Darren2019
JF-Expert Member
- Nov 23, 2019
- 1,112
- 2,379
Nimejaribu kufikiri ni kwanini asilimia kubwa ya fedha za serikali znaishia kwenye matumizi ya kawaida, mojawapo ya sababu niliyoona ni uwepo wa utitiri wa viongozi wengi kwenye ngazi za juu hasa kuanzia wilayani na ukizingatia hawa wanahudumiwa siyo tu mishahara mikubwa bali kuna magari/mafuta, nyumba/malazi, posho za hapa na pale plus ubadhirifu huko maofisini n.k
Ukiangalia wilayani kuna wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala, wenyeviti wa halmashauri n.k
Mkoani, kuna wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa majiji sijui, makatibu tawala, mameya n.k
Ukiangalia majukumu ya hao viongozi yanafanana fanana sana.
Bungeni ndio vile mipesa mingi isiyoendana na ufanisi wa kazi, mbunge mmoja alipwe 12M kwa mwezi, apewe mkopo wa gari 90M, apewe mafuta lita 1000 kila mwezi, apewe pensheni 250M ndani ya miaka mitano, hapo bado wana kamati mbalimbali huko bungeni, uje uweke wakurugenzi wa mashirika na taasisi mbalimbali za serikali, wenyeviti wa bodi na tume mbalimbali.
Wizarani mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu n.k, hivi kuna haja gani ya kuwa na waziri, naibu waziri na katibu mkuu? Na wizara nyingne zina hadi naibu katibu mkuu kwanini tusiwe na mawazIri wataalam ambao pia watakuwa watendaji?
Kwa utitiri huu wa viongozi kwa nchi maskini km Tanzania tutegemee 90% ya bajeti kuishia kwenye matumizi ya kawaida ya kuendesha serikali. JPM aliwahi kuahidi kupunguza ukubwa wa serikali ila alipofika ikulu kumbukumbu zake zikawa zimeliwa na mchwa, ndo kwanza akaanzisha na wizara mpya ambayo hata waziri muhusika hajui majukumu yake...
Enewei...
Tuliambiwa tukilaumu tutoe na pendekezo, kwangu mimi nafikiri hapa ni Katiba mpya tu, labda itasaidia .