UVCCM Arusha watoa tamko zito!

Duh!Kwa hiyo babu wa Loliondo nae kawa agenda ya kisiasa??Hamna agenda zingine za maana zaidi ya hiyo??
 
Mwendo huu wa vijana ndani ya CCM utakuja kufumua mengi tusiyotarajia. Watch this space! Makamba atakuja na majibu kwao soon (guessing)

Ilikuwa niseme kama hivyo, na zaidi, natarajia mikoa mengine wataandaa vikao kupinga:hatari:au kuunga mkono:lol: mfululizo wa hoja hizi.
Mimi, langu jicho.
 
Tamko hili ni jepesi lisilolingana na matarajio ya viongozi wa mwaka kesho au keshokutwa. Limeandikwa kwa maneno mengi likiwa na maudhui hafiifu.

1. Kuhusu ubaguzi, hakuna sababu ya kutafuta kiongozi kwa kuzingatia ukanda, hatujawa Nigeria au jirani zetu.
Jambo nilisolijua ni kuwa hivi rais akitoka kanda fulani inakuwaje? nini maana yake kwa maendeleo na maisha kwa ujumla.Nilishawahi kuishi na waziri wa awamu zote, lakini sikuona alibadilisha vipi maisha yangu.

2. ATCL ni kweli ni aibu kubwa sana,lakini kumbu kumbu zinaonyesha walishawahi kubahatika kuwa na mawaziri wakuu wawili ambao ATCL imefia mikononi mwao. Je walishawahi kuongea nao kama wabunge wao ambao ni wakuu wa serikali kuhusu suala hili?

3. Uchaguzi: hapa hakuna hoja, wamejaribu kukwepa ukweli kwa kuhofia mzee. Kama Gambo aliwahujumu, vipi Mwanza waliwezaje kuwa na wabunge wawili, Sugu na Mdee waliwezaje kushinda majimbo moto, je Gambo alikuwepo huko.? Walitakiwa waeleze kina cha kushindwa ikiwa ni pamoja na kashfa za rushwa kama mbunge wao EL alivyozisababisha. Wameogopa rushwa ili wasimguse mzee.

4.Miundo mbinu: Kama wamekubali ni suala la imani, walichotakiwa ni kusisitiza uboreshaji miundo mbinu mkoani Arusha. Sidhani ni vema pesa za umma zikatumika kwasababu ya Babu, je ikidhirika kuwa ni kinyaboa itakuwaje! Maendeleo ni shughuli endelevu(sustainable) na si matokeo ya (reaction to).

5. Namanga-Nairobi: Walitakiwa watuambie ubora wa barabara hiyo utawasaidiaje wao kuboresha maendeleo yao, na je wanajipangaje kutumia fursa ya Arusha kuwa makao makuu ya E.A. Wangependekeza nini kutumia fursa hiyo. Bara bara bila mipango endelevu kwa wao haina tija zaidi ya kuona Benz zikikruzi kuelekea Arusha au Dar.

Mwisho: Tutegemee tamko gani kutoka kwa Millya, aliyemuomba radhi Lowassa kwa kitendo chake cha kutaka kutumia haki yake ya kidemokrasia kugombea ubunge!!
 
Things are falling apart because the arrow of God is No Longer at Ease!

Hivi hakuna Central Command ya UVCCM?...maana kilichopo sasa ni ...Vijana wa Arusha...Vijana wa Pwani...Vijana wa Dar..Vijana wa Tabora..kila upande wakitoa matamko yao , na zaidi kutumika na wenye nia zao!
Umoja wa vijana ccm ni kikundi cha hatari sana kwa sasa kuliko ilivyowahi kuwa katika historia ta Tanzania. Wamekuwa litmus papers wakitumika kupima legibility na illegibility za watu!
Ziko wapi enzi za TANU YOUTH LEAGUE?....Uko wapi Uzalendo?
Je chama cha Mapinduzi na UONGOZI wake wamesafiri kuelekea nchi gani?...Mbona hawarudi?...

The Episode to be continued!......
Mnara wa babeli

kuna usemi wa wahenga "angenda juu kipungu, hafikilii mbinguni"

Vijana wanatia huruma sana...
 
