nilitegemea utaonyesha uwezo wako wa kuongoza mpaka wananchi tuamini kwamba ulionewa kwenye kufukuzwa, lakini kwa haya yote uliyoyasema hapa kwenye hii thread, naomba nikwambie kwamba huna uwezo wa kuongoza wala kutafuta maoni ya aina yoyote kwa taifa, na ndio maana hili taifa tumekwama sana, I mean kiongozi wa stature yako anashindwa kujibu hoja za hotuba yake mwenyewe, badala yake unanijibu mwananchi kama mimi ninayekuuliza ishus za baba, mama na location yangu? Damn maan!

Ahsante Sana Mheshimiwa na Mungu Aibariki JF, maana huko kote umesfiwa sana sasa hapa tunakuomba ubebe msalaba wako unalilia baba na mama zetu wananchi na location zetu, kweli hili taifa sijui tulilogwa na nani, I mean can you imagine Trump anamuuliza Obama cheti cha kuzaliwa, halafu Obama anaaanza kumjibu kwamba wewe umezaliwa kwenye utajiri hujui lolote kuhusu umasikini? ha! ha! ha! ha! ha! ha!, Only in Tanzania!

William @ NYC, USA.




 

- Duh! noumaaaaa!

Willie @ NYC, USA.
 


  • Ukisoma taarifa ya richmond hakuna mahali ambapo unaona Lowasa kasemwabali preamble ambayo nayo imejaaa maneno.
Kwa kizungu wanasema hukusoma ripoti btn the lines. Hata mtu wa kidato cha Nne angejua tu. Otherwise ulisoma ripoti ukiwa biased. Mwananchi yeyote neutraal na hawakutaka kumvua nguo la sivyo hata Pension yake ya UPM angeilia segerea

  • Mzee Lowasa umeifanyia kazi kubwa sana nchi yetu
Kazi kubwa zipi hizo ebu taja mbili tu ???? Alafu Kwani yeye ni expatraite wa nje. Ni wajibu kukiogozi yeyote. Hatu exepect kazi ndogo kwaiongozi yeyote ni CCM tu ndo inalet down taifa. Lowasa hajafanya kazi. yeye na Jk ni watu wa kucheza na media tu. Tena Lowasa anazidiwa na Pinda the only diffrence pinda hana tamaa ya madaraka ndio maana yeye hangaiki sana na media kupamba habari zake. na cha muhimu ni muaminifu na mzalendo kwa taifa

  • Kuna marafiki zangu maDC wanasema kuwa tangu Lowasa ametoka na wao wanajisikia wako likizo.
Hao marafii zako hawakuepewa U DC kwa uwezo wao bali waliepwa kwa urafiki . Ni aibu sana wewe kuandika haya. DC anataka asukumwe kama gari bovu???!!!!!. Yaani wao motivation ya wao kuwa DC mpaka Lowasa awe PM. Kumbe sifa za uchapakazi wa Lowasa ni sababu ya kukimbizana na ma dc wabovu. teh teh teh. Waulize hao marafiki zako Vip Lowasa angekuwa Rais alafu PM akawa JK . Je wangejisikia wako maternity leave

  • Naweza kusema kuwa hakuna mwanasiasa ndani ya ccm au waziri yeyote anaeweza kusema kuwa ana uwezo wa kiutendaji kama wa Lowassa
Hahahahhaa Aiseeeee utendaji gani sasa kama ofisi yake imeweza kuingia mkataba kampuni hewa. Katika karne hii ya Dotcom jiulize kwa nn huyu mtedaji na watu wake walishindwa hili? Nakuambia tena Lowasa hamzidi hata Pinda sana sana ni kutumia magazeti. Labda kama unamliganisha Lowasa na mwenzake JK. maana wote ni wasanii

  • Siasa haina uwezo wa kutoa kiongozi bora na ndio maana mimi sitaki kugombea siasa za tanzania
Aiseee kumbe yote uliyokuwa unaongea kuhusu Lowasa ilikuwa nini :A S-confused1:


Mkuuu kifupi ondoa propaganda za kusema hakuna kama Lowasa.
 

- Mkulu Ngongo Salute!

William @ NYC, USA.
 

