Uteuzi wa CEO mpya wa Air Tanzania

Hili shirika limeshakufa kabla kazi haijaanza.
Nadhani walitakiwa kusuka menejiment kwanZa
 
Wafanyakazi wa umma wana uhakika wa mishahara kila mwezi private sector usipojituma na kufanya kazi kwa weledi hauna kazi hivyo watu ujituma sana na ma CEO mengi ujitahidi kufanya kazi kufikia malengo ya kampuni.
Huu ndo mzizi wa fitina huko serikalini aiseeee
 
Bado watu wana akili za Kutawaliwa.... Mashirika Yanaendeshwa kwa system yake kwa Mfano Shirika la Bima la Taifa mfumo wake hata ukimchukua balozi akae department yeyote hawezi shindwa maana mfumo upo yaani unasoma cha kufanya na cha kutokufanya either umamrishe fulani afanye kwa muda muafaka nini aguse nini asiguse so kila mmoja pale anajua wajibu wake... Sasa hapo ATC am sure watakuwa wana mifumo yao pia... na siku hizi c.e.o yeyote maamuzi yake yana limit yake zaidi ya maendeleo hufanywa na body... Mzungu mzungu wtf

No wonder mashirika haya yana hali mbaya, likiwemo Shirika la Bima la Taifa. Mfumo ni nini? Ni kama vile unapendekeza mashirika haya ya kibiashara yaendeshwe kwa utaratibu uleule ulioyafanya yakafa au yakafeli. Biashara imekuwa ya ushindani sana. Ubunifu wa hali ya juu unatakiwa (for this, one needs to be able to attract and retain creative/innovative minds). Unnecessary bureaucracy in the name of mfumo inadumaza ubunifu. Wafanyakazi wanakuwa tu kama robots, sticking to routines or mfumo in your lexicon.
 
Hapa anatakiwa mzungu ambaye hawezi kupoke vi MEMO kutoka kwa nani eti katibu mkuu wa chama ameandika kimemo kuwa mwanaye apewe nafasi kwenye ndege huku hamna hela na nauli, kingine JPM ATCL isiingiliwe na siasa iache iwe huru kabisa ijiendeshe na uongozi wake ujitegemee, vinginevyo tutachekwa sana tu.
ATCL hiyo unayoiona leo ilishapitia kwenye uongozi wa hao wazungu unaowataka. Zamani iliitwa ATC, walipokuja hao wazungu wako ndipo wakabadili jina kuwa ATCL sanjari na kumuondoa Twiga mkiani. Ndio kusema umesahau, au hujui, au ulikuwa hujazaliwa?
 
Hivi Watanzania bado tunamawazo kwamba watu watakaotuletea maendeleo ni watu kutoka nje .ajabu kweli hii!.Mimi ninaamini kwamba wapo watanzania wenye uwezo wa kuongoza ATCL kwa mafanikio makubwa..Tuachane na mawazo mgando ya kutegemea watu wa nje kwa maendeleo yetu."MAENDELEO CHANYA YA TANZANIA YATALETWA NA WATANZANIA WENYEWE".Watu wa nje tunaweza kushirikiana nao kwa baadhi ya mambo mfano kupata teknologia na ujuzi mwingine kwa kupeleka watu wetu huko kwao, kujifunza au kuwaleta hao wataalumu hapa nchini kuwafundisha watu wetu.Sio kila kitu tunakimbilia watu wa nje kutusaidia..Tuwaamini wataalamu wetu wa ndani, tuwapende na serikali iwape ushirikiano wa kila hali.
 
