UVCCM Arusha watoa tamko zito!

Naona kampeni za uchaguzi zimeanza mapema this time around, vizuri sana, hivi kadi ka kupigia kura tunaenda kuzipata wapi, maana wengine majina yetu hayakuwepo kwenye list iliyopita.
 
tfa.jpg
Turning and turning in the widening gyre
The falcon cannot hear the falconer;
Things fall apart; the center cannot hold;
Mere anarchy is loosed upon the world.
KWAHERIHI CHAMA CHA MAPINDUZI HATA MFANYAJE MAJI YALISHAMWAGIKA
GOD BLESS TANZANIA TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA. MAKOFI TAFADHALI
 
Mimi naona Mrisho Gambo alizungumza ukweli, lakini bahati mbaya ukweli si maarufu tena kwa Milya na wana mtandao. Sasa watu tunahitaji kujua mchezo unavyoendelea. Kuna uwezekano mkubwa wa, badala ya CCM kuvunjika, nchi yetu itapatwa na misukosuko mikubwa hapo mbeleni. Sabau kubwa ni hizi 1. Haki haitakiwi 2. Ukweli unafunikwa kwa nguvu nyingi 3. Demokrasi haitakiwi 4. Pesa, Uchawi, Umafia nk ndio silaha yao (mafisadi)
 
Duh!Kwa hiyo babu wa Loliondo nae kawa agenda ya kisiasa??Hamna agenda zingine za maana zaidi ya hiyo??

KWani hujui? Ndio maana Wakuu wa Mikoa wanaenda kwa gharama za serikali na walikuwamo viongozi wa vyama maana na Ndesamburo naye alienda lakini yeye nadhani Chadema hawajihusishi
 
MAAZIMIO

  1. Baraza limesikitishwa sana na kauli zilizotolewa na baadhi ya vijana wa UVCCM wakianza kuhubiri siasa ya kibaguzi wa makabila kwa kutoa matamko kwambaRais 2015 asitoke kanda ya kaskazini,Baraza linachukua fursa hii kuwaonya vijana wenzetu hao wanaopotoka, na labda kama ambavyo wamekumbushwa juzi, tuwaambie tena kwamba Rais wa awamu ya kwanza Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitokea mkoa wa Mara (KANDA YA ZIWA), Rais wa awamu ya pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi alitokea Zanzibar (VISIWANI), Rais awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa alitokea Mtwara (KANDA YA KUSINI) NA Rais wetu wa sasa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete anatokea mkoa wa Pwani (KANDA YA PWANI), sasa kama hawa vijana wenzetu wangetaka watanzania wafanye uchaguzi kwa kuangalia maeneo ambayo viongozi hao wanatoka, basi tungetegemea waseme sasa kwamba 2015 ni zamu ya Rais kutokea KANDA YA KASKAZINI AU, NYANDA ZA JUU KUSINI, na tunaamini kote huku kuna viongozi mahiri na makini wenye uwezo wa kuongoza nchi vizuri kabisa, lakini sisi kama vijana weledi wa CCM na tuliolelewa vizuri kwenye misingi thabiti ya nchi yetu ya UMOJA na AMANI, hatuamini hata siku moja kwenye kuchagua viongozi kwa kuangalia Rangi, Dini au kabila, Baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishaonya kwa ukali sana kuhusu ubaguzi wa aina yoyote, sisi tunaamini kila Raia wa Tanzania kutokea upande wowote ule wa nchi anayo haki ya kikatiba ya kuwania nafasi ya URAIS na wananchi wa Tanzania watampima kwa rekodi yake ya uongozi na uwezo wake wa kutatua matatizo ya wananchi, hii ndiyo Tanzania tunayoifahamu sisi kama vijana wa Chama Cha Mapinduzi.
Huu ndio msingi mkuu wa yote yanayotokea, Urais wa 2015, wanagombea Lowassa na Sumaye na kila mmoja anaona anafaa na sasa wanaanza kutafunana wenyewe na wote wanarudia mbinu zile zile za mwaka 2005 ambako UVCCM walianza Dodoma kutumika. Hapa wanataka kutuambia wazi kwamba Lowassa ndiye Rais afaaye na ukiangalia mtiririko wa taarifa hadi hitimisho la kusema "....Tutashinda Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kishindo zaidi." uitana wazi wanakolenga na mkakati mzima wa kikao na mchakato wote ikiwamo kikao cha Impala kupanga mikakati wakiongozwa na Fred EL na kufadhiliwa na EL na Ole Medeye.

