Uteuzi Mkurugenzi wa TBC, Katibu Mkuu na Naibu Makatibu Wakuu

JK hana sifa za uongozi kiukweli.Hana uteuzi wa kitaaluma bali kumjua mtu.Natoa mfano huu dhahiri.Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Ruvuma mama Christine Ishengoma aliondolewa mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kuharibu kazi mkoani hapo.watu walishangilia kuondoka kwake.Lakini miezi miwili tu toka aondoke,Jk amemrudisha tena kuwa mkuu wa mkoa huo pale pale.Hapa unajifunza nini katika hili?Hakuna mwingine wa kufanya kazi hizo?Ukizingatia kuwa yeye ni mbunge.kazi zote hizi za nini?
 
Ndugu Wanajamii,

Napenda kuunga mkono mabadiliko haya,lakini mabadiliko haya yasiwe ni mabadiliko tu ya nafasi bali yawe mabadiliko ya kuleta tija na ufanisi katika kufanya kazi.
 
Ina maana Luhanjo ndio kaondoka iwapo huyo jamaa Yambesi anakaimu? Maana Luhanjo nae umri ndio umemtupa mkono unless alisign affidavit ya kupunguza miaka ili asistaafu mapema!!

Kwani mtu hawezi ku delegete? akiongea wa chini yake tayari amestaafu!!! looo usiwe na mawazo finyu
 
Hongera Ndugu Mshana,

Lakini fuata nyendo za Tindo za kuleta uhuru wa TBC,bila kuijali serikali ya CCM,maana mwenzio alitolewa kwa sababu za Kisiasa,Je wewe unatafanya nini au ni kuwa tu Kibaraka wa CCM,usiwe hivyo.Timiza wajibu wako kwa Umma.
 
Wanashindwaje kuzitangaza hizi nafasi ili Watanzania waziwanie kwa uwazi, sifa na vigezo vinavyohitajika? Wachache wanaoteuliwa kwa mtindo huu kisha wakafanyakazi kwa kujiamini, kitaaluma na kwa maslahi ya Taifa hasa kwa chombo kama hiki kinachoendeshwa kwa kodi zetu wote. Wabunge wetu mtahoji hili mkirudi mjengoni mwezi JUne? Sheria iliyoianzisha TBC inasemaje kwa nafasi hii? Niliona kikao kilichopita mkihangaika na nafasi ya Chief Court Administrator. Hii je ambayo inatugusa wote?
 
Hongera Bwana Clement Senzota Mwete Mshana, Nenda kafanye alichokutuma aliyekuteua usije ukafuata ya Tido yeye huenda alikuwa hajajua vizuri TBC ni mali ya nani ndiyo maama akaruhusu mijadala nchi nzima japo wamiliki hawakushiriki.

Hiki ndo kitu cha kufurahia katika Tz ya leo yenye matatizo lukuki.Au ndo wale wale.
 
binadamu wema huwatakia mema wenzao! tunawatakia wateule wote afya njema na wakumbuke wamebeba dhamana za uongozi kwa niaba yetu wote,ameen
 
Hongera Bwana Clement Senzota Mwete Mshana, Nenda kafanye alichokutuma aliyekuteua usije ukafuata ya Tido yeye huenda alikuwa hajajua vizuri TBC ni mali ya nani ndiyo maama akaruhusu mijadala nchi nzima japo wamiliki hawakushiriki.

Tido Mhano yuko wapi kwa sasa?namba nijuzwe
 
Picha+no+3.JPG


Wengi wanamjua Mshana toka akiwa TBC (TVT), mimi ni miongoni mwa wachache ambaye tumemfahamu tangu akiwa newsroom ya RTD miaka ilee kabla hata hajapanda mlimani (UD) na kurejea newsroom ya RTD. TVT ilipoanzishwa ndio alikuwa mhariri wa kwanza Mkurugenzi akiwa ni Samwilu Mwafissi.

Mimi nilipata bahati kufanya nae kazi kwa karibu, kwani ni yeye binafsi ndiye aliyenifungulia mlango wa mimi kujiunga TBC mwaka 2000.

Kilichofuatia naomba ni reserve my comments (kutokana na conflict of interest) ila lets hope for the best, people do change for the better of for worse, lets hope Mshana has changed for the better hivyo ataipaisha TBC to an imaginable heights!.

Hongera Clement Mshana!.
 
Uyu jamaa ametokea The Guardian, alikua Director Pale, ni mchapakazi mzuri sana, but tuangalie kama anaweza kuleta equal right kwy iyo media.

Usikurupuke, huyo hajawahi kuwa Mkurugenzi wa The Guardian aliyepo pale anaitwa Kiondo Mshana... no research no right so speak...
 
Bora kamtoa kampeleka huko, huyu jamaa alikua kikwazo sana kwenye maendeleo ya Nishati kwa ujumla. watakoma huko Maji.


Ukiona hivyo, ujue target ni Mwandosya. Jamaa atamwekea zengwe mpaka Mwandosya abwage Manyanga. Mtandao mpya wa wajanja.....
 
Mhh sidhani kama una uhakika na uyasemayo juu ya huyu jamaa "Mshana". Muda mfupi tu aliokaa kama kamishna hapo wizara ya habari, amejionesha kuwa ni mtu wa mfumo wa serikali, ni mtu anayefanya kulingana na nini serikali inataka. Kwa huyu jamaa kuwa pale TBC, vyama vya upinzani vilie tu, masuala ya airtime hayatakuwa sawa na ile ya CCM. Kama nchi nafikiri imerudi nyuma hatua zaidi ya mia kwa kumtosa TIDO MHANDO, alijitahidi kuibadilisha TBC angalau ikaonekana kama ipo kwa ajili ya watanzania wote.
Mkuu nakunaliana na wewe Tido alifanya mengi.Bwana Mshana alikua mkuu wa MAELEZO chombo amabacho tunaweza kusema ni muhimu katika medani za habari Tanzania.Lakini wakati wote kimekua kikisuasua,nivigumu kuamini ya kwamba chombo muhimu kama hicho katika fani ya habari hakina hata website katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia! Hii inamaanisha kwa chama tawala CCM habari sahihi kwa manufaa ya wananchi ni adui wake mkubwa.Kwa maana hiyo kiongozi makini katika nafasi hiyo hatakiwi.Wataweka mtu figure head vyombo hivyo vitakua vikiongozwa kutoka Ikulu na kina Salva Rweyemamu.Tusitegemee kipya.
 
Kwa nini tbc haiko clear kama cnn au bbc au tv za congo na kenya?

Hivi how hard i it kwao kununua kioo cha kuonyesha picha safi?
 
Back
Top Bottom