Utumishi mmefunika kombe? Kwanini Watumishi wa ajira 2014 - 2017 wawekwe daraja moja?

Mnachokifanya sasa sio sawa kuwaweka ajira 2014, 2015, 2016, 2017 kwenye daraja moja bila kuangalia umri kazini. Mnachokifanya sasa ni kusahau miaka watumishi waliopotezewa kwenye masuala ya uhakiki na vyeti feki. Pia kuna ajira 2012 na 2013 walikaa miaka 6 bila kupanda kwa sababu za kilichoitwa uhakiki.

NINI KIFANYIKE?
Ili kusawazisha hili, inatakiwa muhesabu miaka ya mtumishi tangu aajiriwe na daraja ambalo angetakiwa awepo kisha mumuweke hapo.

Mfano: Ajira 2012, 2013 wenye degree sasa wanatakiwa wawe TGS F etc.

Ila hiki mnachokifanya sasa ni sawa na kufunika kombe ili mradi mambo yaende. Je hawa waliopoteza miaka 2, 3, 4 kupisha uhakiki wanafidiwa vipi?

Cc: Waziri - Utumishi
Cc: Katibu Mkuu Kiongozi
Cc: Rais JMT
Kuna wa 2017 waliopandishwa?
 
Mwendazake (R.I.P) alivuruga Sana nchi, ikiwemo sheria na mikataba ya kazi.
Ndio maana wizara zake alizowahi kuongoza zilikuwa zikilipishwa fidia na faini kwenye hukumu za kesi za ndani na nje kwa maamuzi aliyoyafa ya.
 
Ila wewe ni bongolala kabisa, unaweka mtandaoni barua yako ya conf na ukaacha kumb.Na hadharani? Mwajiri wako akuchukulie hatua kali sana.. na kwa hiyo Kumbukumbu Namba huchomoki
Kupanda cheo nayo ni siri?
Jwtz wanapewa vyeo uwanjani kabisa Ikulu au Monduli chuoni tena kwa sherehe kubwa na makamera kibao.
 
Watumishi wameanza zengwe zao sasa yaani mizengwe tu wakipandishwa shida wasipo pandishwa napo shida tu
 
Kha na nyie walimu shukuruni kwa icho mlichokipata,mlikaa miaka mitano bila kupanda misharaha,leo mnapandishwa daraa kwa ajili ya kubadiliashiwa mshahara mnalalamika,Kuweni na shukrani mkiwa kashifu ivyo mnakosea na pia mnawavunja moyo hata kwa uko mbeleni kuja kuwafikiria kuwapandishia tena
 
Back
Top Bottom