Makamba Nishati pekee Ilimshinda. Je, Biteko atamudu Nishati na Naibu Waziri Mkuu?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,803
71,229
Nishati imeshaonekana ni wizara ngumu na yenye changamoto nyingi sana kuzimudu ndio maana January Makamba kiuhakika alishindwa kuimudu.

Sasa wizara hiyo amepewa Dotto Biteko, lakini pamoja na ugumu wa wizara hiyo bado kapewa jukumu lingine la kuwa Naibu Waziri mkuu atakayeratibu shughuli za serikali.
Hakika kazi zote hizo ni shughuli pevu, jee Biteko ataweza kweli?

Na huku kwenye Nishati kuliko mshinda Makamba kutapataje ahueni kama sio kuanza kuwa nchi ya giza kama kawa?

Mie nadhani wahusika wamekurupuka tuu katika hili.
 
Ukiona tu Biteko amepewa kofia mbili ujue ameaminiwa, hata hivyo nikitazama kwa makini zaidi naona kile cheo cha NWM ni kama geresha tu, kwasababu hata majukumu yake hayajulikani, hapo Biteko zaidi anatakiwa focus na Nishati.
 
Hiki cheo siyo kipya japo sijawahi kuonaimpact yake kwenye kuongeza tija.
Ninakumbuka Marehemu Mrema kuwahi kuvaa kofia hii enzi ya utawala wa Mzee Mwinyi, sikumbuki kama kuna kilichoongezeka, hata hadhi yake huwa kama haipo hivi.
Kumbukeni hata mazishi ya Mrema, yalikuwa kawaida sana.
Ninafikiri hizi nafasi za kuundaunda kwa sababu Rais anayo mamlaka, kwa upande wangu ni kuongeza gharama na urasimu usio na sababu.
Pengine ndio sababu hatukuwahi kuona Marais wengine waliofuata wakiapply hiyo kwenye tawala zao.
Labda Pengine Waziri Mkuu aliyepo ameomba msaidizi kwa sababu ambazo hatutakiwi kuzijua ingawa inawezekana kwa njia hii ya kumpa cheo hicho, imekuwa rahisi kumtoa kwenye madini alikoonekana anafanya vizuri.
Na zaidi nakumbuka hata Mzee Mwinyi alipompa Mrema ilikuwa kama gia ya kumuondoa au kumpunguzia makali kwenye nafasi aliyokuwa wakati ule, Waziri wa mambo ya ndani. Ni kama hakuwa akifurahishwa na utendaji wa Mrema, japo hata mimi sikuupenda kivile, na kuwa kuna maeneo alifanya vizuri.
Kwani huwa sivutiwi na mtu asiyeheshimu mipaka ya kazi ya kazi yake.
Inakuwa kama unadharirisha utu wa mtu,sijui unamwita kiongozi mbele za watu unampa microphone eti ajieleze huku akizomewa..
 
Back
Top Bottom