Siku ya uzinduzi watu wapande free kama mabasi ya mwendokasi treni za mwakyembe au daraja la kigamboni
 
Kiukweli awe mtu mwenye kujua anachofanya na awe mbunifu kila wakati.
Ethiopian airlines ina miaka 70 tangia ianzishwe na inamilikiwa 100% na serikali, hiyo inasaidia kwani nchi nyingi ndege zao huyumba kiuchumi labda baada ya majanga lakini Ethiopian inazidi kuwa kubwa.
Hata Emirates imefika hapo kwa sababu ni 100% government na inasimamiwa haswa kwa kuiboresha kila wakati, kweli wazungu wamo waliobobea kwa mikakati ya biashara
 
No wonder mashirika haya yana hali mbaya, likiwemo Shirika la Bima la Taifa. Mfumo ni nini? Ni kama vile unapendekeza mashirika haya ya kibiashara yaendeshwe kwa utaratibu uleule ulioyafanya yakafa au yakafeli. Biashara imekuwa ya ushindani sana. Ubunifu wa hali ya juu unatakiwa (for this, one needs to be able to attract and retain creative/innovative minds). Unnecessary bureaucracy in the name of mfumo inadumaza ubunifu. Wafanyakazi wanakuwa tu kama robots, sticking to routines or mfumo in your lexicon.
Mfumo haudumazi maana una kanuni na bila kanuni Kampuni haiendi mwisho wa siku mtaishia kutumbuana... so mifumo ya makampuni nyingi ni mizuri tatizo ni uaminifu wa wafanayakazi na management pia... kuna watu huwezi wadhania kama wanaiba kumbe ni vibaka hatari makazini bora vibaka wa nje
 
Hivi hamjui tuna wabongo wako vizuri katika hiyo field kuliko mnavyozani. Niwape tu mfano Rwanda Airways inaongozwa na mbongo. Pia mjue shirika hili by hook or any other litainuka kipindi cha mhesmiwa President kwa kuwa nia anayo na uthibiti anao. Hongera watanzania kwa kumchagua mheshimiwa rais.
 
Nasikia tayari serikali imetoa tangazo la kumuajiri CEO mpya wa air Tanzania, serikali iwe makini sana kumuajiri CEO, huyu ndiye anayeandaa dira na mwelekeo wa kampuni,

Anashawishi na anaongoza shirika, naomba serikali imuajiri mtu wa nje kama wazungu wazoefu waliofanya kazi hizi kwa makampuni makubwa na yamekuwa kwa kasi leo hii tunayaona yakiwa na mafanikio makubwa.

ATCL imeshabadilisha ma CEO sijui mara ngapi wote hakuna ambaye utendaji kazi wake umeonekana kuifufua ATCL kazi ilikuwa kuajiri tu huku wakijua hakuna kazi wafanyakazi hao wanazozifanya.

JPM liangalie swala hili utawalaumu watendaji kazi wako bure kumbe mlimchagua mtu ambaye sio sahihi kuisimamia ATCL. ukimchukua CEO mzungu mwenye uwezo mkubwa na umpe pesa ATCL itafukuzana na KQ (Kenya Airways) hapa sio pa kuchezea eti CEO lazima awe mtanzania, na akiwekwa mtanzania nawapa miezi 6 tutampima nitarudi tena hapa kuwapa jibu.

watanzania sio kwamba hatuna uwezo hapana ila tuna katabia flani hivi ndio maana wengi tunapata taabu sana kufanya kazi kwenye mashirika ya kimataifa wengine tunakimbia wengine tuna survive na wengine tunakomaa,

Hapa anatakiwa mzungu ambaye hawezi kupoke vi MEMO kutoka kwa nani eti katibu mkuu wa chama ameandika kimemo kuwa mwanaye apewe nafasi kwenye ndege huku hamna hela na nauli, kingine JPM ATCL isiingiliwe na siasa iache iwe huru kabisa ijiendeshe na uongozi wake ujitegemee, vinginevyo tutachekwa sana tu.
Naunga hoja,na ndege zenyewe kumbe sii za ATCL ni za wakala wa ndege za serikali.
 
Mzungu sio suluhisho bali inatakiwa mtu ambaye ni comitted ,mbunifu na mchapa kazi kama yule bwana wa DAWASCO na kama wamekosa mtu bora huyo bwana apewe ATCL ainyooshe kama alivyonyoosha Dawasco
 
download (1).jpg


Tim Clark ndie CEO wa EMIRATES kwa sasa. Ni muingereza
 
Back
Top Bottom