SoC04 Uuzwaji holela wa vileo unaangamiza nguvu kazi ya taifa kwa kasi, na hii sio Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Saul Mongi

New Member
Jan 30, 2021
1
1
Ili taifa letu la Tanzania lipate maendeleo kwenye nyanja zote lazima likuwe kiuchumi hadi ngazi ya uchumi wa juu.Bidhaa za vileo ni moja ya bidhaa zinazoongoza kwa kukuza pato la taifa kupitia kodi na leseni za biashara na taifa letu linajivunia kwasababu inachangia uchumi wa taifa, lakini kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na uuzwaji holela wa vileo hasa pombe kali bila utaratibu na pasipo kuzingatia rika. Hii imetokana na kupungua kwa ufuatiliaji kutoka kwenye mamlaka za serikali zinazohusika na leseni za uzwaji wa vileo.

Kumekuwa na ongezeko la maduka na vibanda vinavyouza vileo hasa pombe kali ikiwemo kwenye vituo vya mabasi na kwenye makazi ya watu (majumbani), hii imepelekea utumiaji holela wa vileo hasa kwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa.Muda wowote unakuta mtu amelewa na ana kichupa kidogo mfuko,vileo hasa pombe kali zimekuwa zikipimwa hasa kwenye maduka (alimaarufu maduka ya mangi) ndo maana ni rahisi sana kupatikana wakati wowote.

Watumiaji wengi wa vileo hasa rika la chini (vijana) wameshakuwa na urahibu kwasababu ya kunywa bila mpangilio na bila kujali afya. Kiukweli kuna hatari ya kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa miaka 5 hadi 25 ijayo kama tutakuwa na idadi kubwa ya watu waliohathirika na utumiaji wa pombe kali. Ili uchumi ukue ni lazima kuwe na rasilimali watu wenye nguvu na uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.Kwasasa unaweza kuona na kujivunia watu wengi kujiajiri katika sekta hii ya uuzaji wa vileo kwamba wanajipatia kipato na wanakuza pato la taifa bila kuangalia athari zitokanazo na uuzwaji usiofuata taratibu.

Lengo la andiko hili sio kukataza au kushitaki mtu bali ni kuufahamisha uma na mamlaka zinazohusika na vileo pamoja na mambo ya kijamii kuhusu uzaji holela ili kuifikia TANZANIA TUITAKAYO yenye rasilimali watu wenye weledi, hari na mahiri kwenye uzalisha mali. Pengine linachukuliwa kwa urahisi lakini sio jambo la kufumbia macho ilihali madhara yake ni makubwa kwa miaka ijayo. Pia madhara hayawezi kuwa tu kwenye uchumi na rasilimali watu bali pia kwenye maswala ya kijamii kama ongezeko la uhalifu, migogoro ya ndoa na watu wasio na makazi maalumu.

NINI KIFANYIKE KUIFIKIA TANZANIA TUITAKAYO MIAKA 5 HADI 25 IJAYO

1. Lazima mamlaka zipitie leseni za uzaji wa vileo na kutoa leseni kwa wauzaji wa vileo vya jadi maeneo ya vijiji ili kufuatilia mwenendo wa uuzaji wa hivi vileo.Ngazi ya usimamizi lazima ianzie mamlaka za chini yani mjumbe,kijiji/mtaa mpaka ngazi ya taifa. 2.Kuondoa au kusogeza maduka yanayouzwa vileo mbali na makazi ya watu ili kukiokoa kiza kinachokua (watoto) kujihusisha na utumiaji au shughuli za vileo.

3. Muda maalumu wa kuuza vileo lazima uwekwe na kwenye maeneo ambayo tayari muda umeshawekwa basi usimamiwe ili kuruhusu watu wafanye shughuli za uzalishaji mali.

4. Jukumu la kudhibiti swala hili ni la jamii nzima kukemea na kutumia vileo hasa pombe kali kwa usitaarabu,ni vyema pia tukawalinda na watoto wasijiingize kwenye vileo kama kuto watuma kutununualia vileo.

5. Elimu itolewe juu ya madhara ya utumiaji wa pombe kali bila kufuata utaratibu (nidhamu) ili kudhibiti matumizi holela ya vileo na kupunguza au kuzuia matumizi holela ya vileo.

6. Uagizwaji wa vileo kutoka nje ya mipaka ya Tanzania lazima uwekewe utaratibu na ushirikishwaji wa mamlaka ya vipimo (TBS) ishirikishwe kila hatua ili kuzuia vileo visivyofaa au vyenye madhara kwa watumiaji.

7. Mamlaka ya vipimo kwakushirikiana na wizara ya afya ifanye tathimini ya vileo vyote vyenye madhara ya kiafya kwa watumiaji na kuvifungia hasa pombe za jadi.

8. Mamlaka ifuatilie na kukagua mara kwa mara uzalishaji wa vileo kwenye viwanda vilivyo ndani ya nchi.

9. Kabla ya kusajili viwanda vipya vya kutengeneza vileo lazima mamlaka ijihakikishie usalama wa kinywaji husika kwa usalama wa watumiaji.

10. Mamlaka za kisheria lazima ziwajibike kuwachukulia wale wote wanaoenda kinyume na taratibu za uzalishaji,usambazaji na uuzwaji wa vileo.Ikibainika viashiria vya rushwa pia sheria na hatua zichukuliwe ili kuweka mazingira sawa na kufuata utaratibu sahihi.

HITIMISHO
Tanzania tuitakayo lazima iwe na nguvu kazi kwaajili ya kukuza uzalisha mali ili kuchangia pato la taifa na kukuza uchumi kwa maendeleo endelevu.Lazima madhara yatokanayo na utumiaji wa vileo hasa pombe kali na pombe haramu yashughulikiwe kwa kasi na iwe mipango endelevu ili kujenga taifa lenye rasilimali watu wenye nguvu na hari ya maendeleo.

Matumizi yasiyo ya kisaarabu pia yanachochea maradhi ya sukari,maradhi ya figo na yanaongeza umasikini kwa kasi hivyo kutengeneza taifa lenye watu dhaifu kwa asilimia kubwa.Ni vyema watumiaji wakaambiwa vileo ni kiburudisho tu na ni vyema kunywa kistaarabu ili kuzitunza afya za miili yetu.
 
Mimi, ninakubaliana na andiko, kwa kujaribu kupunguza tatizo la ulevi nchini. Ni zuri

Hata hivyo hizo mbinu za kisheria na kimfumo pekee haziwezi kuendesha mtu mmoja mmoja kuachana na ulevi. Hali ikibana sana ulevi utaendelea kupitia magendo.

Tunahitaji mbinu itakayofanya ulevi usiwe kivutio kwao hao vijana/walevi husika na kiotomati tatizo litakuwa limedhibitiwa.

Kwa sababu, mtu asiye na malengo thabiti ndiye hujipoteza/hupotezwa na vilevi. Mwenye malengo anaweza kulewa kama starehe lakini hatapotea mazima abadani.
Screenshot_20240511-182234_Gallery.jpg

Ipo haja ya kurejea falsafa ya kitaifa na sera zitakazowezesha watu wake kuishi kwa matumaini na malengo thabiti.
 
Back
Top Bottom