Utumwa mpya ndani ya Kanisa

Kitena

Kitena

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Messages
332
Points
250
Kitena

Kitena

JF-Expert Member
Joined May 28, 2012
332 250
Nimeituma kama nami livyoikuta namani itawagusa wengi an ndio hali halisi iliyipi kwa sasa.

UTUMWA MPYA NDANI YA KANISA

Pale udadisi unapokwenda likizo (reasoning)
Ndani ya Kanisani,watu kwa kukosa maarifa wanaibiwa. Kwa bahati mbaya hatujifunzi kutoka kwa Wabeloya, hawa walikuwa wadadisi.

Watu wa huko walikuwa wasikivu zaidi kuliko wale wa Thesalonike. Waliupokea ule ujumbe kwa hamu kubwa, wakawa wanayachunguza Maandiko Matakatifu kila siku, ili kuona kama yale waliyosema Paulo na Sila yalikuwa kweli.

Watu Wanaibiwa kwa kupitia magonjwa yao , wanaibiwa kwa kupitia umaskini wao, wanaibiwa kwa kupitia kukata tamaa kwao , wanaibiwa kwa kupitia kutokujua kwao.

Wengi wao shida zao haziondoshwi ingawa mtumishi wa bwana (The man of God ) anaendelea kuneemeka.

Wanaibiwa kwa kutumi jina la yule ambaye alipotakiwa kulipa kodi ilibidi amtume mfuasi wake kupata hela kwenye kinywa cha Samaki.

Wanaibiwa kwa kutumia jina la yule ambaye alikuwa hana mahali pa kulaza ubavu wake .

Huu ninauita wizi wa bila kutumia nguvu.

Wizi huu unatokea sana Africa nzima ambapo waumini kiupofu wanafuata na kutimiza maagizo ya uongozi.

Kwa uaminifu mkubwa wanapanga foleni kununua miujiza kwa njia ya mafuta, maji , chumvi, vitamba nk. Kwa mtu yeyote anayejiita Mtumishi wa Mungu (The man of God).
Wengi wao wakihubiriwa kuwa kuna laana ya ukoo au kizazi ili hali maandiko yanatufundisha kuwa laana zote zilimalizwa pale msalabani .
Changamoto nyingi walizo nazo wakristo wengi Barani Africa kama umaskini na baadhi ya magonjwa,sio za kiroho,bali ni Ujinga.Mafundisho mengi kwa waumini ni juu ya laana ya kizazi au Ukoo (Generational curse) ingawa Mambo mengi ni ujinga wa kizazi au ukoo (Generational ignorance)

Katika Makala yake iliyochapishwa na jarida la Modern Ghana , toleo no.215 la April 2019 Mwandishi Kay Musonda ansema!

Afrika kwa sasa inashuhudia aina mpya ya utumwa kupitia Ukristo (ulokole). Aina hii ya utumwa wa imani imewafanya watu wengi kuwa wavivu wa kufikiri na uwezo wa kutafakari mambo umedumazwa.

Baadhi ya wachungaji wa kilokole wamejipa uungu mtu. Wanapenda kutukuzwa, kuabudiwa na kusujudiwa. Wanajituza wao zaidi kuliko kumtukuza yule wanayemhubiri.

Wachungaji wa aina hii hawawezi kuongelea mafanikio ya watu weusi kama Barack Obama, Serena Williums, na Usain Bolt. Hawawezi kuongelea wagunduzi waliosaidia kutransform dunia kama akina Albert Einstein, Steve Jobs na wengine. Hawawezi kuongelea Wanasayansi waliodedicate maisha yao na wengine kufia maabara wakitafuta dawa za kutibu magonjwa mbalimbali yanayoisumbua Afrika.

Hawawezi kuongea kuhusu wanafasihi vijana kama Chimamanda Ngozi na Ben Okri, au wakongwe kama Chinua Achebe na Ngugi wa Thiong'o.

Kila pembe ya dunia kuna watu waliofanikiwa kutokana na maarifa, bidii, ubunifu, na weledi. Wapo wafanyabiashara, wanasiasa, wanafasihi na hata wanasayansi wanaofanya mambo makubwa ya kuisaidia dunia yetu. Lakini wachungaji wa Afrika hawatawaongelea watu wa aina hii.

Wao wataongelea mtu aliyepata kazi kimiujiza licha ya kukosa sifa za kupata kazi hiyo, kwa sababu tu aliombewa na kupewa mafuta ya upako siku ya interview ya kazi.

Wataongelea kuhusu kijana aliyetoa mshahara wake wote kwa miezi mitatu mfululizo kwa Mchungaji wake kama mbegu ya mafanikio, baadae akawa 'Boss' kazini.

Au wataongelea kuhusu kijana aliyefeli sekondari lakini baada ya baba yake kumalizia ukarabati wa nyumba ya Mchungaji, alipokea barua ya kupata 'admision' chuo kikuu bila hata kurudia mitihani.

Wachungaji hawa hutumia 'miujiza na shuhuda feki' kama njia ya kuwafumba akili wafuasi wao. Kule Afrika kusini kuna Mchungaji alidanganya kufufua mtu. Hata alipoomba msamaha bado kuna waumini wanaendelea kumuamini na kumsujudu.

Wachungaji hawa wamegundua haya ndio mahubiri yanayopendwa sana huku Afrika. Hawataki kuhubiri kuhusu Aliko Dangote alivyoanza biashara na magumu aliyopitia.

Wanahubiri kuhusu mama Janeth aliyekua mama Ntilie huko Enugu, lakini alipotumia mtaji wake wote wa shilingi laki 5 kununua mafuta ya upako kwa Nabii fulani, ghafla biashara yake ikakua na sasa anamiliki mahoteli makubwa pande zote za nchi. Yani bila mtaji, bila business plan, bila timeline ghafla tu akamiliki mahoteli. Na waumini watashangia kwa kusema Ameen.

Aina hii ya ukristo imepanda mbegu ya uvivu wa kufikiri kwa vijana wengi wa Afrika ambao wanalazimishwa kumuona Mungu kama Mfadhili wa wavivu, au wasiostahili. Kwamba mwanafunzi hata asiposoma anajua akipewa mafuta ya upako atafaulu tu siku ya mtihani. Mfanyabiashara hata asipokua mbunifu anajua akienda kwa 'baba wa miujiza' biashara yake itapanuka ghafla bin vuu. Mfanyakazi hata asipowajibika kazini anajua akitoa fungu la kumi kwa 'Dokta Upako' atapanda cheo.

Kwa baadhi ya makanisa Africa namna pekee ya kufanikiwa ni kufanya kile wanachokiita kupanda mbegu, kupaka mafuta ya upako au kunyunyuziwa maji ya baraka. Eti wanaofanikiwa haraka ni watu 30 wa mwazo wanaokimbilia mbele ya kanisa kila mmoja akiwa ameshika noti ya dola 100.

Aina hii ya mahubiri inawafanya watu waamini kwamba Mungu hawapendi wanaojituma na kuwa wabunifu katika kazi, badala yake anawapenda zaidi wanaotoa zaka, sadaka, malimbuko na fungu la 10 hata kama ni wavivu. Hii sio sawa hata kidogo kwa sababu Biblia inakataa uvivu kwa nguvu zote ( *Mithali 12:27 Bali mtu mvivu hapiki Mawindo yake; Bali Mwenye bidii anazo mali za thamani).*
_
Watu wanaaminishwa kwamba ukishatoa sadaka kanisani unaweza kuamka kila siku asubuhi ukapayuka 'Mimi ni Milionea' halafu ukavuta shuka na kuendelea kulala fofofo, ukisubiri sadaka uliyotoa ikupe muujiza wa kuokota hela, ili upate mtaji wa biashara unayoiwaza.

Mtu huna kazi, huna biashara wala wazo la biashara, huna ujuzi, huna elimu, lakini kila siku unashinda kanisani kumsikiliza Mchungaji anayesema kesho utakua milionea na wewe unasema "Baba napokea/Dady I receive". Huu ni utani.

Waambieni wanaofanya utani huu kwa kofia za Uchungaji, Uaskofu, Unabii au Utume kwamba wanamkosea Mungu. Waambieni Mungu wetu ni Mungu wa kanuni, na hana kanuni ya kuwabariki wavivu. Tuache kufundisha waumini wetu kwamba uvivu unalipa kupitia miujiza.

Mafanikio ni matokeo ya bidii, ubunifu na weledi. Biblia inazungumzia kuhusu karama. Hebu kila mtu atumie karama alizopewa kwa bidii, ubunifu na weledi aone kama hatafanikiwa. Sio sahihi kuwaambia watu wabweteke tu na kusubiria mafanikio kama kusubiria daladala kituoni kwa sababu tu wamepakwa mafuta ya upako.

Mungu alishatubariki *tangu wakati wa uumbaji wetu. Ni wajibu wetu kujibidisha katika yale tufanyayo ili baraka zake ziambatane nasi ( *Kumb 28:6 Utabarikiwa uingiapo utabarikiwa na utokapo).*

Wazungu na Wachina wanazidi kushindana katika kuitawala dunia kwenye mambo mbalimbali kuanzia viwanda, biashara, sayansi na teknolojia. Sisi tuko 'busy' kununua maji ya upako tukiamini yatatufanya tuwe kama Jack Ma au Bill Gates. Upuuzi.

Tumeumbwa kuitawala hii dunia (Mwanzo 1:28Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na kila kiumbw chenye uhai kiendacho juu ya nchi). Tutumie vipawa na karama tulizopewa ili kutimiza kusudi hilo la Mungu. Tusiruhusu Askofu, Mchungaji, Nabii, mtume au kiongozi mwingine yeyote wa dini atutawale akili zetu kwa kutuhubiria mafanikio ya miujiza. Wao wanaishi kifahari kwa sadaka za waumini wao, huku waumini wakiendelea kuwa mafukara wa kutupwa.

Biblia inasema kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa ( *Mithali 1:7 Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu).* Tutafute maarifa, tufanye kazi kwa bidii, na tumuabudu Mungu katika Roho na kweli. Kwa kufanya hivyo tutapata MAFANIKIO katika mambo yote tuyafanyayo.

NB: Makala hii inazungumzia baadhi ya makanisa ya kilokole sio yote. Dont generalize. Yapo makanisa ya kilokole yenye misingi bora, lakini mengine yamejaa upotoshaji. Haya ndio yaliyozungumzwa hapa. Tafsiri isiyo rasmi imefanywa
na Malisa GJ.
Tukutane wiki ijayo panapo majaliwa.
 
EINSTEIN112

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Messages
5,583
Points
2,000
EINSTEIN112

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2018
5,583 2,000
Umeandika kishabiki wala sio kwa nia ya kufundisha, bila shaka hata tone ni wewe ni moja ya wafuasi wa watoto wa Hajiri
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
46,253
Points
2,000
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
46,253 2,000
Makanisa yaliojawa na shuhuda.

Huwa sielewi nini maana ya zile shuhuda.

Mtu anatolewa pepo anawekewa mic ili wasikie pepo linaongea.

Siku nzima unashinda kanisani, huna kazi za kufanya.

Upumbavu sana.
 
dronedrake

dronedrake

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2013
Messages
3,867
Points
2,000
dronedrake

dronedrake

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2013
3,867 2,000
mwenye samari atupie hapa
 
Ocran

Ocran

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2017
Messages
819
Points
1,000
Ocran

Ocran

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2017
819 1,000
Binafsi nimemuelewa sana, kiukweli mimi ni mmoja wapo nnayepinga sana huu utaratibu wa baadhi ya makanisa yalivyo sasaivi,mfano mzuri kabisa ni uyo mchungaji aliedanganya kufufua mtu na bado waumini wanaenda ilo kanisa, cha kustaajabu mpaka sasaivi kuna matabaka ya wanaotoa sadaka nyingi na wanao toa sadaka kidogo.
 
GwaB

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Messages
1,313
Points
2,000
GwaB

GwaB

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2014
1,313 2,000
Ni wachache watakaoshawishika kutoa uzoefu wao kulingana na mada hii kwa kudhani kuwa kufanya hivyo ni kukufuru. Maelezo yote haya yanahitimisha maneno yaliyoko kwenye vitabu vya Dini yasemayo hivi; "Watu wangu huangamia kwa kukosa maarifa". Hii ndio maana Afrika imevamiwa na Dini za kila aina na waafrika wamebaki kuwa waumini wanaofuata kama vipofu wakati makanisa yakifungwa huko Ulaya kwa kukosa waumini.

Kuna sehemu moja nchini Rwanda inaitwa "Kibeho", Eneo hili limetangazwa na kanisa katoliki kuwa sehemu takatifu ambapo wanadai kuwa mtawa Maria mtakatifu alionekana hapo kabla ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Wenyeji wa eneo hilo ambako wengi waliuana wenyewe kwa wenyewe, wanaamini kuwa kweli Maria alionekana hapo hata kama hawana ushahidi. kanisa hilo limeendelea kujilimbikizia mapesa kutoka kwa watu masikini ambao ndio wangepaswa kusaidiwa. Hoteli iliyopo hapo kwa ajili ya mahujaji, ina bei mbaya na huwezi kuamini kuwa inafanya biashara. Ama kwa hakika wajinga ndio waliwao!.
 
tinkanyarwele

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Messages
1,445
Points
2,000
tinkanyarwele

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2016
1,445 2,000
Nimekuelewa sana mto mada , hasante
 
Faru Kabula

Faru Kabula

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Messages
12,066
Points
2,000
Faru Kabula

Faru Kabula

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2009
12,066 2,000
Kama wale wanaoshuhudia mafanikio waliyoyapata nao ni sehemu ya hao manabii, basi huo unaweza ukaitwa wizi, lakini kama si sehemu yao, bali walifanikiwa bila kufanya mipango na huyo nabii, basi huo si wizi. Ukweli wanaujua watoa shuhuda, ila jambo la msingi ni kuamini katika Kristu aliye hai na kusadiki kwamba yeye pekee ndio njia, kweli na uzima
 
Faru Kabula

Faru Kabula

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Messages
12,066
Points
2,000
Faru Kabula

Faru Kabula

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2009
12,066 2,000
Kuna sehemu moja nchini Rwanda inaitwa "Kibeho", Eneo hili limetangazwa na kanisa katoliki kuwa sehemu takatifu ambapo wanadai kuwa mtawa Maria mtakatifu alionekana hapo kabla ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Wenyeji wa eneo hilo ambalo wengi waliuana wenyewe kwa wenyewe, wanaamini kuwa kweli Maria alionekana hapo hata kama hawana ushahidi. kanisa hilo limeendelea kujilimbikizia mapesa kutoka kwa watu masikini ambao ndio wangepaswa kusaidiwa. Hoteli iliyopo hapo kwa ajili ya mahujaji, ina bei mbaya na huwezi kuamini kuwa inafanya biashara. Ama kwa hakika wajinga ndio waliwao!.
Nadhani unatafuta kichaka cha kuyaficha maudhui ya mada hii kuhusu ulaghai wa baadhi ya mitume na manabii wa kilokole, kwa kuliingiza Kanisa Katoliki ili ionekane nalo linafanya ulaghai. Hebu soma tena na tena, usilichafue RC Church, halina hizo habari za kutoza hela kwa ajili ya miujiza
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
12,047
Points
2,000
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
12,047 2,000
Nimeituma kama nami livyoikuta namani itawagusa wengi an ndio hali halisi iliyipi kwa sasa.

UTUMWA MPYA NDANI YA KANISA

Pale udadisi unapokwenda likizo (reasoning)
Ndani ya Kanisani,watu kwa kukosa maarifa wanaibiwa. Kwa bahati mbaya hatujifunzi kutoka kwa Wabeloya, hawa walikuwa wadadisi.

Watu wa huko walikuwa wasikivu zaidi kuliko wale wa Thesalonike. Waliupokea ule ujumbe kwa hamu kubwa, wakawa wanayachunguza Maandiko Matakatifu kila siku, ili kuona kama yale waliyosema Paulo na Sila yalikuwa kweli.

Watu Wanaibiwa kwa kupitia magonjwa yao , wanaibiwa kwa kupitia umaskini wao, wanaibiwa kwa kupitia kukata tamaa kwao , wanaibiwa kwa kupitia kutokujua kwao.

Wengi wao shida zao haziondoshwi ingawa mtumishi wa bwana (The man of God ) anaendelea kuneemeka.

Wanaibiwa kwa kutumi jina la yule ambaye alipotakiwa kulipa kodi ilibidi amtume mfuasi wake kupata hela kwenye kinywa cha Samaki.

Wanaibiwa kwa kutumia jina la yule ambaye alikuwa hana mahali pa kulaza ubavu wake .

Huu ninauita wizi wa bila kutumia nguvu.

Wizi huu unatokea sana Africa nzima ambapo waumini kiupofu wanafuata na kutimiza maagizo ya uongozi.

Kwa uaminifu mkubwa wanapanga foleni kununua miujiza kwa njia ya mafuta, maji , chumvi, vitamba nk. Kwa mtu yeyote anayejiita Mtumishi wa Mungu (The man of God).
Wengi wao wakihubiriwa kuwa kuna laana ya ukoo au kizazi ili hali maandiko yanatufundisha kuwa laana zote zilimalizwa pale msalabani .
Changamoto nyingi walizo nazo wakristo wengi Barani Africa kama umaskini na baadhi ya magonjwa,sio za kiroho,bali ni Ujinga.Mafundisho mengi kwa waumini ni juu ya laana ya kizazi au Ukoo (Generational curse) ingawa Mambo mengi ni ujinga wa kizazi au ukoo (Generational ignorance)

Katika Makala yake iliyochapishwa na jarida la Modern Ghana , toleo no.215 la April 2019 Mwandishi Kay Musonda ansema!

Afrika kwa sasa inashuhudia aina mpya ya utumwa kupitia Ukristo (ulokole). Aina hii ya utumwa wa imani imewafanya watu wengi kuwa wavivu wa kufikiri na uwezo wa kutafakari mambo umedumazwa.

Baadhi ya wachungaji wa kilokole wamejipa uungu mtu. Wanapenda kutukuzwa, kuabudiwa na kusujudiwa. Wanajituza wao zaidi kuliko kumtukuza yule wanayemhubiri.

Wachungaji wa aina hii hawawezi kuongelea mafanikio ya watu weusi kama Barack Obama, Serena Williums, na Usain Bolt. Hawawezi kuongelea wagunduzi waliosaidia kutransform dunia kama akina Albert Einstein, Steve Jobs na wengine. Hawawezi kuongelea Wanasayansi waliodedicate maisha yao na wengine kufia maabara wakitafuta dawa za kutibu magonjwa mbalimbali yanayoisumbua Afrika.

Hawawezi kuongea kuhusu wanafasihi vijana kama Chimamanda Ngozi na Ben Okri, au wakongwe kama Chinua Achebe na Ngugi wa Thiong'o.

Kila pembe ya dunia kuna watu waliofanikiwa kutokana na maarifa, bidii, ubunifu, na weledi. Wapo wafanyabiashara, wanasiasa, wanafasihi na hata wanasayansi wanaofanya mambo makubwa ya kuisaidia dunia yetu. Lakini wachungaji wa Afrika hawatawaongelea watu wa aina hii.

Wao wataongelea mtu aliyepata kazi kimiujiza licha ya kukosa sifa za kupata kazi hiyo, kwa sababu tu aliombewa na kupewa mafuta ya upako siku ya interview ya kazi.

Wataongelea kuhusu kijana aliyetoa mshahara wake wote kwa miezi mitatu mfululizo kwa Mchungaji wake kama mbegu ya mafanikio, baadae akawa 'Boss' kazini.

Au wataongelea kuhusu kijana aliyefeli sekondari lakini baada ya baba yake kumalizia ukarabati wa nyumba ya Mchungaji, alipokea barua ya kupata 'admision' chuo kikuu bila hata kurudia mitihani.

Wachungaji hawa hutumia 'miujiza na shuhuda feki' kama njia ya kuwafumba akili wafuasi wao. Kule Afrika kusini kuna Mchungaji alidanganya kufufua mtu. Hata alipoomba msamaha bado kuna waumini wanaendelea kumuamini na kumsujudu.

Wachungaji hawa wamegundua haya ndio mahubiri yanayopendwa sana huku Afrika. Hawataki kuhubiri kuhusu Aliko Dangote alivyoanza biashara na magumu aliyopitia.

Wanahubiri kuhusu mama Janeth aliyekua mama Ntilie huko Enugu, lakini alipotumia mtaji wake wote wa shilingi laki 5 kununua mafuta ya upako kwa Nabii fulani, ghafla biashara yake ikakua na sasa anamiliki mahoteli makubwa pande zote za nchi. Yani bila mtaji, bila business plan, bila timeline ghafla tu akamiliki mahoteli. Na waumini watashangia kwa kusema Ameen.

Aina hii ya ukristo imepanda mbegu ya uvivu wa kufikiri kwa vijana wengi wa Afrika ambao wanalazimishwa kumuona Mungu kama Mfadhili wa wavivu, au wasiostahili. Kwamba mwanafunzi hata asiposoma anajua akipewa mafuta ya upako atafaulu tu siku ya mtihani. Mfanyabiashara hata asipokua mbunifu anajua akienda kwa 'baba wa miujiza' biashara yake itapanuka ghafla bin vuu. Mfanyakazi hata asipowajibika kazini anajua akitoa fungu la kumi kwa 'Dokta Upako' atapanda cheo.

Kwa baadhi ya makanisa Africa namna pekee ya kufanikiwa ni kufanya kile wanachokiita kupanda mbegu, kupaka mafuta ya upako au kunyunyuziwa maji ya baraka. Eti wanaofanikiwa haraka ni watu 30 wa mwazo wanaokimbilia mbele ya kanisa kila mmoja akiwa ameshika noti ya dola 100.

Aina hii ya mahubiri inawafanya watu waamini kwamba Mungu hawapendi wanaojituma na kuwa wabunifu katika kazi, badala yake anawapenda zaidi wanaotoa zaka, sadaka, malimbuko na fungu la 10 hata kama ni wavivu. Hii sio sawa hata kidogo kwa sababu Biblia inakataa uvivu kwa nguvu zote ( *Mithali 12:27 Bali mtu mvivu hapiki Mawindo yake; Bali Mwenye bidii anazo mali za thamani).*
_
Watu wanaaminishwa kwamba ukishatoa sadaka kanisani unaweza kuamka kila siku asubuhi ukapayuka 'Mimi ni Milionea' halafu ukavuta shuka na kuendelea kulala fofofo, ukisubiri sadaka uliyotoa ikupe muujiza wa kuokota hela, ili upate mtaji wa biashara unayoiwaza.

Mtu huna kazi, huna biashara wala wazo la biashara, huna ujuzi, huna elimu, lakini kila siku unashinda kanisani kumsikiliza Mchungaji anayesema kesho utakua milionea na wewe unasema "Baba napokea/Dady I receive". Huu ni utani.

Waambieni wanaofanya utani huu kwa kofia za Uchungaji, Uaskofu, Unabii au Utume kwamba wanamkosea Mungu. Waambieni Mungu wetu ni Mungu wa kanuni, na hana kanuni ya kuwabariki wavivu. Tuache kufundisha waumini wetu kwamba uvivu unalipa kupitia miujiza.

Mafanikio ni matokeo ya bidii, ubunifu na weledi. Biblia inazungumzia kuhusu karama. Hebu kila mtu atumie karama alizopewa kwa bidii, ubunifu na weledi aone kama hatafanikiwa. Sio sahihi kuwaambia watu wabweteke tu na kusubiria mafanikio kama kusubiria daladala kituoni kwa sababu tu wamepakwa mafuta ya upako.

Mungu alishatubariki *tangu wakati wa uumbaji wetu. Ni wajibu wetu kujibidisha katika yale tufanyayo ili baraka zake ziambatane nasi ( *Kumb 28:6 Utabarikiwa uingiapo utabarikiwa na utokapo).*

Wazungu na Wachina wanazidi kushindana katika kuitawala dunia kwenye mambo mbalimbali kuanzia viwanda, biashara, sayansi na teknolojia. Sisi tuko 'busy' kununua maji ya upako tukiamini yatatufanya tuwe kama Jack Ma au Bill Gates. Upuuzi.

Tumeumbwa kuitawala hii dunia (Mwanzo 1:28Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na kila kiumbw chenye uhai kiendacho juu ya nchi). Tutumie vipawa na karama tulizopewa ili kutimiza kusudi hilo la Mungu. Tusiruhusu Askofu, Mchungaji, Nabii, mtume au kiongozi mwingine yeyote wa dini atutawale akili zetu kwa kutuhubiria mafanikio ya miujiza. Wao wanaishi kifahari kwa sadaka za waumini wao, huku waumini wakiendelea kuwa mafukara wa kutupwa.

Biblia inasema kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa ( *Mithali 1:7 Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu).* Tutafute maarifa, tufanye kazi kwa bidii, na tumuabudu Mungu katika Roho na kweli. Kwa kufanya hivyo tutapata MAFANIKIO katika mambo yote tuyafanyayo.

NB: Makala hii inazungumzia baadhi ya makanisa ya kilokole sio yote. Dont generalize. Yapo makanisa ya kilokole yenye misingi bora, lakini mengine yamejaa upotoshaji. Haya ndio yaliyozungumzwa hapa. Tafsiri isiyo rasmi imefanywa
na Malisa GJ.
Tukutane wiki ijayo panapo majaliwa.

Nitasoma kesho
 
GwaB

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Messages
1,313
Points
2,000
GwaB

GwaB

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2014
1,313 2,000
Nadhani unatafuta kichaka cha kuyaficha maudhui ya mada hii kuhusu ulaghai wa mitume na manabii wa kilokole, kwa kuliingiza Kanisa Katoliki ili ionekane nalo linafanya ulaghai. Hebu soma tena na tena, usilichafue RC Church, halina hizo habari za kutoza hela kwa ajili ya miujiza
Nilichokiona huko Kibeho ni utapeli pia, eneo hilo inasadikiwa kuwa kuna muujiza ulitokea wa kuonekana Maria mtakatifu!! ... Kanisa lile ni la kikatoliki ... Tofauti ni kuwa siyo hilo Katoliki unalolinadi wewe..
 
Forum statistics

Threads 1,336,421
Members 512,614
Posts 32,538,879
Top