Uuzaji Bange ulivyonibadilisha tabia

Historia yangu ni ndefu kidogo ila nitaifupisha

Mwaka fulani baada ya vurugu za hapa na pale Geita Secondary, Butimba Day na Mwanza Sec nilitimuliwa, nikahamia Manguanjuki (Lake) iliyoko Singida kuanza kidato cha tatu.

Pale nilikuwa huru sana, nikawa na tumia hela hovyo hovyo bahati mbaya sana wazazi wangu wakagundua na kunikacha kuwa nijitegemee mwenyewe si nimeshakua na hii ndio ikawa safari yangu rasmi ya kuuza Bange niliwahi kuuza hapo awali ila kwa uchache sana.

Kuna Bro mmoja stand ya zamani ya Singida alikuwa mwanangu sana tulifahamiana kwa sababu ya uchezaji wangu wa pooltable nikishika fimbo hutoki, nikanunua mzigo wa elfu 10 kwake kama kianzio nilivyouza nikapata elfu 30 kama faida nikaona maisha si ndio haya sasa, nikanunua tena wa 20K nikapata elfu 60.

Nilikuwa nikiuza sehemu yoyote yenye pool table nikimaliza mzigo narudi shule chap. Siku moja yule bro nikamsikia anaagiza nikamvizia nikaiba ile namba nikawasiliana na yule jamaa akakataa kabisa hafanyi hiyo biashara ikabidi nimshirikishe tu bro ndo nikapata mzigo wangu wa kwanza pis moja ilikuwa 100 mimi nauza 1000.

Nilipata mzigo wa kwanza kwa elfu 50 na nikapata faida mara mbili nikaagiza tena nikapata laki tatu, nyakati fulani nikiwa likizo Mwanza mama akaniuliza "Mbona huombi hela siku hizi mwenzetu" nikajibu "Huna hela ya kunipa mimi" tulikuwa tunaishi kotaz za Magereza, Butimba. Nikawa najiamini kupitiliza nikaanza kulima mwenyewe Kishiri nikawa maarufu kwa muda mfupi sana nikaacha kuuzia raia maana nilianza kuchomewa nikawa nauza kwa mapoti tu.

Nilivyorudi tena Singida ndio nikawa moto wa gesi hadi vijijini nikawa naenda, kuna kijiji kinaitwa Kinampanda kuna chuo cha Ualimu pale nikaanza kuuza siku moja ambayo nilivunja sheria yetu ni kumuuzia dogo mmoja huko Kinampanda ambaye si mwanafunzi akakamatwa kwa wizi wa kuku, lahaula! akakutwa na bange pia! Wakambana aseme alikoitoa dogo akanitaja nikaanza kuliwa timing na serikali ya kijiji.

Kuna siku nikaenda tena mapis yangu yalikuwa marefu naweka kwenye soksi, najaza mfukoni na kwenye begi nikauza chap chap nikapata laki na nusu ghafla tu begi likabaki tupu nikabakisha za mifukoni kuna wadada wawili wakanifuata na kuniambia unaitwa pale dukani, kufika pale nikaambiwa "ingia mwenyewe" nilikuwa mbabe sana nikaingia kwa matambo nikaiona ile bange yangu iko mezani nilistuka nikakalia pipa lenye maji nikamwaga zote moja tu ikadondoka chini nikaulizwa "hiyo ya nani?" Nikajibu "Yangu" tukapelekwa Polisi nikawa najiamini sana si mtoto wa soldier bana nikaambiwa leta namba ya ndugu yako nikatoa ya bro hakupatikana ikabidi nitoe ya mzee lahaula mzee akasema "fungeni huyo" nilichanganyikiwa ila nikajikaza kiume.

Kesho yake tukawa tunapelekwa Singida mjini na yule dogo kufika center ya kile kijiji tukakutana na Mwinjilisti wa kike wa Singida mjini ambaye mwanae wa kike aliwahi kunitambulisha kwake, alihuzunika sana akawasihi wale maaskari tukae kidogo akajadiliana nao kama masaa matatu wakiwa na watendaji wa kijiji baadae tukafunguliwa pingu na kuambiwa niondoke na nisiwahi kurudi hicho Kijiji tena.

