UVCCM Arusha watoa tamko zito! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM Arusha watoa tamko zito!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Mar 28, 2011.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  MAAZIMIO YA BARAZA LA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

  MKOA WA ARUSHA – LONGIDO

  UTANGULIZI
  Kikao cha baraza la vijana la mkoa wa Arusha kilichokaa leo tarehe 28 Machi 2011, wilayani Longido kama ambavyo taratibu na kanuni za UVCCM zinavyoelekeza. Hili likiwa ni baraza la kwanza kufanyika baada ya uchaguzi mkuu wa 2010, tunapenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete kwa ushindi alioupata na pia kuwapongeza wabunge na madiwani wote wa Chama Cha Mapinduzi na kuwahakikishia kwamba kama vijana tupo tayari kukabiliana na changamoto zote tulizokutana nazo kwenye uchaguzi na tutafanya kazi bega kwa bega kuhakikisha tunafanikisha vizuri zaidi chaguzi zijazo.

  Hili lililikuwa ni baraza la kawaida la kazi na agenda kadhaa zilijadiliwa. Kufuata majadialiano yaliyoendelea kwenye kikao, Baraza la Mkoa wa Arusha limeazimia yafuatayo:

  MAAZIMIO


  1. Baraza limesikitishwa sana na kauli zilizotolewa na baadhi ya vijana wa UVCCM wakianza kuhubiri siasa ya kibaguzi wa makabila kwa kutoa matamko kwambaRais 2015 asitoke kanda ya kaskazini,Baraza linachukua fursa hii kuwaonya vijana wenzetu hao wanaopotoka, na labda kama ambavyo wamekumbushwa juzi, tuwaambie tena kwamba Rais wa awamu ya kwanza Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitokea mkoa wa Mara (KANDA YA ZIWA), Rais wa awamu ya pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi alitokea Zanzibar (VISIWANI), Rais awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa alitokea Mtwara (KANDA YA KUSINI) NA Rais wetu wa sasa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete anatokea mkoa wa Pwani (KANDA YA PWANI), sasa kama hawa vijana wenzetu wangetaka watanzania wafanye uchaguzi kwa kuangalia maeneo ambayo viongozi hao wanatoka, basi tungetegemea waseme sasa kwamba 2015 ni zamu ya Rais kutokea KANDA YA KASKAZINI AU, NYANDA ZA JUU KUSINI, na tunaamini kote huku kuna viongozi mahiri na makini wenye uwezo wa kuongoza nchi vizuri kabisa, lakini sisi kama vijana weledi wa CCM na tuliolelewa vizuri kwenye misingi thabiti ya nchi yetu ya UMOJA na AMANI, hatuamini hata siku moja kwenye kuchagua viongozi kwa kuangalia Rangi, Dini au kabila, Baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishaonya kwa ukali sana kuhusu ubaguzi wa aina yoyote, sisi tunaamini kila Raia wa Tanzania kutokea upande wowote ule wa nchi anayo haki ya kikatiba ya kuwania nafasi ya URAIS na wananchi wa Tanzania watampima kwa rekodi yake ya uongozi na uwezo wake wa kutatua matatizo ya wananchi, hii ndiyo Tanzania tunayoifahamu sisi kama vijana wa Chama Cha Mapinduzi.