Endelea kuota na EDWARD wako, huyo kishapigwa chini tafuteni mwingine mumpigie kampeni, huyo hauziki kwa watanazania wa leo....Hata leo mshauri atoke CCM uone nini kitatokea kama siyo kujibu kesi moja baada ya nyingine, nyambaf kabisa!!!....eti Lowassa this, Lowassa that, hebu mshaurini atoke LEO CCM tumuone huo ubavu wake akiwa nje.... Jitu halina huruma na watanzania halafu leo anatokea mtu kumtetea hapa eti kwa vile kaahidiwa kacheo au kabahasha ka khaki, inakera sana!
 

Hahahahahhah!! This is a winner, asante sana mshikachuma!!

Eti tukitaka kujua history tumtafute bibi wa Ilala na Babu wa Pemba!! Ina maana wamekula memory stick ya historia ya TZ ???

Kama historia yetu haijawa documented kwenye vitabu na maonyesho basi we r goners!! Hatuwezi kurely on porojo za bibi wa Ilala na babu wa Pemba who are not even historic figures like kina Sykes, bibi titi etc...


Mtu akishachafuka na kuanza kuchafua wenzake, sio tu kuwa anasafishika bali anaendelea kutokota topeni na anaowasafisha...

So Bashe get it from me, u r not clean, Lowassa is not clean and there is nothing u can say or do to convince(sp) me otherwise!!

Mshikachuma nimefurahia uchambuzi wako kwakweli, magamba should get out!
 
Kama anayo mivutano Nzega basi ni kawaida ya mizengwe ya CCM huko sina kauli nako. Huyu bwana ametumia sawasawa kutoa elimu ya uraia sio kwa vijana tu, bali pia kwa manape wake na maridhi1 et al. Huo uasili wa Somalia ndio ukabila anaousemea Bashe tusiende huko tukakosa uelekea.

JF ni platform imara ya wanaofikiria kwa kina, kama ni kusemana kwamba sio watanzania basi watu wote walioko mipakani mwa Tanzania sio wananchi wa Tanzania, hata JKN alishasemwa sana utusi wake. Mbona Kinana mmemuachia tum, kwani usomali wake una rangi ya kuwavutia?

Mtu akifanya kazi vizuri kwa manufaa ya wengi mtieni moyo asonge mbele. Maendeleo yakija hayataishia kwenye viunga vya ukoo wake tu. Kwani Chenge ni Msomali anapotuibia vile?

Lowasa je, ni Mkenya? Rostam naye ni Mtanzania ila tabia yake ndio imekosa Utanzania. Kama CCM wangekuwa wanajianika na kufanya hivyo basi hata vyama vya upinzani visingekuwa na nafasi.

Lakini kwa kuwa wanadhani wao ndio vijogoo peke yao, watakula jeuri yao.
 
Waliotoa ujumbe wa kweli kama msomali huyu ndani ya sisiemu ni weng,lakini utekelezaj hakuna!so tusitarajie jpya
 
Hana lolote huyu anapiginia tumbo lake, unategemea Bashe acritise RA, atakula wapi, ni front tu ya kusifisha njia ya boss wake ili waendelee kupeta.
 
SHALOOM JF,

Nimevutiwa na mjadala huu na mnyukano wa BASHE na WILLIAM mnyukano ni mzuri sana unapotoka kwa watu wa MAGAMBAAAAAA HAHAHAHAHAHA.

Nimeamua kuja hapa na mimi kuonyesha ninchokifahamu kuhusu viongozi hawa wawili yaani BASHE na mzee wa TINGA TINGA.

Pia kumueleimisha william na mwisho kumpa ushauri wa bure bashe na maisha yake ya CCM ya baadae kama ambavyo tulimshauri wana mzumbe wenzie tulipokutana nae mwaka jana baada ya kuchakachuliwa.



- Mheshimiwa Bashe, heshima yako sana; kwanza kabisa ningekuomba ufungue mjadala wa Malecela, ili tuweze kujadili huu mjadala wako bila ya kutoka nje ya mada:

HOWEVER nitajaribu kukusaidia kwa kutoka nje kidogo ya mada: Malecela amekua kiongozi wa taifa toka akiwa na umri mdogo sana wa miaka 22, alianza na u-DC Tukuyu, sasa tizama kwamba katika miaka yote ya utumishi wake kwa taifa wewe na wanaokutuma hapa yaani MAPACHA WATATU, mlichonacho ni EPA over him?

