Mkuu kuna siku za mwanzo wakati kila nikiwaona kina wiz khalifa na snoop Dogg wanavyosifia mmea na Mimi nikashawishika kununua.
Nikanunua, nikatoa mbegu na vijiti yale majani nikayasaga kiganjani kama navyoonaga wengine wanavyofanya, kwavile nlikuwa siwezi kuweka kwenye rizla nlichofanya nilinunua sigara nikatoa tumbaku yote alafu ndio nikaingiza bangi humo.
Nikaenda shambani kuivuta, ghafla nikasikia "PAAAA!!!!!" Kama kitu kimepasuka kwenye bangi, ule moshi wake uliumiza koo langu, basi nikaahirisha zoezi nikarudi geto.
Basi geto nmefika nikajilaza kitandani, bwana bwana wee, damu nahisi ikaanza kupita kwa spidi sana kwenye mishipa ya machoni, nilihisi kabisa Leo macho yangu yanapasuka na ntakua kipofu.
Nikanawa nawa na maji angalau kwa mbali ile hali ikapungua kwa mbali ila hali hii ilidumu kwa mwaka unakuta kila wiki lazima kuna siku nahisi damu inapita kwa kasi machoni hasa nikiwa nimeingia kitandani basi nakesha hadi saa nane ndio macho yanatulia.
Sina hamu tena na bange, Je hii ilisababishwa na nini mtaalam