  2. Mkoa wetu wa Arusha ni mkoa uliobarikiwa kwa kuwa na rasilimali nyingi sana na tunamshukuru Mwenyezi Mungu, na mojawapo ya rasilimali hizo ni pamoja na madini ya tanzanite na vivutio vingi vya utalii, na hivi vyote vinahitaji Tanzania kama nchi iweze kutangazwa vizuri KIMATAIFA ili mkoa wetu na taifa tuweze kupata manufaa zaidi kwa rasilimali tulizonazo na moja ya nyenzo muhimu katika kutangaza nchi ni pamoja kuwa na "National Carrier" yako, ambayo inakuwa ni shirika la ndege ambazo serikali ina hisa na shirika hilo linabeba jina la nchi na linapeperusha bendera ya taifa popote pale linapokwenda duniani. Kwa masikitiko makubwa sana na kwa kipindi kirefu, nchi yetu Tanzania tumekuwa na Shirika letu la ATC, ambalo kipindi fulani lilikuwa linarusha ndege mpaka Heathrow, London – Uingereza, lakini shirika hilo leo limekuwa kama mtoto yatima. Sisi vijana tunajiuliza, kama mjasiriamali mzawa amefanikiwa kuendesha shirika lake la PRECISIONAIR kwa mafanikio makubwa, serikali inashindwaje kuendesha ATC? Kama vijana wa mkoa wa Arusha tunaungana na kamati za Bunge na tunaitaka serikali kusimamia hili jambo kwa makini, nasiyo kwa kuinyima ATCL ruzuku tu, bali kuanza kwa kuvunja Bodi ya wakurugenzi na menejimenti yote, hivi sasa ni AIBU KUBWA kwa nchi, tunaomba watuondolee aibu hii haraka iwezekanavyo. Haiingii akilini kama nchi ndogo na tena ambazo zimetoka vitani hivi majuzi kama Rwanda, Burundi na Comoro, wao waweze kuendesha mashirika yao ya ndege zilizobeba majina ya Mataifa yao na sisi kama nchi yenye rasilimali nyingi kiasi hicho tushindwe kuendesha shirika letu la ATCL.


  3. Agenda mojawapo ya kikao chetu ilikuwa ni tathmini ya uchaguzi, na kama baraza tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza viongozi wote wa wilaya za mkoa wa Arusha kwa kufanikisha uchaguzi mkuu vizuri sana na kufanikiwa kushinda majimbo ya uchaguzi matano kati ya saba, tunawapongeza sana. Na pia kusimamia kura za Mwenyekiti wetu wa Chama, Jakaya Mrisho Kikwete kushinda vizuri mkoani kwetu Arusha, tukiongozwa na wenyeji wetu wa kikao chetu wa jimbo la Longido ambaye Rais alipata 85% na tukifuatiwa jimbo la Monduli ambapo Rais alipata asilimia 84%, lakini pamoja na kuwapongeza viongozi waliosaidia kufanikisha uchaguzi mkuu, lazima pia kulaani viongozi wa chama waliotumika kukihujumu chama wakati wa uchaguzi na kutusababishia kushindwa vibaya kwenye majimbo mengine na kumpunguzia sana kura Mhe. Rais wetu, na sisi kama vijana tunasema hatutavumilia viongozi wa namna hiyo, na kwa kuonyesha mfano, na kwa kutekeleza maazimio ya baraza kuu la UVCCM lililokaa wiki iliyopita, baraza limeamua kumsimamisha Ndg. Gambo Mrisho kwa kushiriki kukihujumu chama katika jimbo la Arusha mjini na kuendelea kutoa maneno ya kashfa kuhusu Chama na aliyekuwa mgombea wa Chama chetu Jimbo la Arusha Mjini Dr. Batilda Buriani kwenye maeneneo mbalimbali na hata kwenye ofisi ya UVCCM mkoa mbele ya viongozi wengine wengi, hii ni dhambi ambayo haisameheki na kwasababu hiyo, Baraza limeazimia kuwa kijana huyu siyo mwenzetu na tunamuomba Mwenyekiti wa CCM Taifa kulivalia njuga suala hili kwa maeneo mengine ya nchi ili viongozi wote waliokihujumu chama watupishe mapema, twende tukijiandaa na uchaguzi wa 2015 na wanachama ambao tunaamini wapo tayari kufa kwa kutetea imani za Chama Cha Mapinduzi. Tunaamini kama isingekuwa kwasababu ya viongozi wasaliti kama hawa, Mhe Rais Jakaya Mrisho Kikwete angepata ushindi mkubwa zaidi kuliko ushindi alioupata wa asilimia 61% kwenye uchaguzi mkuu 2010.


