Kitandu Nkoru

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
878
951
Taarifa hiyo kwamba raia wa Zimbabwe wanauza vidole vyao vya miguuni ili kukabiliana na umasikini imesambaa sana nchini Nigeria.

Mwanablogu mmoja wa Zimbabwe amedai kwamba biashara hiyo inafanyika katika kituo kimoja cha maduka katika mji mkuu Harare. Inanukuua ujumbe wa WhatsApp ukiwa na takwimu za hadi $40,000

Lakini waandishi wanasema kiwango cha fedha kinachotumika ni $40,000 kwa kidole gumba , $25,000 kwa kidole cha katikati na $10,000 kwa kidole kidogo.

(£31,800) zinazotolewa na watabibu wa kitamaduni. Wakijulikana kama waganga bandia wanaoshirikishwa na uchawi - hushtumiwa na waganga wa kienyeji wanaoheshimika kwa jina 'sangoma' kusini mwa bara Afrika.

Utani wa vidole umesambaa kote nchini Zimbabwe , vikichapishwa na alama ya reli #Chigunwe, ikimaanisha Vidole vya mguuni katika lugha ya Shona , na hivyobasi kuzua ucheshi wakati ambalo hali ya kiuchumi imekuwa ngumu.

Lakini hakuna hata gazeti moja la Zimbabwe lililochukua habari hiyo na baadhi ya watumiaji wa mtandao wa twitter wamelalamika kwamba utani huo unazuia masuala muhimu yanayowakabili raia katika taifa hilo kuangaziwa.

Mwanablogu kwa jina Gambakwe alichapisha mnamo tarehe 28 mwezi Mei kwamba biashara ya kuuza vidole inaendelea katika duka kuu la Ximex Mall.

Siku chache baada ya chapisho la mwanablogu huyo, gazeti la burudani la H Metro lilichapisha mahojiano na wafanyabiashara wa soko haramu katika duka hilo ambao walisema kwamba , suala lote lilisambazwa kupitia kiasi baada ya baadhi yao kulisambaza kama utani.

Lakini tangu wakati huo, wanasema kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakielekea katika duka hilo la Ximex kuulizia kuhusu biashara hiyo kufuatia uvumi huo.

Watumiaji wa mtandao wa twitter kutoka mataifa kadhaa ya Afrika, ikiwemo Nigeria na Uganda, walianza kuchapisha kwamba raia wa Zimbabwe wamewaza kuuza vidole vyao vya mguuni kwa maelfu ya madola.

Kituo kimoja cha redio nchini Kenya pia kilichapisha ujumbe wa twitter , kikidai zilikuwa habari ambazo hazijathibitishwa, wakiwauliza mashabiki wao ni kiungo gani cha mwili wangelipenda kuuza.

Source: BBC
 
$40,000 kwa gumba moja la mguuni tu,nikiwapa magumba yote mawili nakula $80,000,ulizia hawachukui na gumba za mikononi mkuu?na ofisi zao zipo hapohapo mjini?

Wakuu nauli kutoka Mbezi hadi Harare bei gani,nataka kukopa nauli ya kwenda tu wakati wa kurudi nitarudi na RR yangu.
 
Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Pesa nyingi sana hiyo, n Kama Mil. 131 per 1 toe
 
$40,000 kwa gumba moja la mguuni tu,nikiwapa magumba yote mawili nakula $80,000,ulizia hawachukui na gumba za mikononi mkuu?na ofisi zao zipo hapohapo mjini?

Wakuu nauli kutoka Mbezi hadi Harare bei gani,nataka kukopa nauli ya kwenda tu wakati wa kurudi nitarudi na RR yangu.

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Hamna Hamna utakuwa uko karibu na salary ya Zamani ya Sedio Mane
 
Wengi tumewahi kusikia kuhusu stories kwamba katika baadhi ya Nchi za Ulaya na Asia kwamba figo ni deal, vijana wanauza Figo na kutajirika
Lakini Huko Zimbabwe, vijana wanauza vidole vya Miguu ambapo kidole kimoja kikubwa (kidole gumba) kinafika mpaka USD 40,000, hii nimeona huko Twitter zaidi ya videos tatu vijana wa Zimbabwe wanakatwa vidole na kukabidhiwa gari ama pesa
Nimeshindwa kudownload videos kutokana Twitter hivo naweka screenshot
 
Attachments

  • Screenshot_20220601-155519.png
    Screenshot_20220601-155519.png
    263.2 KB · Views: 76
  • Screenshot_20220601-155528.png
    Screenshot_20220601-155528.png
    229.3 KB · Views: 67
  • IMG_20220602_165035.jpg
    IMG_20220602_165035.jpg
    52.3 KB · Views: 67
Back
Top Bottom