Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,036
2008-03-07 16:27:01
Na Valery Kiyungu, Kunduchi
Shule ya Msingi Ununio iliyoko katika Kata ya Kunduchi Jijini imepokea msaada wa madawati mapya 148 yaliyo na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 264.
Msaada huo uliotolewa na Bw.Peter Jensen, unalenga kupunguza tatizo la uhaba wa madawati hali inayowafanya wanafunzi wengine kukaa chini.
Akipokea msaada huo Bw. Carin Ungele kwa niaba ya Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, amesema msaada huo utapunguza tatizo la upungufu wa madawati shuleni hapo.
``Manispaa ya Kinondoni imefarijika na misaada ya mara kwa mara ambayo hutolewa na Bw. Jensen hususan katika shule hii ya Ununio,`` akasema Bw. Ungele.
Kwa upande wake, Bw. Jensen amesema aliguswa na tatizo hilo na hivyo kuamua kuwapunguzia kero ya muda mrefu wanafunzi hao.
Aidha ameahidi kuendelea kutoa msaada wa samani shuleni hapo utakaowalenga walimu na wanafunzi ili kuboresha kiwango cha elimu.
``Nitaendelea kuisaidia shule hii kwa kuendelea kutoa misaada mingine zaidi ili kuboresha kiwango cha elimu shuleni hapo,`` akasema Bw. Jensen.
Akizungumza na Alasiri muda mfupi baadae Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Rubega Rubega amesema kabla ya kupewa msaada huo idadi kubwa ya wanafunzi walikuwa wakikaa chini.
Hii ni mara ya tatu kwa Bwana Jensen kusaidia shule hiyo ya Ununio yenye wanafunzi 737, ambapo katika mwaka 2003, alitoa msaada wa madawati 20, yenyeb uwezo wa kukaliwa na wanafunzi 100, meza 13, kwa ajili ya walimu, na viti 15, pia kwa matumizi ya walimu wa shule hiyo.