  4. LOLIONDO – ‘KWA BABU', hii imekuwa moja ya vivutio vikubwa sana hapa mkoani kwetu Arusha kwa wananchi kutoka mikoa mbalimbali na hata nje ya nchi kwenda kupata ‘kikombe' kwa babu Loliondo. Tunaelewa na kuheshimu kwamba hili ni suala la imani ya mtu binafsi kwenda Loliondo kwa babu, lakini sasa inapotokea kwamba inaweza kugeuka kuwa janga la kitaifa, sisi kama viongozi hatupaswi kuendelea kukaa kimya tena. Kuna taarifa zinazosema kuwa watu 10-15 wanafariki kila siku wakiwa wanaelekea kwa babu, na tumeona taarifa za mikutano ya wakuu wa mikoa tofauti wakikaa kutafuta suluhisho, na sisi kama vijana wa mkoa wa Arusha tunaitaka Wizara ya Afya kupitia halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kutoa suluhisho haraka iwezekanavyo kwa kusimamia kuboresha miundombinu na siyo kuwaachia KANISA na watumishi wa Babu au kama sivyo kusitisha huduma mpaka miundombinu itakapokuwa tayari na wagonjwa wote warudishwe mahospitalini. Hii ni hali ya hatari ambayo inapaswa sasa kufanyiwa maamuzi magumu.


  5. BARABARA YA ARUSHA – NAMANGA, tunapenda pia kutoa pongezi sana kwa Serikali ya CCM kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi, leo vijana wote walioshiriki baraza hili na kusafiri kutokea Arusha mjini wamejionea kazi nzuri inayoendelea ya barabara ya Arusha-Nairobi na kama siyo taratibu za watu wa uhamiaji mpakani, tunaamini sasa unaweza kufika Nairobi kwa masaa mawili tu, na hii tunaamini ndiyo itawasaidia watanzania kuweza kunufaika zaidi na fursa za shirikisho la Afrika Mashariki. Kwa mafanikio kama haya na mengi mengine, tunaamini kabisa wananchi wataendelea kuwa na imani na Chama Cha Mapinduzi na tutashinda uchaguzi mkuu wa 2015 kwa kishindo zaidi.


  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


  JAMES OLE MILLYA
  MWENYEKITI UVCCM - MKOA WA ARUSHA
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mmhhh ...!!!!

  Nitarejea baadaye mara baada ya kufanyia upasuaji wa kutosha mawazo yenu enyi vijana wenzetu lakini mjue mpaka hivi sasa UVCCM kuna picha mbaya sana ya kupigana nayo kitaifa ndipo mtu yeyote serious aweze kuipa muda mnachosema katika matawi yenu.

  Hata hivyo naamini JF itawatendeeni haki stahiki UVCCM Arusha, tupeni muda kidogo kupitia makabrasha yote na tupime kama hakuna harufu ya Bahasha ya Khaki nyuma ya haya mnayotuambia.
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Edward Lowassa @ work, wanauma nakupulizia tu, binafsi sitegemei jambo lolote jema kutoka CCM. Huyo mwenyekiti wao Milya ni karani wa Lowassa.
   
 4. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,199
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 160
  Sarakasi tupu.

  Ukionja nyama ya mtu huwezi kutamani kuiacha, Nyerere alipata kusema. Baada ya kusema sana kwamba CDM ni chama cha kaskazini na propaganda hizo kushindwa sasa ni zamu ya CCM kubaguana.

  Tunasubiri Pwani nao wajibu baada ya kuelekezwa na Ridhiwan au Mkuu mwenyewe
   
 5. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbona iko shallow kama Post za baadhi ya watetezi wa CCM hapa jamvini?