Kwa hiyo unasema Malecela amekuwa muaminifu huko nyuma kote, isipokuwa akiwa mwishoni mwa utumishi wake kwa taifa, ndio kwa mara ya kwanza taama ya kuiba tena EPA ndio ikamshika?

ha! ha! ha! ha!

*Nianze na William kwanza nishukuru kufahamu huyu ndie william ambae ni mtoto wa mzee Malecela hapa suala la uadilifu la mzee wako lipo katika mashaka kama alikuzaa wewe nje ya ndoa yake (nakubaliana na hoja ya bashe kwamba wewe ni zao la kiongozi asiye muadilifu).

Tuhuma ingine ni kashfa ya helkopta feki ambazo VITHILANI ambae ni family frieand wenu mimi nikiwa ofisi ya waziri mkuu nakumbuka kupitia kamati ya ulinzi ya Bunge ambayo mzee wako alikuwa anaiongozi walishauri serekali tuingie mkataba huo ambao ni kilio kwa taifa letu. Itakumbukwa wafadhili wakuu wa kampeni za 2005 za baba yako ni VITHILANI, JITU PATEL, NA SHIVACOM, hii nituhuma ingine.

Ipo ingine inayomuhusu mzee wako inayohusiana na kina mama pale CCM na UWT nakumbuka mimi nikiwa na msafara wake yeye kama makumu mkiti ugomvi uliotokea Rukwa baada ya katibu wa UWT na afisa idara ya siasa na itikadi aliekuwa mwanamke kupigana na sisi wasaidizi kutafuta njia ya kuficha aibu hiyo.

Si hilo tu tunakumbuka mgogoro wa mzee wako na viongozi kina LONDA na Mzee mkali juu ya ANNE KILANGO,zipo tuhuma wakati wa mwalimu wafanyakazi wa TTCL walirekodi tape sita tofauti za mzee wako akitumia simu ya serekali kutongoza kina mama.

Haya ni baadhi ambayo tunayaweka hapa ,zipo tuhuma ambazo mwalimu mwaka 1995 alimwambia mzindakaya baada ya kupewa landrover 110 na fedha ambazo Malecela alipokea toka kwa viongozi wa nje kuisaidia ccm akazitia kibindoni,
KIJANA USIRUDIE TENA KUTOA KAULI KAMA HIYO HAPO JUU NA KUSEMA JE NI EPA TUU ZIPO NYINGI YA EPA NI NDOGO.

- Bashe wizi wa mali za umma ni tabia ya kwenye damu, kitabu cha Mwalimu ninacho na inaonejkana hujakisoma, ungekisoma ungejua kwamba Mwalimu hakuwahi kumtuhumu Malecela kwa kuiba anyting, lakini niambie ni mwananchi gani wa taifa hili asiyejua Mwalimu alisema nini kuhusu Bosi wako Lowassa? Alisema ni mwizi infact alimfananisha na Escobar yule M-Colombia wa maunga, amabye kazi yake ilikuwa kuuza unga na kujenga majumba, Mwalimu alisema Lowassa ni sawa yule jambazi Escobar kwa sababu Lowasaa akiwa Waziri wa Ofisi Ya Waziri Mkuu, aliiiba hela za magari ya wabunge na kujenga kijiji cha kukodi kule Arusha.

*Hili sitaki kulisemea sana kitabu cha mwalimu kiko wazi kabisa na sijui kama bashe hajasoma mm si msemaji wake,bali BASHE anauhalali wa kukitumia kuonyesha maovu ya MALECELA,mwalimu alitumia LUGHA za heshima kusema ni namna gani PM alishindwa kumshauri RAIS (MZEE MWINYI) itakumbukwa wahindi waligeuza ikulu baraza lao lakupigia soga,wahindi walivopora nchi,malecela alivuitumia nafasi yake kuifanya mamlaka dhaifu,huu ni usaliti mkubwa lkwa TAIFA HILI kuliko tuhuma zozote ambazo ziliwahi kutokea,tunajua ushiriki wa wale wahindi walioibia BOT kupitia BABA yako.KIJANA USIRUDIE.


