Uuzaji Bange ulivyonibadilisha tabia

Latrice

JF-Expert Member
Jan 30, 2020
2,089
2,000
Historia yangu ni ndefu kidogo ila nitaifupisha

Mwaka fulani baada ya vurugu za hapa na pale Geita Secondary, Butimba Day na Mwanza Sec nilitimuliwa, nikahamia Manguanjuki (Lake) iliyoko Singida kuanza kidato cha tatu.

Pale nilikuwa huru sana, nikawa na tumia hela hovyo hovyo bahati mbaya sana wazazi wangu wakagundua na kunikacha kuwa nijitegemee mwenyewe si nimeshakua na hii ndio ikawa safari yangu rasmi ya kuuza Bange niliwahi kuuza hapo awali ila kwa uchache sana.

Kuna Bro mmoja stand ya zamani ya Singida alikuwa mwanangu sana tulifahamiana kwa sababu ya uchezaji wangu wa pooltable nikishika fimbo hutoki, nikanunua mzigo wa elfu 10 kwake kama kianzio nilivyouza nikapata elfu 30 kama faida nikaona maisha si ndio haya sasa, nikanunua tena wa 20K nikapata elfu 60.

Nilikuwa nikiuza sehemu yoyote yenye pool table nikimaliza mzigo narudi shule chap. Siku moja yule bro nikamsikia anaagiza nikamvizia nikaiba ile namba nikawasiliana na yule jamaa akakataa kabisa hafanyi hiyo biashara ikabidi nimshirikishe tu bro ndo nikapata mzigo wangu wa kwanza pis moja ilikuwa 100 mimi nauza 1000.

Nilipata mzigo wa kwanza kwa elfu 50 na nikapata faida mara mbili nikaagiza tena nikapata laki tatu, nyakati fulani nikiwa likizo Mwanza mama akaniuliza "Mbona huombi hela siku hizi mwenzetu" nikajibu "Huna hela ya kunipa mimi" tulikuwa tunaishi kotaz za Magereza, Butimba. Nikawa najiamini kupitiliza nikaanza kulima mwenyewe Kishiri nikawa maarufu kwa muda mfupi sana nikaacha kuuzia raia maana nilianza kuchomewa nikawa nauza kwa mapoti tu.

Nilivyorudi tena Singida ndio nikawa moto wa gesi hadi vijijini nikawa naenda, kuna kijiji kinaitwa Kinampanda kuna chuo cha Ualimu pale nikaanza kuuza siku moja ambayo nilivunja sheria yetu ni kumuuzia dogo mmoja huko Kinampanda ambaye si mwanafunzi akakamatwa kwa wizi wa kuku, lahaula! akakutwa na bange pia! Wakambana aseme alikoitoa dogo akanitaja nikaanza kuliwa timing na serikali ya kijiji.

Kuna siku nikaenda tena mapis yangu yalikuwa marefu naweka kwenye soksi, najaza mfukoni na kwenye begi nikauza chap chap nikapata laki na nusu ghafla tu begi likabaki tupu nikabakisha za mifukoni kuna wadada wawili wakanifuata na kuniambia unaitwa pale dukani, kufika pale nikaambiwa "ingia mwenyewe" nilikuwa mbabe sana nikaingia kwa matambo nikaiona ile bange yangu iko mezani nilistuka nikakalia pipa lenye maji nikamwaga zote moja tu ikadondoka chini nikaulizwa "hiyo ya nani?" Nikajibu "Yangu" tukapelekwa Polisi nikawa najiamini sana si mtoto wa soldier bana nikaambiwa leta namba ya ndugu yako nikatoa ya bro hakupatikana ikabidi nitoe ya mzee lahaula mzee akasema "fungeni huyo" nilichanganyikiwa ila nikajikaza kiume.

Kesho yake tukawa tunapelekwa Singida mjini na yule dogo kufika center ya kile kijiji tukakutana na Mwinjilisti wa kike wa Singida mjini ambaye mwanae wa kike aliwahi kunitambulisha kwake, alihuzunika sana akawasihi wale maaskari tukae kidogo akajadiliana nao kama masaa matatu wakiwa na watendaji wa kijiji baadae tukafunguliwa pingu na kuambiwa niondoke na nisiwahi kurudi hicho Kijiji tena.

Sikukoma yakanikuta makubwa nilipofuata mzigo tena Oldonyo Sambu.


Kipande cha Mwisho.

Baada ya kurudi shule yule Mwinjilisti alikuwa anakuja kunitembelea kila weekend ananipigisha maombi hata nusu saa nzima. Kuna siku alifanya kosa akanipa elfu 20 badala ya elfu 5 aliyozoea, alikuwa akifanya hivi baada ya kugundua wazazi wamenitupa kiaina kutokana na tabia zangu ila kilichomvutia zaidi ni kufanya kwangu vizuri darasani akaamini ipo siku Mungu atanibadilisha.

Katikati ya wiki nilienda Arusha kijiji cha Oldonyo Sambu, nikakutana na washikaji ninaofahamiana nao (sikuwa na urafiki na watu naolingana nao umri) wakanipeleka kwenye bei rahisi zaidi.

Donyo kuna mapori na mmoja wa wale jamaa alikuwa anaendesha lori la kubeba miti humohumo wanatia DIME. (Dime ni Kilo ya bange) baada ya kupata mzigo nikaondoka, ulipoisha nikafata tena. Nilikuwa navaa uniform naporudi Singida ili nisiwe suspected kwa chochote vilevile sikuwa na hofu kabisa.

Wale jamaa wakaona dogo anatupiga gape hivihivi tunaona haiwezekani wakaanza kuleta na wao nilivyoona vile nikaanza kuvuka border sasa.
Napoandika border sio nje ya nchi ni nje ya mkoa nikaanza kuuza Igunga, Nzega na Haydom.
Hili lilikuwa kosa kubwa sana nililowahi kufanya maana nikawa nawauzia watu na maeneo nisioyajua vizuri, muuza bange au madawa yoyote hauzi eneo ambalo halijui ni anamuuzia retailer wa hilo eneo ambaye anawafahamu watu wake.

Nikawa naenda Nzega, pale milori inapaki sana na pooltables ni nyingi nahakikisha sirudi na pis hata moja na ilikuwa hivyo siku zote.

Siku moja niko Nzega nauza usiku kwenye pooltables kumbe sungusungu ndio wameshika kasi, wakati narudi lodge nikadakwa kwanini nazurura alafu peke yangu wakanipeleka ofisini kwao nikalala fresh tu juu ya matofali lile jengo lilikuwa halijakamilika.
Asubuhi majamaa yakanipiga search yakakuta pisi tano mfukoni na laki moja hayakunilazia damu yaliniosha fimbo mbaya alafu yakanipeleka kituoni.

Shukrani sana kwa mzee wangu sikulala hata cello na sikuwahi kurudi Singida tena mpaka baada ya miaka mitatu na nusu.

Hii ni story ya kweli ya maisha yangu.
 

Latrice

JF-Expert Member
Jan 30, 2020
2,089
2,000
Ulifahamiana na wazee wa kituo ndo utapiga hela wao wanakuacha we unawatoa kila mda ,kuna jamaa mmoja alikamatwa mara kibao akajua jinsi ya kula na wao,sometimes wanatukuta tunamonka wanatuacha tu.
Nilikuwa mdogo mkuu ningefahamiana na nani au nani angenisikiliza?

"Akili kubwa, kamwili kembamba ila mi ni mwamba"
Jose Mtambo Kigamboni finest
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom