Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Kuna mengi yalisemwa kuhusu January kuteuliwa kuwa waziri wa nishati, mojawapo likiwa ni kwamba kulikuwa na msukumo fulani kutoka kwa wazee kwa mama kumpa January wizara hiyo nyeti kama chaguo lake.
Sasa kwangu mimi hilo nililiona lina walakini sana. Sina tatizo na Makamba kuwa waziri, lakini kwa nini wizara ya Nishati ambayo ni nyeti sana? Kwa nini tusiwe na waziri katika wizara hii ambae ana ufahamu angalau na mambo ya sera na utawala katika mambo ya nishati? Hakuna Mtanzania ambae angefaa zaidi sana ya Makamba?
Nikasema ngoja nimpe kinachoitwa the benefit of doubt, kwamba mtu ambae hana kabisa background ya energy policy na management atuongozee hii wizara. Kama nilistaajabishwa na uteuzi wake, nilipata na mshituko na yale aliyofanya mara tu baada ya kuteuliwa. Alibadilisha watendaji nyeti wote wa juu katika wizara hii!
Nikauliza ndugu zangu walio karibu na jikoni - kulikoni? Wengi wakasema hataki kufanya kazi na wateule wa Magufuli. Nikauliza hawataki wale wasio na sifa ambao labda Magufuli aliwateua kwa ukabila na urafiki? Nikaambiwa hapana, wote tu.
Sikuamini. Nikamchukulia Dr. Tito Mwinuka ambae alikuwa Mkurugenzi wa Tanesco, ambae nae January alitaka aondoke. Nikaangalia background yake na kuona Mwinuka ni mtu alikuwa kipanga sana kimasomo. Alisoma PCM, akasomea uhandisi pale UDSM na kufaulu vizuri sana hadi kubakizwa kama lecturer. Akaendelea kupanda hadi kuteuliwa kuwa Mkurugenizi wa Tanesco.
Nilishituka hata zaidi kusikia nani atam-replace Dr. Mwinuka - mtu aliesimamia kampuni ya television channel! Nikajiuliza, hivi tuna tatizo gani? Kweli tunafikiri mtu akifanikiwa kusambaza DSTV nchini atafanikiwa kuongoza Tanesco zaidi sana ya mtu kama Dr. Mwinuka? Siamini. Ngoja muda uni prove wrong.
Sasa nilipofikiria kwamba upande wa pili tuna January, ambae alisomea masomo ya kiingereza na historia sijui, na akaja kuwa mwandishi wa hotuba za Kikwete, na kutokana na ukaribu wake na Kikwete na kuwa mtoto wa Makamba akawa waziri. Leo hii huyu ndio anasema simtaki Mwinuka, aondolewe pale Tanesco. Yaani vijana wa UDSM watakuambia nguini ana dictate injinia aondolewe katika kazi ya uinjinia kwa sababu nyepesi sana!
NIkasikitika sana. Ndipo nikakumbuka ule mtazamo kwamba watu wa masomo ya sayansi wanafanya kazi kubwa sana katika maisha yao ya shule, lakini katika maisha wanakuja kuamuliwa mambo na hao waliowaita manguini au hata wale vilaza wa darasani walioamua kuingia kwenye siasa kwa kuwa hawakua na kitu kingine cha kufanya!
Hebu niambieni labda sioni. Tumepata mafanikio yepi katika utendaji wa wizara ya nishati tangu uteuzi hu wa Samia? Mambo yanazidi kuharibika kila siku katika kipindi hiki kigumu ambacho tunahitaji sana wizara hii iongozwe na mtu mwenye utaalamu wa juu wa sera na utawala katika masuaala ya nishati. Sio mzoefu wa kuandika hotuba. Mama usisubiri mambo yaharibike kabisa.
Nadhani dunia inahitaji mapinduzi ya wasomi wa science na teknolojia na kuondokana na kuamuliwa mambo ya kiufundi na watu ambao hawastahili kufanya maamui katika nyanja hizo!
Nikawaambia wanangu, epukeni kozi ngumu za sayansi. Someni historia na kiingereza mje kuwa waandishi wa hotuba za maraisi na mawaziri hata wa nishati au sayansi na teknolojia!