Mwendo huu wa vijana ndani ya CCM utakuja kufumua mengi tusiyotarajia. Watch this space! Makamba atakuja na majibu kwao soon (guessing)

Vikao vya juu vya chama vinakuja end of this week or next week, utasikia KABOOOM!!! tumsubiri Mwenyekigoda ataamuaje!
 
James Millya amekuwa kibaraka wa EL kwa muda mrefu sasa. Alitumwa kwenda kugombea ubunge jimbo la simanjiro ili kumng'oa Ole Sendeka kwani alikuwa mwiba mkali sana kwa mafisadi.

Mpango wao ulishindwa kwenye kura na hata kesi waliombambikia mzee Sendeka ya kutishia kumuua Millya nayo ikashindwa fanikiwa.

Kwakweli inasikitisha sana kuona vijana wanawekwa mifukoni mwa mafisadi kisa wanatanguliza njaa.
 
Inasikitisha sana kuona vijana wa CCM wa arusha hawajui wanachi wa kawaida na hasa vijana priorities zao ni zipi?

  1. Ina maana hawajui arusha kuna shida ya inflation?
  2. Hivi hawawezi kuzungumzia ufisadi na athari za mgao wa umeme?
  3. wameshindwa kutoa tamko la unity wao wanatuambia wanavyofukuzana simply kwasababu mtu kasema ukweli?
  4. Kuna impact gani kwa kijana wa kawaida wa longido na ATCL?
  5. Hivi wameshindwa hata kutathmini arusha kama hub na athari za vurugu za kisiasa na impacts nyingine zitokanazo na vurugu
  6. Wameshindwa hata basi kuonyesha wana upeo na wanapinga ufedhuli?
Tamko lao linaonyesha ni jinsi gani CCM ilivyo out of touch na ordinary wananchi!!! :smash:
 
Mbona iko shallow kama Post za baadhi ya watetezi wa CCM hapa jamvini?

Halafu nilidhani hawa watoto wa vigogo wa CCM wamepelekwa shule nzuri, kumbe hawajaelimika? Kujenga hoja sifuri hata matumizi ya punctuation sifuri!

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kauli ya vijana wa UVCC Arusha imetulia. Sijaona viluilui ndani ya maji machafu kama ile ya Umoja wa vijana wa CCM kitaifa.
Hilo ndilo lilitakiwa kuwa tamko la umoja wa vijana wa ccm kitaifa..

Mkuu, tunatofautiana upeo wa kuchambua hoja ndiyo maana wao wakaandika hivyo walivyoandika kwa maana ya kwamba ndio uwezo wao ulipofika ukomo na wewe ukaona pia kwamba huo ukomo wao ni wa juu kabisa. Fuatilia hapa chini kwa uelewa zaidi.

Tamko hili ni jepesi lisilolingana na matarajio ya viongozi wa mwaka kesho au keshokutwa. Limeandikwa kwa maneno mengi likiwa na maudhui hafiifu.!!

Inasikitisha sana kuona vijana wa CCM wa arusha hawajui wanachi wa kawaida na hasa vijana priorities zao ni zipi?

  1. Ina maana hawajui arusha kuna shida ya inflation?
  2. Hivi hawawezi kuzungumzia ufisadi na athari za mgao wa umeme?
  3. wameshindwa kutoa tamko la unity wao wanatuambia wanavyofukuzana simply kwasababu mtu kasema ukweli?
  4. Kuna impact gani kwa kijana wa kawaida wa longido na ATCL?
  5. Hivi wameshindwa hata kutathmini arusha kama hub na athari za vurugu za kisiasa na impacts nyingine zitokanazo na vurugu
  6. Wameshindwa hata basi kuonyesha wana upeo na wanapinga ufedhuli?
Tamko lao linaonyesha ni jinsi gani CCM ilivyo out of touch na ordinary wananchi!!! :smash:

Niona tamko ndiyo ila sioni lolote zito katika tamko hili ni business as usual.
 