Sikukoma yakanikuta makubwa nilipofuata mzigo tena Oldonyo Sambu.


Kipande cha Mwisho.

Baada ya kurudi shule yule Mwinjilisti alikuwa anakuja kunitembelea kila weekend ananipigisha maombi hata nusu saa nzima. Kuna siku alifanya kosa akanipa elfu 20 badala ya elfu 5 aliyozoea, alikuwa akifanya hivi baada ya kugundua wazazi wamenitupa kiaina kutokana na tabia zangu ila kilichomvutia zaidi ni kufanya kwangu vizuri darasani akaamini ipo siku Mungu atanibadilisha.

Katikati ya wiki nilienda Arusha kijiji cha Oldonyo Sambu, nikakutana na washikaji ninaofahamiana nao (sikuwa na urafiki na watu naolingana nao umri) wakanipeleka kwenye bei rahisi zaidi.

Donyo kuna mapori na mmoja wa wale jamaa alikuwa anaendesha lori la kubeba miti humohumo wanatia DIME. (Dime ni Kilo ya bange) baada ya kupata mzigo nikaondoka, ulipoisha nikafata tena. Nilikuwa navaa uniform naporudi Singida ili nisiwe suspected kwa chochote vilevile sikuwa na hofu kabisa.

Wale jamaa wakaona dogo anatupiga gape hivihivi tunaona haiwezekani wakaanza kuleta na wao nilivyoona vile nikaanza kuvuka border sasa.
Napoandika border sio nje ya nchi ni nje ya mkoa nikaanza kuuza Igunga, Nzega na Haydom.
Hili lilikuwa kosa kubwa sana nililowahi kufanya maana nikawa nawauzia watu na maeneo nisioyajua vizuri, muuza bange au madawa yoyote hauzi eneo ambalo halijui ni anamuuzia retailer wa hilo eneo ambaye anawafahamu watu wake.

Nikawa naenda Nzega, pale milori inapaki sana na pooltables ni nyingi nahakikisha sirudi na pis hata moja na ilikuwa hivyo siku zote.

Siku moja niko Nzega nauza usiku kwenye pooltables kumbe sungusungu ndio wameshika kasi, wakati narudi lodge nikadakwa kwanini nazurura alafu peke yangu wakanipeleka ofisini kwao nikalala fresh tu juu ya matofali lile jengo lilikuwa halijakamilika.
Asubuhi majamaa yakanipiga search yakakuta pisi tano mfukoni na laki moja hayakunilazia damu yaliniosha fimbo mbaya alafu yakanipeleka kituoni.

Shukrani sana kwa mzee wangu sikulala hata cello na sikuwahi kurudi Singida tena mpaka baada ya miaka mitatu na nusu.

Hii ni story ya kweli ya maisha yangu.
Day mtoto wa butimba mwanza ?
 
Tulishawahi kumuibia pusha gunia limejaa bangi alikuaga mkuda knoma hata siku huna hela hakupi hata kushabu...tukapanga mchongo mi mwanangu tukapeleleza tukajua anapoficha tukapita nao wote..tukachinja tukafunga kete tukaanza kuuza tulipiga kama 450k hapo hatukufunga wote...yule pusha alitamani kujinyonga alpokuja kujua ni sisi tunamjbu tu tupeleke polisi hakua na uwezo wa kutufanya chochote maana sisi ndo wazawa
 
Tulishawahi kumuibia pusha gunia limejaa bangi alikuaga mkuda knoma hata siku huna hela hakupi hata kushabu...tukapanga mchongo mi mwanangu tukapeleleza tukajua anapoficha tukapita nao wote..tukachinja tukafunga kete tukaanza kuuza tulipiga kama 450k hapo hatukufunga wote...yule pusha alitamani kujinyonga alpokuja kujua ni sisi tunamjbu tu tupeleke polisi hakua na uwezo wa kutufanya chochote maana sisi ndo wazawa
Daadeki mwingine angewafanya sivyo ndivyo.