- Kuhusu wewe sikufahamu vizuri lakini sio siri kwamba uko kwenye payroll ya nani kwa maneno yako hapa maana yanajisema wazi sana! CCM walikufukuza uongozi kwa sababu ya kutokuwa na maadili, halafu wakakuondoa kwenye kuogmbea ubunge kwa sababu huna maadili, baba yako simjui, lakini at least taifa hili lina ushahidi wa kutosha kuhusu matendo yako mabovu ukiwa kiongozi, ndio maana wakakuondoa kwenye uongozi, na sasa naona unajaribu sana kurudishwa na MAPACHA WATATU kwa sababu huku UV-CCM ndiko peke yake bado mna mikono yenu na mnajaribu kiola njia kuishikilia kwa nguvu, lakini tumeshagundua janja yenu.

*Mimi nimekuwa mwalimu wa BASHE ninamfahamu uwezo na MAPUNGUFU yake,nimekuwa makao makuu ya CHAMA ninafahamu historia ya CHAMA na VIONGOZI ,kwa watanzania wote wanaelewa,BASHE HAJAWAHI KUFUKUZWA CCM hata mara moja,inawezekana hufamu mambo mengi ya nchi yetu ndicho kilichokupelekea kumtuhumu kwamba aliwahi kufukuzwa,kama mtu mmoja alishasema watu hukurupuka juu ya jambo bila kupat taarifa,swala la bashe kuondolewa kuwa mgombea ubunge kwa TUHUMA kwamba si RAIA hii ilikuwa ni aibu kubwa kwa chama na serekali walikurupuka na baada ya siku 3 waligundua walikosea,na hapa ninampongeza kijana huyu kwa kukaa kimya na kuficha AIBU ya mzazi wake na kuamua kurudi kukisaidia chama chake nzega,ingawa sisi wana mageuzi tulimtuhumu sana kwa hilo.

Nikusahihishe HUSSEIN M BASHE hajawahi kufukuzwa ccm kwa kosa lolote,na nimefatilia hili kujiridhisha.


- Bashe mimi sio kiongozi, wewe ndiye kiongozi katika umri wako huo mdogo tayari umeshafukuzwa sehemu mbili muhimu za uongozi wa taifa, sasa unataka nini tena? Moral authority ya kukusanya maoni kuhusu UV-CCM taifa umeipata wapi? Umepewa na hawa MAPACHA WATATU, Moeral authority ya hiyo hotuba yako umeitoa wapi? only in Tanzania, ambapo kiongozi anaweza kufukuzwa mara mbili kwenye taifa na bado akaweza tena kwenda kutoa hotuba kwa ukali, akijidai kujua sana matatizo ya UV-CCM, huku tayari akiwa ameshaharibu mara mbili, unasema ninahitaji kuishi Tanzania kujua haya kwamba huna uwezo wa uongozi na huna Moral authority ya kukusanya maoni yoyote, labda ya namna ya KUWASAFISHA MAPACHA WATATU, kama unavyoonekana kujitahidi sana, you almost did it here, lakini pale uliposema lowassa anafaa na utampigia kura ndipo ulipoharibu!

*Naona kijana hili umelirudia la kufukuzwa nimekueleza na ni vizuri ukakiri kuwa bashe hajawahi kufukuzwa popote ndani ya chama,inawezekana walokupa taarifa wamekupotosha bahati mbaya ama makusudi,nikushauri pia kijana inawezekana kweli lowasa hafai kama ambavyo mwalimu alimuona MALECELA HAFAI lakini kina VITHILANI,na wengine waliona anafaa hayo maono yake na nimepitia hotuba yake sijaona wapi katika hotuba alotoa uvccm akisema lowasa anafaa angetumia hapo tungelimshamngaa BASHE,KAMA ni mawazo yake na si ya uvccm na hajawataka uvccm wamuunge mkno lowasa sioni tatizo liko wapi,kama ambavyo wengi waliona si TATIZO MKAPA ALIPOAMUA KUMKATA MALECELA yeye aliamini hafai na anaefaa ni JK.

- Infact, nina wasi wasi sana na elimu yako pia, maana ungekua nayo basi ungeelewa kwamba hapa JF wananchi tupo huru sana sio kama huko UV-CCM ulikowakomalia na B/S tupu ambazo wewe mwenyewe zimekushinda kuzitimiza kwenye uongozi ndio maana twice umefukuzwa na taifa, I understand kwamba umekuja na watu wako wengi with you hapa JF nilishafahamishwa mapema maana kwenye hayo makundi yenu huwa hamna siri, karibu sana isipokuwa nikutahadharishe one thing, maandishi hayafutiki, na mimi sio kiongozi wala sigombei nafasi yoyote ya taifa so sina anything to lose kwa kulumbana na hoja zako mbuzi sana, HOWEVER NITAKUJIBU MPAKA WANANCHI WAJIONEE WENYEWE UTUPU WAKO WA HOJA, AMBAO UNATHIBITISHA KWAMBA CCM WALIPOKUFUKUZA NAFASI ZAO ZA UONGOZI WALIKUWA RIGHT 100%, I mean wananchi hawana umeme, Tanzania tunalipa Billions zetu za kodi kwa ajili ya umeme ambao haupo, wewe unasema the master minder wa hii National demise utampigia kura maana kama ana makosa kwa nini hajachukuliwa hatua?

*Hili sitalitolea majibu kwani inawezekana taarifa ulizonazo kuwa watakuja hapa JF wengi ni za uhakika,lakini ninachofahamu BASHE JF sio mgeni ni member wa siku nyingi kama ambavyo tulisoma katika gazeti la MWANAHALISI (NADHANI UNALIFAHAMU TUNALIHESHIMU SANA HAPA TANZANIA) Mtua aneitwa MAX aliongea akawataja wana CCM wakwanza kujiunga hapa ni BASHE na NAPE ,unaposema bashe unamkaribisha nimeshangaa kidogo labda na hili umepotoshwa.

Taarifa kwamba amefukuzwa hiyo 100%umepotoshwa na bashe angetakiwa kuja kulijibu hili kiufasaha,swala la ELIMU binafsi nimekuwa mwalimu wake sina shaka juu ya elimu ya BASHE na uwezo wake wa uongozi kitu pekee ambacho nafahamu kuwa ni tatizo lake anatabia ya kusimamia anachikiamini hata kama atabaki peke yake,na mara zote huyu jamaa si NDIO MZEE,kwa tunaofahamu historia za siasa za nchi hii watakumbuka 2007,chaguzi za chama kilichomgharimu ni yeye kupingana na viongozi wa kitaifa na mkoa wake juu ya nani anaefaa kuwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa tabora,akisimamia kumuuonga mkono MZEE ANAEITWA JUMA NKUMBA wakati mtandao ukisema hafai kwakuwa NGUMBA aliwapinga ,nikiwa idara ya uchaguzi CCM makao makuu na Mzee CHIZIII tulimshauri bashe akae mbalina uchaguzi ule akasema atasimamia anachoamini bila kujali nani anampinga huyo mzee.tunafahamu kilichotokea
.

- Lakini unashindwa kujibu swali dogo sana kwamba kwa nini bosi wako unayejaribu sana kumsafisha hapa Lowassa alikimbia kule Bungeni U-Waziri Mkuu bila kufukuzwa?

*Hapa kuna upotoshaji,BOSI WA BASHE si LOWASA tunafahamu si muajiriwa wake,kama tafsiri ya BOSI inatafsiriwa kwa yeye kusema anamuunga mkono lowasa basi umepotosha kija ukweli wa tafsiri hii,balitukijadili kwanini lowasa hakujitetea,inahitaji muda mrefu kulijadili hili kijana muulize mzee malecela ,mwakiembe,samwel sita,wanajua ukweli wa hili,na siku ukimuona MH KIKWETE huko ulaya muulize atakueleza ni SIRI NZITO YA TAIFA LETU.

*ndg wiliamu usinichukulie kama msemaji wa bashe,usinichukulie nimenunuliwa kwani hapa nimeona tayari kila anaekuwa na mtazamo tofauti amenunuliwa.
 

Hapo kwenye Red Ina maana Lowassa hapelekwi mahakamani pamoja na makosa yote aliyonayo kwa vile yuko CCM?
 
very interesting, malecela ana m challenge Bashe kwa kuongelea mambo binafsi kabla hajamaliza na yeye anamshughulikia bashe kwa mambo binafsi, na nilichokiona mdogo wangu malecela nae na hasira nzito inawezekana ni baada ya baba yake kunyukwa vibaya alipoiota ikulu hivyo nae ana fanya lile lile tukose wote, moral authority ya mawazo hayo kwa michango yako unaitoa wapi? kwa wale wasiofahamu tu ni kwamba pamoja na mapungufu yote ya EL hajapatikana Pm hadi leo ukimtoa Moringe aliyefanya kazi na serikali ikawa na heshima kabla ya mbinu chafu za richmond hazifanya kazi yake!
 