MAAZIMIO YA BARAZA LA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MKOA WA ARUSHA – LONGIDO

Agenda mojawapo ya kikao chetu ilikuwa ni tathmini ya uchaguzi, na kama baraza tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza viongozi wote wa wilaya za mkoa wa Arusha kwa kufanikisha uchaguzi mkuu vizuri sana na kufanikiwa kushinda majimbo ya uchaguzi matano kati ya saba, tunawapongeza sana. Na pia kusimamia kura za Mwenyekiti wetu wa Chama, Jakaya Mrisho Kikwete kushinda vizuri mkoani kwetu Arusha, tukiongozwa na wenyeji wetu wa kikao chetu wa jimbo la Longido ambaye Rais alipata 85% na tukifuatiwa jimbo la Monduli ambapo Rais alipata asilimia 84%, lakini pamoja na kuwapongeza viongozi waliosaidia kufanikisha uchaguzi mkuu, lazima pia kulaani viongozi wa chama waliotumika kukihujumu chama wakati wa uchaguzi na kutusababishia kushindwa vibaya kwenye majimbo mengine na kumpunguzia sana kura Mhe. Rais wetu, na sisi kama vijana tunasema hatutavumilia viongozi wa namna hiyo, na kwa kuonyesha mfano, na kwa kutekeleza maazimio ya baraza kuu la[/SIZE][/FONT] UVCCM lililokaa wiki iliyopita, baraza limeamua kumsimamisha Ndg. Gambo Mrisho kwa kushiriki kukihujumu chama katika jimbo la Arusha mjini na kuendelea kutoa maneno ya kashfa kuhusu Chama na aliyekuwa mgombea wa Chama chetu Jimbo la Arusha Mjini Dr. Batilda Buriani kwenye maeneneo mbalimbali na hata kwenye ofisi ya UVCCM mkoa mbele ya viongozi wengine wengi, hii ni dhambi ambayo haisameheki na kwasababu hiyo, Baraza limeazimia kuwa kijana huyu siyo mwenzetu na tunamuomba Mwenyekiti wa CCM Taifa kulivalia njuga suala hili kwa maeneo mengine ya nchi ili viongozi wote waliokihujumu chama watupishe mapema, twende tukijiandaa na uchaguzi wa 2015 na wanachama ambao tunaamini wapo tayari kufa kwa kutetea imani za Chama Cha Mapinduzi. Tunaamini kama isingekuwa kwasababu ya viongozi wasaliti kama hawa, Mhe Rais Jakaya Mrisho Kikwete angepata ushindi mkubwa zaidi kuliko ushindi alioupata wa asilimia 61% kwenye uchaguzi mkuu 2010

Huyu Gambo Mrisho ndiye aliwataja Lowasa, Rostam na Chenge kama chanzo cha tatizo ndani ya CCM katika mkutano wa UVCCM wa juzi? Kama hiyo ni kweli basi CCM inazidi kuvaa magamba badala ya kuyavua......!

TAFAKARI!
 
Mwendo huu wa vijana ndani ya CCM utakuja kufumua mengi tusiyotarajia. Watch this space! Makamba atakuja na majibu kwao soon (guessing)

Kwa hiyo kila mkoa utatoa tamko lake??? Duh!!! tutakuwa na matamko zaidi ya therasini.... sipati picha, maana mikoa mingine ina kambi mbili mbili ( kama Tabora ).... tutegemee matamko mia hivi.

Kweli CCm haina mwenyewe aisee
 
Inasikitisha sana kuona vijana wa CCM wa arusha hawajui wanachi wa kawaida na hasa vijana priorities zao ni zipi?

  1. Ina maana hawajui arusha kuna shida ya inflation?
  2. Hivi hawawezi kuzungumzia ufisadi na athari za mgao wa umeme?
  3. wameshindwa kutoa tamko la unity wao wanatuambia wanavyofukuzana simply kwasababu mtu kasema ukweli?
  4. Kuna impact gani kwa kijana wa kawaida wa longido na ATCL?[/B]
  5. Hivi wameshindwa hata kutathmini arusha kama hub na athari za vurugu za kisiasa na impacts nyingine zitokanazo na vurugu
  6. Wameshindwa hata basi kuonyesha wana upeo na wanapinga ufedhuli?
Tamko lao linaonyesha ni jinsi gani CCM ilivyo out of touch na ordinary wananchi!!! :smash:

Ukiona hivyo ujue kuna mtu analilia taiming shirika hili... EL
 
Duh!Kwa hiyo babu wa Loliondo nae kawa agenda ya kisiasa??Hamna agenda zingine za maana zaidi ya hiyo??