  Halafu nilidhani hawa watoto wa vigogo wa CCM wamepelekwa shule nzuri, kumbe hawajaelimika? Kujenga hoja sifuri hata matumizi ya punctuation sifuri!
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mwendo huu wa vijana ndani ya CCM utakuja kufumua mengi tusiyotarajia. Watch this space! Makamba atakuja na majibu kwao soon (guessing)
   
 7. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ni hao hao SISI EEEE MMMMMM Vijana na staili tofauti tofauti za matamko. Kama ilivyokwisha bainishwa awali, vijana wa CCM wengi hawajui historia na wala hawana utashi juu ya yale wanayotaka umma wa watanzania wayasikie.

  Sina shaka kufikia hitimisho kuwa wanahitaji kuwa na uongozi unaojua vizuri atahri ya haya wanayoendelea kuyatamka na sio staili ya watu kama akina Beno Malisa, Ridhiwan JK wala Shegela. Wanahitaji kuwa na viongozi mwenye dira na upeo wa kuwaongoza kwa dhati na si kwa mitizamo finyu iliyojaa ubinafsi, uroho wa madaraka na hulka ya kutumiwa kama "kisemeo" cha Mafisadi.

  Kwa hali halisi ni kudhihirisha kuwa si Umoja huo tu uliosambaratika bali pia Vikao vikuu vya chama hicho hasa ukifuatilia haya ya Sumaye, Sitta, Rostam, Mwakyembe na Makamba. Na sio chama chao tu, hata Serikali ya Chama hicho haina uhakika ya yale inayofanya hasa ukifuatilia ya Mhe. Presida, Pinda na Magufuli au Mhe. Presida na Watendaji wa Wizara zake kwenye hii ziara anayoendelea nayo ambapo ana lazimika kuwaanika watendaji wake hadharani kana kwamba hakuna mawasiliano ya ndani ya kumwezesha Mkuu kujua yale ambayo aliyaagiza yatekelezwe au yaliyo katika Ilani ya chama chao.
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tamko liliandaliwa hata kabla ya kikao na wao kule Longido walienda kupiga soga tu!! Kazi kweli kweli na viongozi wetu watarajiwa.

  Hoja kuu zilikua namba moja na namba tatu na hii namba tatu kwanza hawajajenga hoja ya tuhuma,lkn pia hawajasema wanamvua uongozzi gani japo hawana mamlaka ya kufanya hayo.

  Jambo kubwa ambalo hawajaligundua ni kwa CCM kujimaliza kwenye kesi ya msingi dhidi ya Lema maana sasa CCM wamemtaja aliyemhujumu Dr Batilda ambaye ni Gambo lakini katika kesi yao mahakamani hajatajwa kwa tamko hili Lema anaweza kutumia maazimio hayo kumaliza kesi.

  Kosa kubwa la Gambo ni kumsema Lowassa na RA pamoja na mtetezi wao DC wa Bunda Francis Isaac aliyeambiwa anafikiri kwa tumbo.... Kazi kweli kweli
   
 9. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lowasa atamaliza kazi yake lini?Kwa mtindo huu vijana hawatapumzika.
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Things are falling apart because the arrow of God is No Longer at Ease!

  Hivi hakuna Central Command ya UVCCM?...maana kilichopo sasa ni ...Vijana wa Arusha...Vijana wa Pwani...Vijana wa Dar..Vijana wa Tabora..kila upande wakitoa matamko yao , na zaidi kutumika na wenye nia zao!
  Umoja wa vijana ccm ni kikundi cha hatari sana kwa sasa kuliko ilivyowahi kuwa katika historia ta Tanzania. Wamekuwa litmus papers wakitumika kupima legibility na illegibility za watu!
  Ziko wapi enzi za TANU YOUTH LEAGUE?....Uko wapi Uzalendo?
  Je chama cha Mapinduzi na UONGOZI wake wamesafiri kuelekea nchi gani?...Mbona hawarudi?...

  The Episode to be continued!......
   
 11. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Msimuue tu kama ambavyo mmeshamtishia!
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Nasubiri UVCCM Mwanza halafu na UVCCM Mbeya na wenyewe!! Jamani, can't they just break this party waanze moja?
   
 13. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #13
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kazi ipo..Lowassa katumia kipaza sauti chake!..Maneno ya Gambo yamemuingia sawia!
   
 14. n

  nndondo JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Hongera sana mdogo wangu Gambo, umesema kweli vijana hawa wote wanafiki watageuka wachawi kama hao wakina lowasa mara watakapogikia umri wake, shit kabisa wanatia kinyaa, Millya nae anaongea? makubwa mwaka huu ama kweli tutaona paka kavaa raizoni na mbwa kakaa high table, yote hayo ni mambo ya CCM 2015 hawakumbuki kwamba wembe ni ule ule ulionwanyoa mwaka jana mpaka wakaiba mpaka kura za maruhani, kiboko yao slaa na chadema peoples power kwa kwenda mbele
   
 15. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa hajamaliza hata mwaka mmoja katika awamu hii ya pili ya Urais, jamaa zake wanataka kutoana macho. Lazima wamkumbuke Kolimba, aliwaambia hawana dira walibisha sana. Sasa JK kila siku anasikia matamko ya vijana. Lazima mvi zimkote mtu mzimaa awamu huu
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kauli ya vijana wa UVCC Arusha imetulia. Sijaona viluilui ndani ya maji machafu kama ile ya Umoja wa vijana wa CCM kitaifa.
  Hilo ndilo lilitakiwa kuwa tamko la umoja wa vijana wa ccm kitaifa.

  Wamejitahidi kutumia vizuri mfumo wa saikoloji na kukwepa siasa za kuchimbiana mikwara. Ndio mambo tunayotaka.
  Kwa mtazamo wangu hapa kauli vijana hawa imewaaibisha sana baadhi ya viongozi wa ccm kitaifa kama akina Makamba, Chilingati nk.
  Kauli yenye mvuto na busara kama hiyo ilitazamiwa kutolewa na viongozi wa kitaifa wa umoja wa vijana na uongozi wa ccm kitaifa.
   
 17. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #17
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Gambo-facebook.com 2011-3-29 0-8-15.jpg

  Gambo2-facebook.com 2011-3-29 0-26-30 (2).jpg Gambo1-facebook.com 2011-3-29 0-26-30 (1).jpg

  Kutoka kwenye ukuta wake wa surakitabu (facebook)....mmh!...hiyo ya kuuwawa ni hatari sasa tunakoelekea!
   
 18. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
 19. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  ccm diee ccm die ccm kufaaa unasubiri nini hata kwa kikombe cha babu hutaponaaaaa
   
 20. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Millya ndiye aliyeandika barua kwa aliyekua Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula kabla ya mwaka 2005 akilalamika kutishwa na Lowassa kuwa aache kumsaliti kwani yeye ni ndugu yake na anapaswa kumuunga mkono kama anataka mambo yake yanyooke. Millya alimwambia Mangula kwamba Lowassa alimwambia kwamba ameshakubaliana na Rais Mkapa kwamba JK atakua Rais na yeye (Lowassa) atakua Waziri Mkuu na Millya ataaibika. Lowassa akamsihi ajinge naye na asimsaliti.

  Mazungumzo hayo yalifanyika nyumbani kwa Lowassa baada ya Millya na viongozi wenzake wa Dodoma, Kilimanjaro, Dar es Salaam na mikoa mingine kutoa matamko kumpinga Kikwete. Baadae ni Millya ambaye amekuja kumbana Lowassa na alionekana kama tishio kuelekea 2010 kabla ya kubwaga manyanga na kumwachia na hatimaye kumuunga mkono Lowassa. Je, Millya ametishwa tena? Na safari hii ameambiwa nani ni Rais na nani PM? Je, Millya hataki kupoteza tena kama alivyompinga JK? Ama 2005 alitumwa na Lowassa kumpinga JK kiana na sasa kazi iliisha na anapaswa sasa kuingia ndani tena?

  Jamani kama unaamini kwamba hili tamko ni halali na Lowassa ameonewa, karibu sana utapata majibu humu
   
Loading...