Mlikuwa mnauzaje kitaani?
 
Njaa mbaya sana Kuna siku njaa ilinibana Kuna washkaji wakanikuta sehem na kausafiri wangu uchwara wakaniambia tubebee mzigo wetu hadi Dar. Nilitetemeka
sana nilipokuja gundua ni mzigo wa wa bange. Lakini nilikuja kugundua
kumbe jamaa wanatembea kwa nguvu za Giza maana walinishindia mzigo hadi siti

ilibaki moja tu ya mbele ya dereva na abiria wakapulizia perfume Kisha mbele ya gari kilifungwa kitambaa kidogo chenye dawa , Basi nikahakikishiwa Hadi nafika Dar hakuna atakaeipiga mkono, kweli bwana nikifika napita barrier hakuna wa kuniuliza mpaka naingia Dar salama. Niliposhusha tu nikasema mungu wangu sitarudia tena lakini nililipwa pesa ndefu.
 
DeWitt J tulikua tunauza jero mchana alf ikifka usiku ni buku sana sana madereva wa malori ndo walikua wanachukua stick nyingi...alf si tulikua hatuvuti huo tuliouiba si unajua unaweza kua chizi bure maana tuliemuibia alkua mtu wa kwa sangoma sana
Mlipofeli ni kuacha kuvuta mngekuwa na ideas nyingi za biashara mngevuta.

Mimi nilikuwa silali hata siku mbili kabisa nashinda viwanja vya mpira siku za weekend na enzi hizo mirungi imeshika kasi sana nilikuwa sikosi.

Kuuza kiwanja cha mpira na pooltables ni rahisi zaidi maana kote nilikuwa nafahamiana na watu na ni mtu mbaya wa hiyo michezo. Hadi nikaitwa Kete
 
Kwa uzoefu wako bange ya wapi ambayo wateja wenyewe walikua wanasema enheee mzigo ndiwo!
 
Njaa mbaya sana Kuna siku njaa ilinibana Kuna washkaji wakanikuta sehem na kausafiri wangu uchwara wakaniambia tubebee mzigo wetu hadi Dar. Nilitetemeka
sana nilipokuja gundua ni mzigo wa wa bange. Lakini nilikuja kugundua
kumbe jamaa wanatembea kwa nguvu za Giza maana walinishindia mzigo hadi siti

ilibaki moja tu ya mbele ya dereva na abiria wakapulizia perfume Kisha mbele ya gari kilifungwa kitambaa kidogo chenye dawa , Basi nikahakikishiwa Hadi nafika Dar hakuna atakaeipiga mkono, kweli bwana nikifika napita barrier hakuna wa kuniuliza mpaka naingia Dar salama. Niliposhusha tu nikasema mungu wangu sitarudia tena lakini nililipwa pesa ndefu.
Waganga wanasaidia sometimes inakuwa hata si uganga ni kujiamini tu ambako amekupa mganga ndio kunakokufanya ufanikiwe.

Kuna mganga alikuwepo Manyoni (sijui kama bado yupo) yeye anakufukia kwenye kichuguu kilichopo kwenye mikaratusi hadi kiunoni usiku kama dakika kumi tu anafanya mambo yake ukitoka hapo hakuna anayekuteteresha.
 
@DeWittj kuvuta tulikua tunavuta sana tu ila sio mzigo tuloiba tuliogopa anaweza akatia laana siku tunavuta unatoka na road...tulikua tunauza hadi stand ilikua vigumu kugundua maana tulikua mabishoo haswaa
Uwe bishoo, handsome na unaweza vitu fulani fulani vya kijamii hata hustukiwi.
 
Hii stori itaendelea kama nyingine za urongo au ndio urongo umekatika.......
 
Back
Top Bottom