Ni ajenda.... maana Babu wa Loliondo ni dili la Lowasa, subirini atakaposema ameoteshwa na mungu kuhusu Rais ajeye... fisadi anapotaka Urais, atatumia rasilimali zote na kwa gharama yeyote.
 
Things are falling apart because the arrow of God is No Longer at Ease!

Hivi hakuna Central Command ya UVCCM?...maana kilichopo sasa ni ...Vijana wa Arusha...Vijana wa Pwani...Vijana wa Dar..Vijana wa Tabora..kila upande wakitoa matamko yao , na zaidi kutumika na wenye nia zao!
Umoja wa vijana ccm ni kikundi cha hatari sana kwa sasa kuliko ilivyowahi kuwa katika historia ta Tanzania. Wamekuwa litmus papers wakitumika kupima legibility na illegibility za watu!
Ziko wapi enzi za TANU YOUTH LEAGUE?....Uko wapi Uzalendo?
Je chama cha Mapinduzi na UONGOZI wake wamesafiri kuelekea nchi gani?...Mbona hawarudi?...

The Episode to be continued!......

Hatima ya hivi vi UVCCM vitageuka kama MUNGIKI ya kenya kwani ilianza kidigokidogo kisha vigogo wakaanza kuwatumia kwa maslahi binafsi ikawa out of control yakatokea ya kutokea tuangalie kwa makini
 
Millya ndiye aliyeandika barua kwa aliyekua Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula kabla ya mwaka 2005 akilalamika kutishwa na Lowassa kuwa aache kumsaliti kwani yeye ni ndugu yake na anapaswa kumuunga mkono kama anataka mambo yake yanyooke. Millya alimwambia Mangula kwamba Lowassa alimwambia kwamba ameshakubaliana na Rais Mkapa kwamba JK atakua Rais na yeye (Lowassa) atakua Waziri Mkuu na Millya ataaibika. Lowassa akamsihi ajinge naye na asimsaliti. Mazungumzo hayo yalifanyika nyumbani kwa Lowassa baada ya Millya na viongozi wenzake wa Dodoma, Kilimanjaro, Dar es Salaam na mikoa mingine kutoa matamko kumpinga Kikwete. Baadae ni Millya ambaye amekuja kumbana Lowassa na alionekana kama tishio kuelekea 2010 kabla ya kubwaga manyanga na kumwachia na hatimaye kumuunga mkono Lowassa. Je, Millya ametishwa tena? Na safari hii ameambiwa nani ni Rais na nani PM? Je, Millya hataki kupoteza tena kama alivyompinga JK? Ama 2005 alitumwa na Lowassa kumpinga JK kiana na sasa kazi iliisha na anapaswa sasa kuingia ndani tena?

Jamani kama unaamini kwamba hili tamko ni halali na Lowassa ameonewa, karibu sana utapata majibu humu

Umesomeka mkuu... mwenye macho haambiwi tazama
 
Things are falling apart because the arrow of God is No Longer at Ease!

You have reminded me of the past beautiful stories .. No longer at Ease, The song of Lawino, The song of Okol.

Do you remember "Osokoni tree" ? Never uproot a pumpkin at your homesteaded.

Umofia kwenu?..............
 
Merisho Gambo......huu ni wakati wako wa kuwaonesha kwa vitendo kwamba huko tayari kutembea juu ya maneno yako.......na hauko tayari kuwa mnafiki na kuja kuwa Mchawi uzeeni Watanzania wapo nyuma yako!!
 
Mrisho Gambo......huu ni wakati wako wa kuwaonesha kwa vitendo kwamba huko tayari kutembea juu ya maneno yako.......na hauko tayari kuwa mnafiki na kuja kuwa Mchawi uzeeni Watanzania wapo nyuma yako!!
 
Back
Top Bottom