Best informative thread of the month!
 

- Ha! ha! ha! ha! ha! ha!, Mheshimiwa Bashe Bashe! ha! ha! ha! ha! ha!, Message sent and delivered, & received!

William @ NYC, USA.
 


- Kwa kweli Mheshimiwa sana Bashe, umesikika na kueleweka sana, karibu sana tukate ishus na tuelimishane zaidi na UBARIKIWE SANA NA MUNGU WA MBINGUNI!

william @ NYC, USA.
 
Bashe: Nikutoe shaka juu ya jambo moja: Sina historia ya kuficha wala kutafuna maneno katika jambo ninaloliamini

Mjadala umefungwa au! Nachangia kidogo nikiwa nje ya 'family feud'

Ndugu Bashe, Naomba unishahihishe kama nitakuwa nimeelewa baadhi ya mambo kinyume, lengo langu ni kupata ufafanuzi ili kuondoa maneno yasiyo na uthibitisho au utata.
Kwa vile umejitokeza nashukuru endapo utajibu hoja hapo juu na zitokanazo na thread.

1. Wewe umezaliwa Nzega umekulia na kusomea Tanzania ukitumia respources zote kama raia.
Mwaka 2009(kama sijakosea) ukiwa unajiandaa kugombea ubunge ulienda mahakamani ili kupata uraia wa Tanzania.

Swali: Ukiwa unajiamini, ni kwanini ulienda kuomba uraia ili hali ukijua wewe ni raia? Je hapo si kutafuna maneno. Je unajiamini kwa lipi endapo hukuweza kujiamini kwa yanayokuhusu.

2. Kama unajiamini, katika hotuba yako umetumia maneno ' CCM kutokuwa na social justice'.
Tafadhali tufanunulie ni social justice ipi na ushahidi gani unao wewe wa kuonyesha kuwa
social justice haipo ndani ya chama chako.

3. Katika hotuba yako umesema kuwa CCM isijiingize katika majadiliano kama kudai watu fulani
ni mafisadi. Umesema CCM ijikite katika kujibu hoja za wananchi.

Swali: a)Unataka umma uelewe kuwa ufisadi si sehemu ya hoja za wananchi na wana CCM?

b)Je si kweli kuwa ufisadi ndio unaoipunguzia CCM umaarufu na kwamba ni muhimu
kuushughullikia.
c)Kama chama chako hutaki kiongelee ufisadi, utawezeja kuendeleza sera za chama huku
kikundi cha watu wachache ndani ya chama kikihodhi chama na serikali kwa maslahi
binafsi ?

Nipo tayari kusahihishwa.
 
Maajabu sana katika hii nchni yetu! Rais aliwai kusema kuwa huyu Jamaa si Raia tena alitangaza na nchni nzima mkamsikia, Rais haitendei haki nchni yake hata hii tabia ni magamba inapaswa kuondolewa ndani ya CCM na Ikulu inakuwaje Rais useme kitu alafu kionekane kama kituko!

Ujasiri na Kiapo cha kulinda katiba na mipaka ya Jamhuri ya Tanzania bila woga upo wapi?!


KAKA HAYO NI MATUNDA YA UPEO MDOGO WA RAIS WETU KUFIKIRI, for a serious president when you talk about something ni kwamba unauhakika nacho na especially intelingisia yako iko makini. Tanzania inteligensia ipo kwenye kuzuia maandamano na si kumpa rais concrete issues azungumze hadharani, waziri anasema si raia, uhamiaji wanasema raia na passport wamempa na rais anakuja kusema sio raia yaani inakereketa kweli kuona how serious the govt is not!! uswahili swahili sijui kwa nini nyerere aliing'ang'ania kyela saa hizi ningekuwa malawi!!
 
Hapo kwenye Red Ina maana Lowassa hapelekwi mahakamani pamoja na makosa yote aliyonayo kwa vile yuko CCM?

Reffer kauli ya Fredrick T. Sumaye - " Ukitaka mambo yakunyookee ingia CCM", end of quote.
 

- Well, MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA PIA AIBARIKI SANA JF!

William @ NYC, USA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…