Agenda mojawapo ya kikao chetu ilikuwa ni tathmini ya uchaguzi, na kama baraza tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza viongozi wote wa wilaya za mkoa wa Arusha kwa kufanikisha uchaguzi mkuu vizuri sana na kufanikiwa kushinda majimbo ya uchaguzi matano kati ya saba, tunawapongeza sana. Na pia kusimamia kura za Mwenyekiti wetu wa Chama, Jakaya Mrisho Kikwete kushinda vizuri mkoani kwetu Arusha, tukiongozwa na wenyeji wetu wa kikao chetu wa jimbo la Longido ambaye Rais alipata 85% na tukifuatiwa jimbo la Monduli ambapo Rais alipata asilimia 84%, lakini pamoja na kuwapongeza viongozi waliosaidia kufanikisha uchaguzi mkuu, lazima pia kulaani viongozi wa chama waliotumika kukihujumu chama wakati wa uchaguzi na kutusababishia kushindwa vibaya kwenye majimbo mengine na kumpunguzia sana kura Mhe. Rais wetu, na sisi kama vijana tunasema hatutavumilia viongozi wa namna hiyo, na kwa kuonyesha mfano, na kwa kutekeleza maazimio ya baraza kuu la UVCCM lililokaa wiki iliyopita, baraza limeamua kumsimamisha Ndg. Gambo Mrisho kwa kushiriki kukihujumu chama katika jimbo la Arusha mjini na kuendelea kutoa maneno ya kashfa kuhusu Chama na aliyekuwa mgombea wa Chama chetu Jimbo la Arusha Mjini Dr. Batilda Buriani kwenye maeneneo mbalimbali na hata kwenye ofisi ya UVCCM mkoa mbele ya viongozi wengine wengi, hii ni dhambi ambayo haisameheki na kwasababu hiyo, Baraza limeazimia kuwa kijana huyu siyo mwenzetu na tunamuomba Mwenyekiti wa CCM Taifa kulivalia njuga suala hili kwa maeneo mengine ya nchi ili viongozi wote waliokihujumu chama watupishe mapema, twende tukijiandaa na uchaguzi wa 2015 na wanachama ambao tunaamini wapo tayari kufa kwa kutetea imani za Chama Cha Mapinduzi. Tunaamini kama isingekuwa kwasababu ya viongozi wasaliti kama hawa, Mhe Rais Jakaya Mrisho Kikwete angepata ushindi mkubwa zaidi kuliko ushindi alioupata wa asilimia 61% kwenye uchaguzi mkuu 2010.

Kwanza tatizo la Arusha si Gambo ni Batilda mwenyewe na tatizo la Gambo si uchaguzi wa 2010 bali 2015 na tatizo si amekichafua chama bali amemchafua Lowassa na tatizo si UVCCM bali tatizo ni CCM na uongozi mzima wa chama hicho kuanzia Taifa hadi mkoa wa Arusha. Hapa ndio tujue JK kwa kuendelea kulea tatizo mambo yatamharibikia yeye mwenyewe na jamaa watamshughulikia kwa sana.
 
Mwendo huu wa vijana ndani ya CCM utakuja kufumua mengi tusiyotarajia. Watch this space! Makamba atakuja na majibu kwao soon (guessing)
Pinda nae ameonya majibizano ya mambo ya chama kwenye vyombo vya habari kwa kutumia vyombo vya habari!!!
 
pinda angetumia vikao vya chama kuwaonya sumaye na uvccm,lakini ametumia vyombo hivyo hivyo.
 
mmmmh yetu macho, sasa hivi hiyo timu haina kiongozi, kila mtu anapiga mpira directions tofauti, huyu kule na huyu hapa, yaani ni tafrani.
Kuiweka sawa yataka busara ya hali ya juu na si kazi ndogo, tuwaombee Mungu awanusuru kwani ni kama train ambayo inakaribia kudumbukia mtoni kwani daraja mbele yake limekatika na haiwezi simama ghafla kama gari!
 
Itatuchukuwa muda gani kugundua kwamba kiongozi wa nchi kisha pata tatizo la akili?
Je, ni nani anastahili kuamua kwamba afya ya Rais sasa hivi haimuruhusu kuendelela na kazi yake?

Sioni dalili kwamba sasa hivi kuna kiongozi wa nchi.
 
Mwendo huu wa vijana ndani ya CCM utakuja kufumua mengi tusiyotarajia. Watch this space! Makamba atakuja na majibu kwao soon (guessing)
mkuu makamba hatoi jibu lolote kwa sasa anajua akitoa anaongea pumba tuu!
 
Tamko hili ni jepesi lisilolingana na matarajio ya viongozi wa mwaka kesho au keshokutwa. Limeandikwa kwa maneno mengi likiwa na maudhui hafiifu.

1. Kuhusu ubaguzi, hakuna sababu ya kutafuta kiongozi kwa kuzingatia ukanda, hatujawa Nigeria au jirani zetu.
Jambo nilisolijua ni kuwa hivi rais akitoka kanda fulani inakuwaje? nini maana yake kwa maendeleo na maisha kwa ujumla.Nilishawahi kuishi na waziri wa awamu zote, lakini sikuona alibadilisha vipi maisha yangu.

2. ..........................

We jamaa acha utani. Huoni Chalinze sasa hivi angalau ina nyumba mbili za gorofa? Tena karibu na barabara! Pwani siku hizi hatumwagi 'razi.' Tunalinda heshima ya mwenzetu ikulu!
 
sioni sababu ya kumbebesha Lowasa suala hili, hali ni mbaya tu ndani ya CCM na UVCCM hawataki kubaki nyuma na kuburuzwa. Kama alivyosema Mwanakijiji nami nasubiri matamko zaidi kutoka kanda zingine.
 
Back
Top Bottom