Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Kuna waraka ulitolewa mwezi april kuhusu aina ya watumishi wanaostahili kupanda madaraja ya utumishi, lakini naona kila wilaya ikipandisha kivyake bila kujali kigezo kikubwa cha kutumikia daraja kwa miaka minne na utendaji bora wa kazi.
Kwa mfano, kuna ajira mpya za 2012 na 2013 wameenda masomoni mwishoni mwa 2017 na 2018 lakini walikuwa wamekaa vituoni kwa zaidi ya miaka 4 ila unaambiwa hawastahili kupanda. Kwanini?
Kuna wengine walipanda 2013 na wakaenda masomoni mwishoni mwa 2017 na 2018, eti nao hawapandi! Kwanini?
Kuna baadhi ya halmashauri zimepandisha 2012 tu, wengine 2013, wengine 2014, huku wengine wakipandisha wote (2012, 2013 na 2014) ila cha ajabu ni kwamba mshahara haujabadilika! Je, nani alaumiwe? Serikali au Wakurugenzi?
TAMISEMI majibu yenu yanasubiriwa, kwa maana watumishi wakienda kuulizia wilayani wanaambiwa wawaulize TAMISEMI.