Utumwa mpya ndani ya Kanisa

Utumwa mpya ndani ya Kanisa

Nakubaliana asilimia 100 na hii mada yake Kitena. Big up sana mtoa mada !!!!!

Kama wewe unajiita ni Mkristo, jambo la kwanza unalotakiwa kufanya ni kuwa unasoma Biblia. Uisome yote uimalize, na utafakari kila ulichosoma. Ukiwa unafanya hivyo, matapeli kama hao manabii na mitume feki hawawezi kuchukua pesa zako. Kuna mistari mingi kwenye Biblia inayoeleza wazi kwamba hicho kinachofanywa na hao mitume na manabii kwa kusema watu watabarikiwa na kupona kwa kutoa pesa nyingi na kuuza mafuta, maji n.k. ni utapeli mtupu. Tuangalie mifano michache tu.

a) Kuna yule mama mjane aliyetoa sadaka senti mbili ambazo ndizo peke yake alizokuwa nazo. Yesu akasema ametoa KULIKO WENGINE WOTE. (Lk 21:2-4). Kwa maneno mengine, Mungu hambariki mtu kwa sababu ametoa pesa nyingi kama sadaka, bali anaangalia moyo wake wa kujitoa.

b) YESU ALIWAKATAZA KABISA WAFUASI WAKE WASITOZE FEDHA ILI KUOMBEA WATU UPONYAJI AU KUWATOA MAPEPO.
Yesu aliwaambia wafuasi wake:- Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; MMEPATA BURE TOENI BURE (Mt 10:8). Kwa maana hiyo, ukiona mtumishi yeyote anayewaambia watu watoe pesa nyingi ili wapate miujizi NI MTAPELI

c) Ni Yesu mwenyewe ambaye anaponya watu kwa kutumia NENO LAKE. Yesu akitamka uponyaji juu ya mgonjwa, au akitamka maiti afufuke, muujiza huo unatokea. Mtumishi wa Mungu aliyeokoka na yuko vizuri kiroho anakuwa na Yesu ndani yake. Kwa hivyo, anapoombea watu, YULE YESU ALIYE NDANI YA HUYO MTUMISHI NDIYE ANAYEPONYA . Kwenye Kitabu cha 2 Wakorintho tunasoma pale Mtume Paulo alipoandika:- "....mnatafuta dalili ya Kristo, asemaye ndani yangu......"(2 Kor 13:3). Na kwenye Kitabu cha Wagalatia tunasoma:- wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; (Gal 2:20)
Maana ya hii mistari ni wazi kwamba anayefanya uponyaji wa kweli, ni Yesu ANAYEISHI NDANI YA MTUMISHI WAKE. Kwa sababu hiyo, KINACHOSABABISHA UPONYAJI SIO SADAKA ILIYOTOLEWA au mafuta, maji , chumvi n.k.bali ni IMANI ya mtu aliyonayo kwamba Yesu aliye ndani ya huyo mtumishi ndio atamfanya huyo mtu apone. Mara nyingi sana, Yesu alipowaponya watu aliwaambia IMANI YAKO IMEKUPONYA (Soma Mt 9:22, Mk 5:34, Mk 10:52, Lk 8:48 n.k.)

Zaidi ya haya maelezo hapa juu, yapo mambo mengine ambayo ni lazima wewe Mkristo uyaelewe.

1. Wewe unayeenda kuombewa ili utajirike, upone, upate mwenza wa ndoa n.k. utambue kwamba Yesu hakuwa anafanya tu miujiza watu wakapona, na wengine wakafufuka, na wengine wakatolewe mapepo ili kufurihisha watu waliokuwa wanamfuata kama vile alikuwa mcheza sarakasi. Alikuwa anafanya hiyo miujiza ili watu waelewe kwamba Yeye ndiye yule Kristo aliyekuwa ametabiriwa na manabii mbalimbali tangu zamani na kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu mwenye uwezo wa ki-Mungu. Hao mitume na manabii wanaoponya watu kwa kutumia mafuta, maji n.k. WANAWAFANYA WATU WAAMINI HIVYO VITU BADALA YA KUMWAMINI YESU. Ni dhambi mbaya sana !!! Ni kuendekeza ibada ya sanamu (kuabudu vitu - yaani kuamini kwamba mafuta na maji n.k. ndio yanaponya badala ya kuamini kwamba Yesu aliye Mungu ndiye anayeponya).

2. Zamani za Yesu mafuta ya mizeituni yalikuwepo, chumvi ilikuwepo, na maji yalikuwepo. Mbona Yesu hakuvitumia kumponya mtu yeyote?
Ukimwona mtume au nabii au mtumishi yeyote yule anayetumia hivyo vitu "kuponya", au mtu anayemwamini mtumishi kama huyo muulize swali hili hili:- Je, mbona hakuna mahali popote pale kwenye Biblia tunaposoma kwamba Yesu aliponya watu kwa kutumia mafuta, au chumvi au maji n.k.?

Biblia iko wazi kabisa. Mungu mwenyewe amesema:- WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA (Hosea 4:6 (a)

Kama wewe unayesoma post hii ni Mkristo, nakuomba sana tafadhali soma mistari yote ya Biblia niliyoandika ili ujue ukweli ni upi. Usije kuangamizwa kwa kukosa maarifa. Mungu akubariki.
 
Ukishaelewa Mungu hayupo, na habari za kuwepo kwake ni hadithi za watu tu, haya mengine hayawezi kukusumbua sana.
Wewe na wenzako ambao deeply inside mnaamini kwa dhati uwepo wa Mungu, lakini kwakuwa hamna utayari wa kumkubali kwa maneno hasa mbele ya watu,,,,,,,,mkiwa kwenye ndege turbulence ikatokea ndiyo wa kwanza kusema Oooh my God,, hamtulii nature ifanye kazi yake, mnakuwa wa kwanza kumkiri Mwenyezi
 
Mtu huna kazi, huna biashara wala wazo la biashara, huna ujuzi, huna elimu, lakini kila siku unashinda kanisani kumsikiliza Mchungaji anayesema kesho utakua milionea na wewe unasema "Baba napokea/Dady I receive".

 
Kwani wewe ume "claim" nini hapo juu na mimi nikakujibu vipi?

Unajifanya hujaelewa?
Hujaeleza unataka ushahidi gani.

Naweza kukwambia kutaka kwako ushahidi ni ushahidi kwamba Mungu hayupo.

Angekuwepo kila mtu angemjua yupo na kusingekuwa na mtu anayetaka kupewa ushahidi kwa mwengine kwamba Mungu hayupo.
 
UK I on a MTU anaongea Kama we wewe lazima no China MBA ya aliyekuambia sad aka lazima nani😤😤😟
Ndio maana mimi niliamua kuacha kwenda kanisani kwa ajili ya mambo kama. Haya niliona sisi washirika ndo mitaji ya wachungaji mitume na manabii.. Kanisa ni mimi mwenyewe hekalu ni roho yangu na. Mwili wangu baaada ya Yesu kunifia msalabani aliondoa kiambaza au ukuta uliokuwepo umezuia Mawasiliano yangu na Mungu ila now najiachia mimi mwenyewe kwa Mungu wangu alieniumba moja kwa moja na ananisikia vizuri sio kuibiwa na kutapeliwa na hawa wahuni wajanja wanajiitwa watumishi wa Mungu.
 
Hujaeleza unataka ushahidi gani.

Naweza kukwambia kutaka kwako ushahidi ni ushahidi kwamba Mungu hayupo.

Angekuwepo kila mtu angemjua yupo na kusingekuwa na mtu anayetaka kupewa ushahidi kwa mwengine kwamba Mungu hayupo.
Unashindwa kuthibitisha kauli yako.

Mpaka sasa mbili bila. Kila post utayoleta bila ushahidi ujuwe ni bao.
 
Makanisa yaliojawa na shuhuda. Huwa sielewi nini maana ya zile shuhuda. Mtu anatolewa pepo anawekewa mic ili wasikie pepo linaongea. Siku nzima unashinda kanisani, huna kazi za kufanya. Upumbavu sana.

Hahahahaa! Kazi wanakuwa nayo, ni kusema haleluyah, ameen!
 
Tatu bila.

Kumbe unaongea kitu huna ushahidi nacho.

Pole sana.
Wewe umeshindwa kutaja hata ushahidi unaotaka ukoje.

Umeshindwa kuuliza swali, halafu unasema sijajibu.

Mimi naweza kukwambia nipe ushahidi ulio logically consistent kwamba Mungu yupo.

Very specific request.

Toa uahshidi.
 
Mkuu nimekuelewa mno umeeleza kwa logic na bila kua na mihemko kifupi hili swala la miujiza limekua ni tatizo kuanzia ngazi ya familia hadi jamii kwa ujumla pale Iringa kuna kanisa linaitwa Overcomers mahubiri yake kwa kiasi kikubwa ni kuhusu hizo mambo sijui mafuta mara sijui muujiza gani ukisikiliza kama tu una akili timamu unaona wazi ni utapeli lakini kama unavyosema roho za uvivu zinapelekea kuona kua ndio kimbilio
 
Back
Top Bottom